Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

- He was much involved in Africa problems, how about our problems at home bro?

William.

mkuu, with all due respect, sometime I do ask my self. Were you really and seriously contesting for a seat in the EA assembly or you just wanted people to notice your presence after coming back from majuu?

Kwa sababu, maswali mengine unayouliza huwa yananipa shida sana kuamini, kwamba je ungepata ile nafasi ya ubunge ungekuwa unauliza maswali yenye mwelekeo wa mantiki hizo?
Unasema(nyerere)"He was much involved in Africa problems, how about our problems at home bro"?
Kwako wewe uvamizi wa Amini halikuwa tatizo? Na kumuondoa hadi kwake ili asitusumbue tena nalo pia halikuwa suluhisho?
pole sana mkuu.
 
[1] Mwl kumpatia hifadhi Obote ilikuwa kosa ?.

[2] Mwl kuwapatia hifadhi wakimbizi toka Uganda ilikuwa kosa ?.

[3] Wakimbizi toka Uganda walikuwa wakwanza kuivamia Uganda au majeshi ya Uganda walianzisha vita na Tanzania ?.

[4] Idd Amin kuitangazia dunia kwamba Kagera ni sehemu ya Uganda alikuwa sahihi ?.

[5] Mwl[Tanzania] kuipiga Uganda hadi kumwondoa Idd Amini madarakani alifanya vema ?.

Nikipewa majibu ya maswali yangu machache bila kuingiza ushabiki tunaweza kujua kwa uhakika zaidi nani alikuwa mkosaji
 
Kwahiyo mlitaka aachwe madarakani ili arudi?ama aliwanong'oneza kuwa Kagera ni ya Tanzania?
 
Sasa tuamini kilichotokea au kilichopangwa kutokea, mi naona hapa wewe ndio unayepotosha ukweli kwa ajili ya kulinda unachokiamini.samahani aisee, mimi huu nauita ni unafiki na uchonganishi.

Nini kilichotokea na nini kichopangwa kutokea?! Kwani Wanajeshi wa Uganda waliokuwa Tanzania ukimbizini hawakuvuka mpaka na kwenda kufanya jaribio la mapinduzi?! Suala sio kama mapinduzi hayo yalifanikiwa au hayakufanikiwa bali suala ni Tanzania kutumika kama kituo cha mafunzo kwani isingewezekana kuvuka mpaka na kwenda kumpindua Amin bila kufanya maandalizi na mafunzo ya mapinduzi. sasa hapo uchochezi upo wapi?! Au unakataa kwamba hakuna Wanajeshi wa Uganda ambao walivuka na kuingia Uganda kufanya jaribio la mapinduzi?!
 
mkuu unajua kati ya uganda na tanzania ni nani alikuwa mchokozi??

Je? Wajua ni kwanin? Uganda waliitandika tanzania na mpaka kuvuka mipaka??

In short.Nyerere alikuwa swaiba ake sana obote na pind idd amin alipo mpindua abote nyerere hakufurahia kabisa.Hivyo tanzania ilimuhifanyi obote na mkakati kabambe wa kumng'oa idd amin madarakan uliundwa kuna vijana waganda na watanzania walipewa mafunzo na kuanza kumletea choko choko idd amin kwa kuingia uganda na kufanya fujo walivyo fukuzwa walikimbilia tanzania choko choko zikazid wakaenda tena kufanya fujo na wakafanya uharibifu mkubwa sana uganda idd amin akakasirika akawatandika na kuwafukuza mpaka tanzania na kuingia kilomita kazaa tanzania.
Hapo ndipo nyerere alipokuwa anapataka haraka haraka akautangazia umma kwamba idd amin anataka kuitwa baadhi ya ardhi ya tz na kutangaza vita.
Je? Hapo mwenye kosa nani?? Na je? Ni nani hapo ni mchokozi wa mwenzake?

