Vita vya Ukraine: $ 1bn zatolewa kuzuia uhaba wa chakula barani Afrika

Vita vya Ukraine: $ 1bn zatolewa kuzuia uhaba wa chakula barani Afrika

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inapanga kuchangisha $1bn (£759m) katika muda wa wiki moja kusaidia uzalishaji wa kilimo barani Afrika na kulinda bara la Afrika kutokana na uhaba wa chakula unaotokana na uvamizi unaoendelea wa Urusi nchini Ukraine.

Nchi nyingi za Kiafrika zinategemea mataifa hayo mawili yanayopigana kwa usambazaji wao wa nafaka.

Somalia, Benin, Misri na Sudan zinaongoza kwenye orodha ya nchi ambazo zinategemea pakubwa Urusi na Ukraine, huku zaidi ya 70% ya ngano yao ikitoka katika mataifa hayo mawili.

“AfDB inaona ongezeko hili la bei ya ngano, mahindi na maharagwe ya soya kama uwezekano wa kuzidisha uhaba wa chakula na kuongeza mfumuko wa bei,” Rais wa AfDB Akinwumi Adesina alisema.

Mkopeshaji huyo wa kimataifa anasema ataitisha mkutano wa mawaziri wa fedha na kilimo barani Afrika ili kutekeleza mpango huo.

Kupitia mfuko huo, AfDB inalenga kuongeza uzalishaji wa mpunga wa ngano, mahindi na soya kwa kutumia teknolojia zinazostahimili hali ya hewa, zikiwemo aina za mazao zinazostahimili joto na ukame.

Aina ya ngano inayostahimili joto tayari imejaribiwa nchini Sudan na Ethiopia.

Kulingana na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD), angalau mataifa 25 ya Afŕika yanaagiza zaidi ya thuluthi moja ya ngano yao kutoka Russia na Ukrainia.

Kwa hakika, kwa 15 kati yao, sehemu hiyo ni zaidi ya nusu ya matumizi yao ya kila mwaka ya ngano ambayo yanatoka katika mataifa hayo mawili yanayopigana.

BBC Swahili
 
Tengeneza maandazi,chapati, mikate na vitambua na hilo dona lako la mahindi.
Kwani nikivikosa hivyo siishi?? Wengine tumevijulia ukubwani.......kwani kabla ya hapo hakukua na maisha?
 
Kila "Mbuzi" hula sawa na urefu wa kamba yake. ---- Alisema mkuu mmoja.
kabisa mkuu,kuna tobo flani la kupiga hela flani hivi,nipo naonganisha kamba mpaka ifike bandarini,dili liki tiki kwa huruma niliyonayo basi nafungua saccos ya mikopo kwa mabinti kuanzia 18yrs mpaka 21.
 
Hili bara la Afrika sijui lina laana gani? Hizo pesa walishindwa kuwasaidia waafrika wenzao wanaotaabika na vita&ukimbizi na kukosa vyakula, mpka kwenda kumpa mtu wa mbali huko ambaye hata mchango wako kwake ni Uselessness.
..

Mungu atakuwa anaziona akili za waafrika ni hovyo sana, hayo majitu ya Ukraine si ndyo hayo hayo yaliyokuwa yananyanyasa watu weusi wasivuke border?

Kwanza ni aibu eti kinchi cha Ukraine kiwe na uwezo wa kuilisha afrika nzima ktk baadhi ya mazao.

Afrika lini itapata viongoz wenye akili timamu
 
Kwenye shida ndio akili zinaanza kufanya kazi.
Huu ndio mwanzo wa kuacha ujinga na utegemezi kwa afrika.
 
Hili bara la Afrika sijui lina laana gani? Hizo pesa walishindwa kuwasaidia waafrika wenzao wanaotaabika na vita&ukimbizi na kukosa vyakula, mpka kwenda kumpa mtu wa mbali huko ambaye hata mchango wako kwake ni Uselessness.
..

Mungu atakuwa anaziona akili za waafrika ni hovyo sana, hayo majitu ya Ukraine si ndyo hayo hayo yaliyokuwa yananyanyasa watu weusi wasivuke border?

Kwanza ni aibu eti kinchi cha Ukraine kiwe na uwezo wa kuilisha afrika nzima ktk baadhi ya mazao.

Afrika lini itapata viongoz wenye akili timamu
Umesoma mada ukaielewa vizuri kweli mkuu?
 
Back
Top Bottom