Vita vya Matumizi ya Silaha za masafa Marefu sasa vita imeanza Rasmi!!

Ata wewe hukuleta chanzo chochote badala yake ni porojo tu

russia imeingia hayo makubaliano ba north korea baada ya sasa kubakiwa na jeshi lake la akiba tu, wanajesh wengi wa urusi wameshauliwa, wafungwa na hata hao raia aliopeleka na kuwapa mikataba kw nguv waende vitani

kumbuka russia ilipoivamia ukraine tayari urusi walishafanikiwa kuchuku eneo la ardhi la ukraine lenye ukubwa nchi ya Newserland adui akatolewa kyev na kusukumwa huko mpakani

maeneo aliyochukua russia ni partially sio full ndio mana vita ina mwaka wa 3 inaendelea ukraine kurejesha maeneo yao

Lakini mafanikio zaid kwa ukraine ni kuweza kumtoa adui ndani na sasa unaskia huko Kurks eneo la ardhi la russia lishamegwa ni ukraine na askari aliokodi north korea ni kwa ajili ya kuisaidia urusi irudishe hilo eneo lake ambalo jamaa wanasonga mbele tu kuelekea moscow
 
Still unabwabwaja tena aiseeee.
Unajisahaulisha kuwa nyuma ya Ukraine kuna NATO na Kuna askari wao ambao wanaingizwa Kwa mgongo wa mercenaries kuiunga mkono Ukraine.
Umejisahaulisha kuwa mazungumzo ya amani ya Uturuki ndio yaliipooza makali Urusi kushambulia.
Millitary personnel wa Urusi wapo na wapo Kwa idadi kubwa tu,hao askari wa kukodi,kuchukua wafungwa yote ililenga KUZUIA vifo vya wanajeshi wa Urusi Kwa wingi.

Kwahiyo Urusi kuingia makubaliano ya kijeshi na N.Korea ni dhaifu ila Ukraine kusaidiwa na NATO sio udhaifu!???
Maeneo ambayo Urusi amechukua ni maeneo kamili sio ya nusu nusu.
Eneo lililochukuliwa nusu nusu ni DONBAS peke yake.
Urusi imeshanyakua 18% ya ardhi ya Ukraine na anazidi kusonga mbele.
Hapo Kursk hakuna askari wa Ukraine ataepona,mji wa kuingizia msaada wa Sumy umezungukwa,askari walioingia Kursk ndio hao hao hadi sasa na wanazidi kufa Kila leo.
Ukitaka ripoti tunakuletea hapa.
Ingekua Urusi dhaifu isingesonga mbele kuendelea kuchukua maeneo ya Ukraine.
Kila leo Urusi inazidi kuchukua maeneo.
 
Embu soma hii news article kutoka BBC huwenda kidogo ikakurudisha akili.
 
Hii ni habari ya Oktoba 25 imehaririwa tena leo.
Hii ni hali ya Ukraine huko Kursk.
Inasemekana Russia imerudisha 46% ya eneo walilonyakua Ukraine.
Hadi kufikia mwisho wa huu mwaka sidhani kama kutasalia askari wa Ukraine hapo Kursk.
 
Mimi siwezi kufanyia kazi taarifa zinazosemekana kama ulivyoeleza hapo juu, lete vyanzo vya uhakika hapa niweze kukusaidia
Inamaana Hadi THE WASHINGTON POST hauwaamini!?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Mkuu uwe na nyakati njema usinimalize nguvu pasipo na maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…