Vita vya Matumizi ya Silaha za masafa Marefu sasa vita imeanza Rasmi!!

Vita vya Matumizi ya Silaha za masafa Marefu sasa vita imeanza Rasmi!!

Wakuu tujongee...Sasa katika kitu kilikuwa kikingojewa na mataifa mengi wakitaka kujua uwezo wa Urusi sasa kinakaribia,hii ni baada ya Ukraine Usiku wa kuamkia leo Kutumia hizo silaha za masafa marefu aina ya(ATACMS)
akilenga miji mikuu iliyopo kalibu na mpaka wa Urusi!!
  • Ukraine imetumia Mfumo wa Makombora wa Masafa marefu uliotengenezwa na Marekani (ATACMS) kugonga kituo cha kijeshi katika eneo la mpaka wa Urusi la Bryansk, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi, baada ya Washington kuondoa vikwazo vya matumizi yao dhidi ya malengo ya Urusi.
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov alisema matumizi ya silaha za masafa marefu aina ya ATACMS kwa Ukraine ya yaliashiria "awamu mpya ya vita vya Magharibi" dhidi ya Urusi na Moscow itachukua "vivyo hivyo".
  • Rais wa Marekani Joe Biden ameidhinisha kutoa mabomu ya ardhini dhidi ya wafanyakazi kwa Ukraine katika kile ambacho kimeonekana kama mabadiliko mengine ya sera kuhusu silaha zinazotolewa kwa Kyiv na utawala wake unaomaliza muda wake, kulingana na ripoti.
  • Pentagon itaitumia Ukraine angalau $275m katika silaha mpya, shirika la habari la Associated Press liliripoti likiwanukuu maafisa wa Marekani.
  • Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, umepokea taarifa za "shambulio kubwa la anga" siku ya Jumatano na litafungwa, Idara ya Masuala ya Ubalozi wa Marekani ilisema katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X.
  • Mifumo ya ulinzi ya anga ya Urusi iliharibu ndege 44 za Ukraine usiku kucha, zikiwemo 20 katika eneo la kaskazini-magharibi la Novgorod na 24 katika maeneo kadhaa ya kati na magharibi, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi.

Kwa habari zaidi PITIA HAPA
Miji mikuu iliyo kalibu, wewe ni kiachaa au ujinga wako kichwani, kalibu ni kitu gani?
 
Usiwe unaropoka man,dunia hii RUSSIA KIVITA NI WAR MACHINE.
Dunia hii taifa lililozoea vita na lenye experience ya vita ni Russia.
Zungumza vyote ila kivita hakuna taifa sio hata hiyo USA yenyewe inaweza kupambana na Russia.
Uliza Korea war USA alikumbana na nini Russia ilipoamua kuisaidia North Korea pamoja na China.
vita dhidi ya Moldova , Georgia na Ukraine ?
 
Hiv unajua karibu nusu ya waukrein ni warusi na karibu mataifa 15 yaliyojimega so wakati urusi anapigana wakati huo mataifa yote yalikuwa ndan yake so Russia anapigana na waukrein ambao kimsingi ni jamii moja inayojuana vizuri. Kuliko westerners
Urusi sio USSR , usichanganye madesa , Urusi na Ukraine wote walikuwa ndani ya USSR na sio ndani ya Urusi
 
Sasa ukisikia kuna vita Ukraine mawazo yako unafkiri vinapigwa wapi eneo gani? maeneo ndio hayo ya Donbas russia amechukua maeneo partially vita inaendelea sasa kama urusi ana majimbo 4 na ametangaza utawala wake na sheria zake kwenye hayo majimbo vita iko wapi? jiongezee na nenda kaangalie ramani hayo ni maeneo ya mpakani mkuu
Russia imeshanyakua majimbo manne na imeshaweka hadi mamluki wake.
Haijalishi kuwa ni mpakani ila ndio yameshanyakuliwa.
Vita inayoendelea ni ya Ukraine kulazimisha kuyarudisha hayo maeneo.
 
Wakati USA ikipigana na Vietnam GDP yake ilikuwa ndogo kuliko ya Vietnam?
Mbona USA aliamua kuachana na hiyo vita bila kufikia malengo yake?
Hali ndivyo ilivyokuwa Afghanistan ya Wataliban, au Somalia ya akina Waria; USA unayemchunuku alichomoa!!
GDP peke yake haiwezi kuwa determinant factor ya kushinda vita; japo ni kigezo muhimu. Fita ni fita mura; havina macho.
🤣

Nyinyi vijana wa 2000 mnamatatizo sana! Afghanistan USA alienda kwa malengo gani mkuu! Unaweza kuyaeleza hapa?
 