Ndio mana hata kamanda gadafi alimuunga mkono idd amin na kumsaidia kwa sababu uhuni wote alikuwa anaufahamu.
"Kilabise nkukunalaa nti omugga kagera yensalo ya Uganda ne Tanzania" hayo ni maneno yaliyo kuwa yanasikika kutoka radio uganda yakimaanisha, imeonekana wazi kuwa mto kagera ndo mpaka wa Uganda na Tanzania, wakati inatangazwa mwalimu alikuwa bado hajapeleka jeshi lake
 
Kwahiyo mlitaka aachwe madarakani ili arudi?ama aliwanong'oneza kuwa Kagera ni ya Tanzania?

Mkuu jmushi1,
Tujadili KIINI na sio MATOKEO. Isingewezekana kumwacha Amin anaivamia Tanzania bila kumtia adabu lakini bado ukweli unabaki pale pale kwamba kiini cha haya yote ni Tanzania. Inawezekana hapo baadae Amin angeanza uchokozi yeye lakini hadi sasa tunapozungumza, mchokozi alikuwa Nyerere kabla Amin hajafanya uchokozi wa wazi wazi! Suala la Nyerer kumhifadhi Obote sio tatizo lakini suala la kuwaacha waganda waliokuwa wanampinga Amin watumie ardhi ya Tanzania kuendeshea harakati zao lilikuwa ni uchokozi wa hali ya juu ambao Tanzania tuliufanya dhidi ya Uganda ya Amin! Na ndio maana hata OAU hawakuiunga mkono Tanzania pamoja na Nyerere kuitaka OAU imlaani Amin....OAU walifahamu kwamba ni sisi wenyewe ambao tuliingilia masuala ya ndani ya Uganda. Tanzania ilikuwa ni Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika lengo likiwa kuondosha wageni ambao walikuwa wameikalia Afrika lakini hatukuwa na haki ya kuingilia masuala ya nchi nyingine ya Afrika hususani kama matatizo ambayo yalikuwapo ni baina ya wao kwa wao.
 
ndiye aliitia nchi katika janga la umasikini na madeni ambayo mpaka ulimwengu huu utakwisha hatuwezi kulipa

tutaendelea kulipa riba za deni,

sababu ni kumrudisha mkatoliki mlevi mwenzake madarakani
hivi una taarifa kuwa deni la taifa limekuwa zaidi baada ya jk kwenda ikulu, ukilinganisha na Nkapa alivo likuta na alivoliacha?
 
Nini kilichotokea na nini kichopangwa kutokea?! Kwani Wanajeshi wa Uganda waliokuwa Tanzania ukimbizini hawakuvuka mpaka na kwenda kufanya jaribio la mapinduzi?! Suala sio kama mapinduzi hayo yalifanikiwa au hayakufanikiwa bali suala ni Tanzania kutumika kama kituo cha mafunzo kwani isingewezekana kuvuka mpaka na kwenda kumpindua Amin bila kufanya maandalizi na mafunzo ya mapinduzi. sasa hapo uchochezi upo wapi?! Au unakataa kwamba hakuna Wanajeshi wa Uganda ambao walivuka na kuingia Uganda kufanya jaribio la mapinduzi?!
wanajeshi wakimbizi, wakati wanakimbilia Tanzania ni Mwalimu aliyewaita? Baada ya kukimbilia Tanzania ndio walipoteza haki ya kurudi kwao? Idd Amini alichukua hatua gani za kidiplomasia kuwacontain hao wakimbizi? Aliomba ruhusa kuingia Tanzania kuwaangamiza hao wakimbizi? Well, Uwapo wa Amini Kampala ulikuwa na usalama kwetu? Kama jibu ni hapana, Je haukuwa wajibu wetu kuhakikisha anaondoka kampala? Maamuzi yale yamezorotesha mahusiano yetu na Uganda as of today? Ni nini hasa kinatulazimisha kuzungumzia haya sasa, just curiosity au ni agenda ya kuficha kitu, au kuanzia kitu, can some one go straight to the point?

Mbona hamlalamikii mchango wetu kwenye kuwaondoa wakoroni msumbiji? South Africa? au issue ya Uganda ndio pekee yenye loop holes za kumsakamia marehemu?

