Vita ya 3 ya dunia (WW3)

Vita ya 3 ya dunia (WW3)

Vita kuu ya dunia haitotokea, hii vita ya Ukraine imetokea kwa sababu.
Putin alitaka Russia iogopwe duniani kama super power kama hapo awali na iheshimike kama ilivyokuwa awali, pia Putin alitaka kuleta uwiano wa nguvu ya ushawishi katika siasa na jeshi barani ulaya.

Sidhani kama WW3 itatokea na hata ikitokea haitokuwa mbaya na uharibifu na mauaji ya kutisha kama WW2 kwa sababu WW2 ushindi wako ilikuwa ni wingi wa silaha ulizonazo, hivyo vita inaendelea na silaha zinazalishwa, ndio maana engineers walibuni silaha ambazo ni gharama nafuu kutengeneza na pia inatengenezeka kiurahisi, kushinda tengeneza silaha nyingi kuliko adui yako.

Hapo mtachapana hadi mmoja aishiwe kila kitu akubali either uishiwe askari, silaha n.k hivyo ukipata nafasi kumtandika adui unamtandika kisawa sawa hadi anakaa, ndio maana ilikuwa vita ya kutisha sana.

Tanks zilikuwa na vyuma vya kutosha, ile steel yenyewe nzito balaa, zilikuwepo bunduki za mbao, askari walivaa simple kabisa.

Sasa njoo ufananishe na leo, jinsi technology ilivyo,mambo yalivyo complicated.
Kwanza tuanze na mfano wa tank maarufu ya kimarekani ambayo ni Abrams M1, kwanza ina software za kuiendesha, ina mifumo ya optics ambayo ni complex halafu kingine unaweza shangaa ihiki kifaru kinatumia engine ya ndege(jet engine) 😂
Yani kwanza kutengeneza tu hiko kifaru hadi engineers waliosoma rocket science wanahusika, software engineers na wataalamu wa masuala ya optics hatujaongeza wakali wa milipuko n.k sasa watu wenye elimu hizi na walio qualify kuwapata kwa wingi si rahisi sana kwa sababu inachukua miaka mtu kuwa mtaalamu kiasi hiko. Kumbuka Abrams tank inafika 8 millions usd. sio mchezo. Hivyo kwenye vita kuzalisha tanks kama hizi kwa wingi zaidi ni swali la kujiuliza itakuwaje?

Hatujazungumzia jet fighter za leo zilivyo complicated na gharama kuliko hata Abrams M1 tank maradufu kwenye bei, service na tech, madude kama F22 Raptor si mchezo, hebu linganisha na zile ndege za ww2 unaweza kucheka.

Hata ukija kwa askari wa miguu, askari wa leo wana tumia vifaa vya kisasa, bunduki za kisasa , bulletproof vest, na vifaa vingine ambavyo vina high tech na ni gharama sana. Sio sawa na ww2 ambapo eqipments was made to be cheap, reliable, na rahisi kuzalisha.

USA ww2 ilifikisha hadi servicemen milioni 16, kwa leo hilo jambo haliwezekani, kuzalisha gears za kutosha kwa ajili ya askari milioni 16 haiwezekani na haa ikiwezekana ku afford haitowezekana labda askari wapewe manati na mishale. ww2 nchi nyingi ziliweza ku replace losses kwa urahisi lakini kwa leo si kazi nyepesi hata kidogo. Mnamaliza vita wananchi wanaanza kula nyasi kama mbuzi kwa miaka hata 30 flani au zaidi.

Ukitafakari gharama na complexity ya vifaa vitakavyotumika kwenye ww3 ni wazi kila mmoja anaogopa kujiingiza huko. Kingine leo kuna misilaha ya nuclear, hakuna raia anataka kuleta mchezo na nuclear.

Hayo ni maoni yangu kwamba ww3 haitotokea na ikitokea haitozidi ww2.
 
Nuclear weapons are a big deterrent and I believe WW III will never happen. If it does, Homo Sapiens will obliterate himself and make the only planet that is known to support life inhabitable.
I am 100% sure YAHWEH won't let this happen revelation 11:18
 
WW3 tayari ishatokea.

Tatiz la sisi WAAFRIKA tunasubiri mpk MZUNGU aseme kwamba DUNIA imeingia ktk Vita ya 3.

Anaebisha kuhusu Vita ya 3 aje tuelekezane kwa Hoja solid.
Wengine hatujui kama mimi.