Kwa wauza silaha, vita ni michezo kama michezo mingine. Wanacheza wenye ubavu unaokaribiana, kila mtu akipigania malengo yake yenye maslahi makubwa.

Mpambano ni baina ya US + NATO Vs Russia ( hasimu wao wa muda mrefu) uwanja ukiwa ardhi ya Ukrein

Hilo la kutumia masafaa marefu lolionekana mapema, USA amefanya substitution kuweka mshambuliaji anayemuamini zaidi ili angalau aona matokeo yatakuwaje. Kila mara anapofanya sub anaambulia hasara.
Naona kama Russia anaenda kuumizwa kwani enzi zake zilikuwa ni zile enzi Russia ilikuwa ni USSR. Lakini kwa sasa naona hiko ni kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifunzia kunyoa. Hizo nyuklia Putin alizosema zinaweza kutumika ikibidi na kujijengea makontena (shetlers)eti ya kujihifadhi dhidi ya mionzi hatari ya Nukes ni aina fulani ya kichekesho au mkwara wa aina yake.
 
Ni kweli kabisa.

Mtu ukivamiwa na wahalifu Basi una haki zote kabisa za kujihami na kujilinda kwa kutumia njia yoyote ile inayowezekana.
Ni sahihi kabisa ila isije tena kuwa kwa kujihami kwako unapitiliza hadi na wewe unakuwa tena umevamia kwake i.e. unageuka kuwa mvamizi.
Anachafanya Ukraine ni kuharibu na kubomoa vituo vya kijeshi, maghala ya silaha n.k. vya Mrusi ambavyo vilitumika au vinatumika kuwezesha mashambulizi dhidi ya Ukraine na vipo mbali kiasi kwamba inabidi kutumia silaha/makombora ya masafa marefu kitu ambacho mwanzoni alizuiliwa na waliotoa makombora hayo. Kwa kitendo cha kibali kutolewa kwa Ukraine na chap' Ukraine kuanza kuyatumia ndo tunamwona Mrusi akihaha na kutoa vitisho na mikwara ya kutumia Nyuklia ikibidi. Maji yamemfika Mrusi shingoni.
 
Ni vizuri kuendelea kuiheshimu USA na kuipa hadhi yake mkaacha kabisa kuifananisha na vitaifa kama vya Ulaya na ama Ukraine ambayo inaisumbua Russia

Tuandikeni kwa tahadhari wakuu huku tukijua kuwa, jimbo moja tu hapo USA, GDP yake ni sawa na Russia yote!
Sawa mmarekan wa kwa tumbo
 
Naona kama Russia anaenda kuumizwa kwani enzi zake zilikuwa ni zile enzi Russia ilikuwa ni USSR. Lakini kwa sasa naona hiko ni kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifunzia kunyoa. Hizo nyuklia Putin alizosema zinaweza kutumika ikibidi na kujijengea makontena (shetlers)eti ya kujihifadhi dhidi ya mionzi hatari ya Nukes ni aina fulani ya kichekesho au mkwara wa aina yake.
NATO wa micheweni bwana? Wewe ndiye wa kuilecture URUSI?
 
Wee kweli umechanganyikiwa 😃😃😃

Sasa unakuta mtu kama Huyu Ndiye unabishana nae ,like seriously wenzio Kila siku majimbo Yana chukuliwa huko wewe unasema Ukraine kafanikiwa kuwatoa Russia nchini kwake !!
Mmmmh! Hivi anaye lialia kwa sasa ni yupi kati ya Ukraine na Urusi? Hukumwona Mrusi akilalamika kwamba majitu ya masafa marefu yame tumika dhidi yake na kisha akaanza kujihami kwa kujitengenezea Shetlers?
 
Russia Analia Lia !? Yaani mtu aliyeanzisha vita anaanzaje kulia Kwa mfano , Kwanza lengo la Hiyo vita unalijua !? Kama unalijua hauoni kuwa Russia mpaka sasa Ndiye mnufaika maana Ukraine mpaka Leo haijafanikiwa kujiunga na NATO na Hao NATO wenyewe pia wanaogopa kuiingiza Ukraine ktk umoja wao , vita hata tuseme kuwa Leo iiishe hapo mnufaika ni Russia kwanza atabaki na vipande vya ardhi ambavyo amevimega toka Ukraine pili atakuwa amefanikiwa kuizuia Ukraine kujiunga na maadui wake NATO , so Russia anaanzaje kulia Lia Kwa mfano 🤣 🤣