Sikilizeni, Hii nchi imekuwa na mawaziri wakuu wengi sana, Warioba,Kawawa,Malecera,Lowasa,Sumaye, Pinda,Sokoine n.k Taifa litawaenzi hawa kutokana na namna kwa ujumla linavyochukulia michango yao, Na pia Taifa litawapuuzia au kuwabeza viongozi wote ambao ama walishindwa au wanashindwa kuonyesha misimamo yao ya dhati katika kupigania, kulinda,kuboresha na kuendeleza maslahi ya Taifa hili, Taifa haliwajibiki kwa mtu yeyote yule wakati likitekeleza haki hii wakati wowote ule.
 
[1] Mwl kumpatia hifadhi Obote ilikuwa kosa ?.

[2] Mwl kuwapatia hifadhi wakimbizi toka Uganda ilikuwa kosa ?.

[3] Wakimbizi toka Uganda walikuwa wakwanza kuivamia Uganda au majeshi ya Uganda walianzisha vita na Tanzania ?.

[4] Idd Amin kuitangazia dunia kwamba Kagera ni sehemu ya Uganda alikuwa sahihi ?.

[5] Mwl[Tanzania] kuipiga Uganda hadi kumwondoa Idd Amini madarakani alifanya vema ?.

Nikipewa majibu ya maswali yangu machache bila kuingiza ushabiki tunaweza kujua kwa uhakika zaidi nani alikuwa mkosaji

[1] Mwl kumpatia hifadhi Obote ilikuwa kosa ?.

Haikuwa kosa hata kidogo huku nikiamini alifanya hivyo kwa dhamira ya kibinadamu, kinyume chake ni kosa!

Wakimbizi wa Uganda ndio walikuwa wa kwanza kuivamia Uganda!

[4] Idd Amin kuitangazia dunia kwamba Kagera ni sehemu ya Uganda alikuwa sahihi ?.

Hakukuwa Sahihi kwakuwa Kagera ilikuwa ni sehemu ya Tanzania.

[5] Mwl[Tanzania] kuipiga Uganda hadi kumwondoa Idd Amini madarakani alifanya vema ?.

Hakufanya vema.Busara ya Vita ya vita ya aina ile ni sawa Gulf War ambapo UN ilipitisha Azimio la kuishambulia Iraq ambayo ilikuwa imeikalia Kuwait. Kilichofanyika ni kumwondoa Sadaam toka ardhi ya Kuwait tu na si zaidi ya pale. Kinyume chake, ni uhuni ambao ulifanywa na Geroge Bush JR ambae kwa kutumia kisingizo cha uwepo wa silaha za maangamizi, alihakikisha hadi Sadam anaondoka kabisa madarakani....!! Hivyo basi, ilitosha tu kumwondoa Amin ndani ya mipaka ya Tanzania na sisi kuimarisha mipaka yetu huku tukihakikisha Waganda waliomo ukimbizini hawaitumii ardhi yetu kufanya chokochoko.

Nikipewa majibu ya maswali yangu machache bila kuingiza ushabiki tunaweza kujua kwa uhakika zaidi nani alikuwa mkosaji.
 
NasDaz,labda tujiulize swali la muhimu kwanza,je ni kipi kilianza kati ya imani ya Amin kuwa Kagera ni ya Uganda na mwalimu kuwapokea kina Obote?
 
Last edited by a moderator:
William,
Mimi sijui ukweli juu ya vita hii. Ila umenikumbusha kitu ambacho kimenifanya nicheke, ngoja nikushirikishe. Baba yangu alinisimulia wakati wa vita hivyo, (Sikumbuki vizuri maana ni marehemu kwa sasa) alinitajia jina la mtu kama hili lako la pili (Malecera) au Kawawa, alienda kuwatembelea na akaitisha mkutano akawa anawahimiza na kuwatia moyo, "Piganeni wala msiogope chochote". Ghafla ikakatiza ndege ya kivita ya Uganda, alikimbilia kwenye handaki mara moja. Baada ya hapo aliondoka kabisa eneo lile. Kwa maana hii, ule mkutano haujafungwa mpaka kesho, maana alikatisha mara moja.
Lakini pia kama kuna agenda ya siri alikuwa nayo kiongozi wa nchi wakati huo, kama ulivyohisiwa kwamba ndilo lengo la maada yako, basi hakuwa peke yake, waulizeni hata akina Malecera na wengine waliokuwepo wakati huo, nini kilisababisha waingize wazee wetu vitani.
Mkuu okoa mbavu zangu basi, inamaana huyu junior anaendeleza mkutano hule ambao haukufungwa? tuwasubirie vilembwe wataufunga labda! mkutano unao umli wa miaka 32 sasa, malecela oyeeeeeeee!
 
