Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Asolutely wrong Bill. Baada ya Amin alifuata Lule ambaye aliondolewa na kurithiwa na Binaisa.
Binaisa alikuwa 'arrested' na akina Tito Okello.
Ndani ya serikali ya Binaisa Museveni alikuwa waziri wa Ulinzi na kisha kuhamishwa wizara hiyo.
Kabla ya Obote kushinda uchaguzi, uganda ilikuwa inaongozwa na kamati ya muda.
Aliyemondoa Obote ni Museveni. Hadi hapo Lule na Binaisa walikuwa hawana uwezo dhidi ya Obote.
Kusema ya kuwa Binaisa na Lule walimuondoa Obote ili kumkomoa mwalimu na siasa zake si kweli na nadiriki kusema ni upotoshaji wa 'short cut' ili hukumu ipatikane hata kwa mashitaka ya kuunga unga.
Obote aliporudi mara ya pili alifanya mauaji ya raia wengi hasa jimbo la kati. Hata alipotorka na kufika mpakani mwa Kenya, Nyerere hakukubali arudi Tanzania.
Sababu kubwa ya Amin kuvamia Kagera kwa mujibu wake ni madai kuwa Kagera ni sehemu ya Uganda. Alipofanikiwa kupora mali, kuvuruga maisha ya watu wa Kagera, Amin alipandisha bendera ya Uganda na kumteua mkuu mpya wa Wilaya ya Kagera.
Vita ya Kagera inaweza kuwa ni 'failed policy' kama unavyodai. Ni vema basi utueleze ingekuwa wewe upo katika nafasi ya kutoa maamuzi unadhani nini ungefanya wananchi wako wakiwa wameuawa na kufukuzwa katika eneo lao na kipande cha nchi kuchukulia?
Museveni hakumuondoa Obote. Obote alipinduliwa na majeshi yake.