You must kidding
 
Russia imeshanyakua majimbo manne na imeshaweka hadi mamluki wake.
Haijalishi kuwa ni mpakani ila ndio yameshanyakuliwa.
Vita inayoendelea ni ya Ukraine kulazimisha kuyarudisha hayo maeneo.
Sasa kama Ukraine anapigana kurudisha maeneo maana yake vita inapiganwa ndani yake hayo maeneo na ndio maana russia inapiga kelele vita iishe ukraine imuachie hayo majimbo, Lakini Ukraine wameahidi hadi Cremea itarudi kama ilivyo mipaka yao ya asili, wewe tulia utajanambia
 
Usiongope mkuu,Russia haijawahi kupiga kelele kuwa iachiwe hayo maeneo.
Bali iliwahi kutoa masharti ya mazungumzo ya amani ambayo ni Urkaine kuondoa askari wake Kursk na Ukraine kukubali kuwa majimbo yaliyochukuliwa na Russia ni ardhi ya Russia,tofauti na hapo hakuna makubaliano ya amani.
Ukraine kakataa na Russia akasema basi hakuna makubaliano ya amani vita iendelee.
Na hadi sasa Ukraine imepoteza askari wengi kiasi inakamata watu hovyo barabarani kuwaingiza jeshini.
Na Russia inazidi kusonga mbele zaidi.
 
Russia Analia Lia !? Yaani mtu aliyeanzisha vita anaanzaje kulia Kwa mfano , Kwanza lengo la Hiyo vita unalijua !? Kama unalijua hauoni kuwa Russia mpaka sasa Ndiye mnufaika maana Ukraine mpaka Leo haijafanikiwa kujiunga na NATO na Hao NATO wenyewe pia wanaogopa kuiingiza Ukraine ktk umoja wao , vita hata tuseme kuwa Leo iiishe hapo mnufaika ni Russia kwanza atabaki na vipande vya ardhi ambavyo amevimega toka Ukraine pili atakuwa amefanikiwa kuizuia Ukraine kujiunga na maadui wake NATO , so Russia anaanzaje kulia Lia Kwa mfano 🤣 🤣

You must kidding
Tena kamega 18% ya ardhi ya Ukraine ukichanganya na Crimea ni total ya 25+% ya ardhi ya Ukraine.
 
Usiongope mkuu,Russia haijawahi kupiga kelele kuwa iachiwe hayo maeneo.
Bali iliwahi kutoa masharti ya mazungumzo ya amani ambayo ni Urkaine kuondoa askari wake Kursk na Ukraine kukubali kuwa majimbo yaliyochukuliwa na Russia ni ardhi ya Russia,tofauti na hapo hakuna makubaliano ya amani.
Ukraine kakataa na Russia akasema basi hakuna makubaliano ya amani vita iendelee.
Na hadi sasa Ukraine imepoteza askari wengi kiasi inakamata watu hovyo barabarani kuwaingiza jeshini.
Na Russia inazidi kusonga mbele zaidi.
Urusi ilipeleka wanajeshi wake Kyiv wakashinda vita wakatoka, wakasajili vijana wao miaka 18 na 60 kwa nguvu na kuwapeleka vitani wengine wakakimbia wote wakaenda na maji, wakapeleka mpaka wafungwa pia wameuliwa na kama utakumbuka ata mtanzania wenu pia alikufa vitani na vita bado mbichi sasa wamekodi askari elfu 10 kutoka North Korea

Wewe umvivu ata wa kusoma habari, russia anapiga kelele aachiwe hayo majimbo amalize vita,
 
Hizo mambo za Urusi kukodi askari sio zote ni za kweli.
Uwe na akili yenye kuchuja habari sio tu kumeza habari zisizo na uhakika.
North Korea askari hawajakodiwa bali ni makubaliano ya kijeshi yaliyoingiwa baina ya Russia na North Korea.
Kitu ulichokisahau ni kuwa Urusi bado ina active personnel wengi sana.
Yote iliyofanya ni KUZUIA vifo vingi vya active personnel wake jeshini.
Jeshi la Ukraine liko DISMANTLED na hakuna asiyejua humu ndani.
Narudia tena USITUONGOPEE RUSSIA HAIJAWAHI KULALAMIKA NA KUPIGA KELELE IACHIWE HAYO MAENEO.
BALI ILILETA MASHARTI KUWA UKRAINE IKITAKA AMANI BASI IFAHAMU KUWA MAJIMBO YALIYOCHUKULIWA NA URUSI NI YA URUSI.
Usitake kutudanganya hapa.

Hivi unajua kama Hadi Sasa Russia imeshaongeza asilimia zaidi ya 5% katika ardhi zinazonyakuliwa!?
Au unajisahaulisha kuwa Urusi inasonga mbele viunga vya Donbas kila leo!?
Au unataka tukuletee ripoti ya Urusi kusonga mbele zaidi huko Ukraine!??

Hata kama ni ushabiki maandazi sio wa kiasi chako aisee wee ni too much.
 
Back
Top Bottom