William, inaonekana una ajenda zako binafsi dhidi ya Baba wa taifa nazo ni kwa nini alimdhibiti vilivyo baba yako na pili ni ajenda ya kidini. Hivyo basi naomba nikuambie tu kwamba propaganda zote chafu dhidi ya Baba wa taifa kamwe hazina nafasi na hazitafanikiwa. Kwa ushauri tu nakusihi ujikite katika mambo ambayo ni relevant na yenye maslahi kwa jamii yote ya kitanzania.[ Mnyisanzu 02.06.2012].
 
aliona raha kumweka yule mkatoliki mlevi pale dar-es salaam akamsaidia kupata askari wa kwenda kufanya hujuma kule kampala , unafikiri amin atafurahia yale .

Angaliwacha waganda wakasolve matatizo yao kwani imngalikuwa nini ??? Si angaliwanasuru kule bukoba na uvamizi??

KAMA ANAVYOSEMA MWENYEWE, "ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuiwacha tena "

baada ya kula nyama za watu kule zanzibar akakimbilia uganda

na alipomaliza huko alishaanza vurugu na kenya kumbuka mambo ya unyang`au

pia alijaribu huko nyuma na malawi lakini kulikuwa kugumu

huyo ndiye mkatoliki nyerere
Kamuzu Banda alikuwa wa imani gani?
 
wanajeshi wakimbizi, wakati wanakimbilia Tanzania ni Mwalimu aliyewaita? Baada ya kukimbilia Tanzania ndio walipoteza haki ya kurudi kwao? Idd Amini alichukua hatua gani za kidiplomasia kuwacontain hao wakimbizi? Aliomba ruhusa kuingia Tanzania kuwaangamiza hao wakimbizi? Well, Uwapo wa Amini Kampala ulikuwa na usalama kwetu? Kama jibu ni hapana, Je haukuwa wajibu wetu kuhakikisha anaondoka kampala? Maamuzi yale yamezorotesha mahusiano yetu na Uganda as of today? Ni nini hasa kinatulazimisha kuzungumzia haya sasa, just curiosity au ni agenda ya kuficha kitu, au kuanzia kitu, can some one go straight to the point?

Acha upotoshaji usio na tija. Nani amesema Waganda hawakuwa na ruhusa ya kurudi kwao?! Ninachosema ni Waganda katika sura ya uanajeshi walioingia Uganda kutokea Tanzania na kwenda kufanya jaribio la mapinduzi na baada ya kushindwa kwa jaribio hilo wakarudi tena Tanzania. Kwa maana nyingine ni kwamba Tanzania ilihifadhi Waganda wanajeshi waliokuwa na lengo la kuipindua serikali ya Amin. Hilo halikubaliki hata kidogo….!!Suala la Tanzanaia kujihusisha na harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika ni suala lililokubalika kisheria. Na usizani kwamba Tanzania ilikurupuka tu from nowhere na kujiweka mbele kwenye suala la ukombozi bali Tanzania ilikuwa ndo Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi ambayo ilikuwa chini ya OAU ambao kama sikosei ilikuwa au iliwahi kuongozwa na Gen. Hasheem Mbita. Hivyo basi suala la Tanzania na ukombozi kusini mwa afrika ilikuwa ni kutekeleza wajibu wake kama Makao Makuu ya Kamati Ya Ukombozi na ndio maana wapigania uhuru kutoka nchoi mbalimbali walipewa hifadhi hapa na kuruhusiwa kuendesha harakati za ukombozi kutokea hapa.

Na kuhusu kama uwepo wa Amin Kampala ilikuwa salama kwetu jibu ni kwamba ilikuwa salama hadi pale Tanzania ilipoamua kuitumia ardhi yake kama uwanja wa mafunzo wa watu waliokuwa wanampinga Amin. Maswali mengine uliyohoji sidhani kama yana msingi....!!!
 