Tufundishe mkuu tupate madini
 
Vita ya 3 ya dunia itaanzia Israel, na itaanzishwa na mataifa ya Ukata kuishambulia Israel, ila haitapiganwa kwenye mataifa mengine, itakuwa ni vita kati ya mataifa ya ulaya, middle East, Africa, America dhidi ya Israel, USA itakuja kupata rais ambaye hataitambua Israel ingawa atakuwa rais mwenye asili ya Israel na ndo atatoa kibali cha Israel kushambuliwa baada ya Israel kukaidi na kukata kutimiza matakwa ya USA ya kuunda mataifa 2, Israel na Paledtina, kwa sababu mpango wa nchi 2 itabidi Israel apoteze nusu ya nchi yake na miji muhimu kama Yerusalem, Nazareth, Bethlehem iende Palestine, tajwa hilo Israel atalikata katu na atasema hatuko tayari kutoa ardhi, tuko tayari kwa lolote, na hapo ndi mabomu ya nuclear yatapigwa, Israel ndo ataanza kutumia bomu la nuclear baada ya kuona mashambulizi kutoka kila mahari

Porojo za kitabu Cha Muddy..
 
Wala. Hamna haja ya huenya kuogopa vita vya tatu, kwani hio vita ni stage muhimu sana katika ukuaji wa mwanadamu, hatuwezi kuiruka io stage.

Ikishapigwa ndipo watu wenye mawazo mapya wateule waliobakia watatueleza namna nyingine ya kuishi kama species hata duniaani.

Na kadri inavyochelewa kupigwa ndivyo hivyo hivyo itakavyoleta maafa makubwa zaidi.
 
WW3 haitokuja kutokea mana hakuna nchi inayotaka vita kwenye ardhi yake ndio mana hakuna mbabe atakayempiga mbabe mwenzake.

Mataifa makubwa/wababe wanapigana kupitia migongo ya wengine na hicho kinachofanya WW3 isiwepo.

Mtasikia tuu USA amepeleka makombora Ukraine au Israel ili kumpiga Palestina au Russia lakini kamwe huwezi kuja kusikia USA ameipiga Russia.
Wewe kweli ni kipofu
 
Vita ya 3 ya dunia itaanzia Israel, na itaanzishwa na mataifa ya Ukata kuishambulia Israel, ila haitapiganwa kwenye mataifa mengine, itakuwa ni vita kati ya mataifa ya ulaya, middle East, Africa, America dhidi ya Israel, USA itakuja kupata rais ambaye hataitambua Israel ingawa atakuwa rais mwenye asili ya Israel na ndo atatoa kibali cha Israel kushambuliwa baada ya Israel kukaidi na kukata kutimiza matakwa ya USA ya kuunda mataifa 2, Israel na Paledtina, kwa sababu mpango wa nchi 2 itabidi Israel apoteze nusu ya nchi yake na miji muhimu kama Yerusalem, Nazareth, Bethlehem iende Palestine, tajwa hilo Israel atalikata katu na atasema hatuko tayari kutoa ardhi, tuko tayari kwa lolote, na hapo ndi mabomu ya nuclear yatapigwa, Israel ndo ataanza kutumia bomu la nuclear baada ya kuona mashambulizi kutoka kila mahari
Umeyapata wapi haya?
 
Nuclear weapons are a big deterrent and I believe WW III will never happen. If it does, Homo Sapiens will obliterate himself and make the only planet that is known to support life inhabitable.
Siyo lazima nuclear bomb zitumike ndiyo iwe vita ya 3 ya dunia ...vita vya 3 vinaweza kutokea hata pasipo kutumika bomb la nuclea watu wakapigana na kufa kwa mamilioni bila ya bomu la nuke kutumia cheki ukrain .
 
Nani Alisema hii ya kwanza na hii ya pili na vigezo ni vipi.
Na ya 4 je utakuwa je.
Hata ikija Africa hasa nchi chini ya jangwa LA Sahara kama wakijiingiza basi ni kiherehere Chao tu. We got no business on their problems. Wacha wapigane Wazungu na waarabu wamalizane wenyewe sisi hayatuhusu.
Shida watu wanapenda haya MA-DINI YA KUJA basi huwaambii kitu. Yamekuwa kama majinga.
 
Hakuna mwenye uthubutu WA kutumia nuclear kwa nchi inayomiliki Nuke sababu nae atapigwa tu. Nuke ndo ulinzi utakaofanya watu wakuogope. But watapigana vita ya kawaida labda tu nitokee marekani ashindwe kichapo ndo Kimbilie nuke maana yeye ndio Ana historia akishindwa anakimbilia polisi
 
Ili iitwe vita ya dunia, lazma ugomvi(conflict) utokee baina ya nchi mbalimbali duniani( kuna mpuuzi anasema kama ukraine na russia kwenye hii thread, hapana)
Mapigano pia yanatokea katika sehemu tofauti tofauti hapa duniani.
Na battle inatokea kati ya nchi ambazo zina vinu vya kutosha, tunasema great powers labda marekani na uingereza au china au ujerumani.