NasDaz,labda tujiulize swali la muhimu kwanza,je ni kipi kilianza kati ya imani ya Amin kuwa Kagera ni ya Uganda na mwalimu kuwapokea kina Obote?

jmushi1,
kitu cha kwanza ni Nyerere kumpokea Obote....lakini nasisitiza, hakuna mtu mwenye akili timamu ambae anaweza kumlaumu Nyerere kwa kumpokea Obote; hata mimi base yangu haipo katika Nyerere kumpokea Obote bali Waganda kuitumia Tanzania kama uwanja wao wa mafunzo huku serikali ikifahamu. Naamini serikali ilifahamu hilo kwavile isingewezekana Waganda waingie nchini mwao na kufanya jaribio la mapinduzi na waliposhindwa wakarudi tena Tanzania bila serikali kufahamu. Kama walifanya njama za mapinduzi kimya kimya, siri ilishafichuka baada ya wao kufurumushwa na wanajeshi watiifu wa Amin. Baada ya hayo kutokea, Nyerere angemfukuza Obote na watu wake kwavile tayari walishauka sheria za ukimbizi.
 
[1] Mwl kumpatia hifadhi Obote ilikuwa kosa ?.

[2] Mwl kuwapatia hifadhi wakimbizi toka Uganda ilikuwa kosa ?.

[3] Wakimbizi toka Uganda walikuwa wakwanza kuivamia Uganda au majeshi ya Uganda walianzisha vita na Tanzania ?.

[4] Idd Amin kuitangazia dunia kwamba Kagera ni sehemu ya Uganda alikuwa sahihi ?.

[5] Mwl[Tanzania] kuipiga Uganda hadi kumwondoa Idd Amini madarakani alifanya vema ?.

Nikipewa majibu ya maswali yangu machache bila kuingiza ushabiki tunaweza kujua kwa uhakika zaidi nani alikuwa mkosaji

Mhe. Ngongo,

Nijaribu kujibu maswali yako, maana nilikuwa mtumishi Serikalini wakati huo:

(1) Hifadhi kwa Obote mwanzoni ilikuwa ni ubinaadam. Lakini Mwalimu alishauriwa Obote aende nchi nyingine, k.m. Switzerlnad ili tuepuke mzozo na Uganda. Nyerere alikataa.

(2) Baada ya kumpatia Obote hifadhi, supporters wake walikimbilia Tz na hakukuwa na namna ya kuepuka kuwahifadhi. Wakati huo Idi Amin alikuwa mbogo; na kuanza ku-eliminate known Obote supporters, kwa hiyo wakaongezeka sana.

(3) Wakimbizi wa Uganda ndio walianza kuvamia Uganda, na nahisi walipata msaada unofficially toka Tz. Hata yule RPC wa Kagera, Hans Poppe aliuawa na Jeshi la Amin na mwili wake ukapelekwa Kampala kwa maonyesho, eti Wachina walikuwa wanatusaidia. Hans Poppe alikuwa Mhehe, chotara wa Kijerumani.

(4) Idi Amin alikosea kutangaza Kagera ni sehemu ya Uganda. Hili lilifanyika miaka mitano au sita baadae, na ilitokana na excesses za udikteta.

(5) Hakukuwa na njia ya kuepuka uvamizi mwingine wa Dictator Idi Amin bila kumtoa madarakani. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima WaTz kwenda mpaka Kampala, na kumsaka popote Uganda alipokimbilia.
 
- Wakuu JF heshima mbele sana, naomba kuuliza tena hivi kulikuwa ana ulazima wa kupiagana Vita na Idd Amin mpaka kumuondoa kwenye madaraka nchini mwake? Yeye alivunja sheria za kimataifa kwa kutuingilia ndani ya mipaka yetu, je na sisi kwa kuvuka mipaka yake pia mbona kama tulijivua nguo kama yeye, yaani tukawa two wrongs!