Sasa kwann waafrika wanaweza jiingiza. Hizi nchi kubwa waafrica walijiingiza sana kwasababu nchi kubwa zilikua zinataka zifanye expansionism kupata raw materials za mapigano. Lazma tujitetee basi na sisi lazma tungeingia. Na hata sasa. Wakileta fyoko.
Tunawalipua pia. So tunakua kwenye vita.
Pia kwenye vita zilizopita Africa tulikua tunapigana kwa interest ya wale colonial masters wetu.
Sasa nikuunge mkono sehemu hapo.
Saiv itakua ngumu sana kwa vita ya tatu ya dunia ,ngumu sana. Kwasababu hatuna interest yyte sisi kupiga. Labda waturushie bomu.
 
Bisha kwa hoja.. kwanin unabisha.
Labffa kwenye video games na movie mnazoangalia.
Vita kuu ya tatu ya dunia inaweza isitokee na ikitokea basi itakua vita ya kuangamiza. Isiyofaa dunia na matokeo yake yatakua mabaya. Hususan katika karne hii ambayo nchi nyingi zimejitosheleza kimashambuliza.
Unadhani, kilichotokea kati ya ukraine na russia, israel na palestine pale Gaza. Ngoma ziinazopigka kule Congo na jeshi dogo tu la UN na la watanzania wakiwepo, vita ya tatu na criterias za vita zikisema zishuke. Dunia hakutakua na pakukojoa.
Na vita msije sema eti si lazma mtutu utumke. Kwa dunia ya sasa. Mtutu ni lazimaaaaa.
 
Vita ya 3 ya dunia itaanzia Israel, na itaanzishwa na mataifa ya Ukata kuishambulia Israel, ila haitapiganwa kwenye mataifa mengine, itakuwa ni vita kati ya mataifa ya ulaya, middle East, Africa, America dhidi ya Israel, USA itakuja kupata rais ambaye hataitambua Israel ingawa atakuwa rais mwenye asili ya Israel na ndo atatoa kibali cha Israel kushambuliwa baada ya Israel kukaidi na kukata kutimiza matakwa ya USA ya kuunda mataifa 2, Israel na Paledtina, kwa sababu mpango wa nchi 2 itabidi Israel apoteze nusu ya nchi yake na miji muhimu kama Yerusalem, Nazareth, Bethlehem iende Palestine, tajwa hilo Israel atalikata katu na atasema hatuko tayari kutoa ardhi, tuko tayari kwa lolote, na hapo ndi mabomu ya nuclear yatapigwa, Israel ndo ataanza kutumia bomu la nuclear baada ya kuona mashambulizi kutoka kila mahari
KwaNi Betlehemu Kwa Sasa IPO Israeli??? Mbona IPO Palestine???
 
Dunia imeshakumbwa na vita nyingi sana, ila kwa mujibu wa historia zipo vita kuu mbili zilizoigawanya dunia kwenye pande mbili, vita zilizosababisha vifo vya mamilioni ya watu, vita ya kwanza ya dunia(WW1) na vita ya pili ya dunia (WW2).

Tangu kuisha kwa vita ya pili ya dunia mnamo mwaka 1945, dunia bado haijapitia vita kubwa iliyoyagawa mataifa ya dunia katika pande mbili, ila kwa yanayoendelea sasa, kuna uwezekano mkubwa wa dunia kuingia katika vita kubwa ambayo inaweza kupelekea kiama (dunia kufika mwisho).

Je nini mtazamo wako wa vita ya tatu ya dunia(WW3), Kipi kitakuwa chanzo? Na dunia itakuwa na sura gani mara baada ya hii vita kuisha??
Hakujawahi kuwa na vita ya kwanza, ya pili, na hakutakuwa na vita ya 3 ya dunia.
Hivyo ni vita vyao wasitushirikishe, yani mgogoro wa Jumbe na Shaban tuuite mgogoro wa mtaa mzima?

Tuna mambo yetu, mengi tu, tunapambana nayo, waviite white wars
 
Hakuna mwenye uthubutu WA kutumia nuclear kwa nchi inayomiliki Nuke sababu nae atapigwa tu. Nuke ndo ulinzi utakaofanya watu wakuogope. But watapigana vita ya kawaida labda tu nitokee marekani ashindwe kichapo ndo Kimbilie nuke maana yeye ndio Ana historia akishindwa anakimbilia polisi
Ndiyo nilicho sema watu wanakosea kudhani vita ya 3 ni bomu la nuclear.....vita vya 3 vinaweza kupiganwa pasipo kutumika nuke na hivyo vita haviwezi kuwa kwa taifa lenye nuclear kuvamia taifa lenye nuclear lenzake ila vitapiganwa mipakani tu au nchi nyingine kama ilivyo sasa ukrain lakini itakuwa tayari vita ya 3 ya dunia ...matumizi ya nuclear yatakuja tu kwa taifa lenye nuclear litakapi lishinda nguvu taifa lenye nuclear na kuvamia ardhi yake.
 
Back
Top Bottom