- I mean kumuondoa tu kwenye ardhi yetu ndio sheria za kimataifa zinavyosema, lakini kwenda mpaka kumuondoa kwenye uongozi wa Taifa lake mbona kama we went too far, na historia ikaishia kutusuta maana tukamuweka Obote, akaishia kuondolewa tena na mwingine, au Great Thinkers mnasema je?

- Na wale mabingwa wa Conspiracy Theories karibuni sana!!

William.

kwa hiyo,ulitaka tumwachie aje atupige hadi Dar es salaam? kama alivyokuwa akijigamba kuwa tutachakaza kagera na mwisho tutawaingilia hadi dar-er-salaam

lengo lilikuwa ni kujilinda na mtu ambae tayari alisha haidi kutaka kuipiga tanzania na wasaidizi wake.maana kama tungemwacha kama utakacho watu wetu ndio wangeumia zaidi,hata tungemtoa ktk mipaka yetu na kumwacha angerejea tena baadae,dawa yake ilikuwa ni moja tu,KUMPIGA
 
Sasa tuamini kilichotokea au kilichopangwa kutokea, mi naona hapa wewe ndio unayepotosha ukweli kwa ajili ya kulinda unachokiamini.samahani aisee, mimi huu nauita ni unafiki na uchonganishi.

Kwa vyovyote itakavyokuwa, Uwapo wa Idd Amini Madarakani Uganda kungeweka security interest za Tanzania Matatani, Kumuondoa ilikuwa maamuzi sahihi bila kujalisha kwamba alituchokoza au hakutuchokoza acheni kufikiria ndani ya box.

Idd Amini alikuwa na close relation na ghadafi, Mwalimu alikwisha kuona madhara ya kuwa close na Taifa lolote linalofungamana na utawala wa ghadafi, kuonyesha kwamba mwalimu alikuwa sahihi angalia madhara ambayo ghadafi ameyaacha africa sasa, Instability ya Mali na Algeria ni matokeo ya interest za ghadafi.

Katika kila taifa ambalo tunalizodoa leo kwamba halina amani na utulivu, matatizo kwenye mataifa hayo yanachangiwa kwa viwango vikubwa na mataifa jirani zao.
Angalia, Burundi, Rwanda, Uganga,Somalia,Sudani,Congo,Mali, kote uko, waasi wanajificha kwenye nchi jirani ama wanapata direct support kutoka nchi za jirani, angalia matatizo yanayoisumbua Nairobi sasa,source ni somalia.

Kama mmeamua kufikiri, ni lazima mfikiri kweli kweli, msisukumwe na hisia zenu ama kuchukua maelezo ya upande mmoja, na nikumbushe kwamba the great thinker as long as Tanzania is concerned is the one who think in the best interest of Tanzania, I do not settle for less than that.

Chuki dhidi ya Mwalimu zinajengwa juu ya dhana dhaifu sana, na yanapata support za watu wenye vichwa vidogo sana, Kwamba Mwalimu aliua watu, which president does not kill, Yes He killed so many people, hata sasa, for the best interest of responsible politics and economical stability of this country, so many people were supposed to have got silenced.

Just like they silenced Balali, Kolimba & CO. Kwa ajiri ya kulinda interest zenu.

Look at Kagame and his Burundi, unazijua siri za kutawalika kwa Burundi wewe. Poor Me. Only the stupid mind will blame the dead.
Unaona sasa....kumbe wewe ndo umedhirisha kwamba unaongelea kuamini kilichopangwa kutokea!!! Kwahiyoo unakiri wazi kwamba Nyerere ndie kiini cha matatizo na alilazimika kumwondoa Amin kwavile tu Amin alikuwa na Close tie na Ghadaff?! Kama ndivyo, basi hilo pia halikubaliki kwakuwa hakuna ushahidi kwamba Amin angeisumbua Tanzania kwavile tu alikuwa na close tie na Ghadaff!!
 
William natamani uje bukoba uone makaburi ya babu zangu na ndugu zangu waliouwawa na majeshi ya Amini. Wewe uko huko mbali na mzee wako wala hukufiwa unakuja na hoja ya kibazaziiiiii............. siku ukifiwa undo utajua uchungu wa kufiwa.
 
Back
Top Bottom