Vita ya Clatous Chota Chama Vs Pablo mmoja kuondoka SIMBA

Vita ya Clatous Chota Chama Vs Pablo mmoja kuondoka SIMBA

Chama mpira ulisha Isha. Match zote siku hizi anapuyanga tu. Jiandaeni na Azam, kagera, Geita, mtibwa, mbeya city wako mbele yenu
Na anamzidi magoli Aucho , unadhani Aucho hali yake ipoje kama Chama kaisha?
 
Tetesi kutoka msimbazi ni kuwa kiungo wa Simba,Clatous Chotta Chama na Kocha Mkuu Pablo Franco walirushiana maneno kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Aprili 30, 2022 katika mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya Yanga.

Inaelezwa tukio ndilo lililisababisha Pablo kumtoa Chama na nafasi yake kuchukuliwa na Bwalya, pia katika mchezo dhidi ya Namungo FC, jana Mei 3, 2022, Chama hakuwepo hata kwenye benchi la timu hiyo.

Kutokana na hali hiyo hapo ni wazi wawili hao hawawezi kufanya kazi pamoja na mmoja lazima aondoke, inaaminika kuwa kinachombakisha Pablo mpaka sasa ni kwa kuwa kuna uwezekano wa Simba kukutana na Yanga kwa mara nyingine katika Kombe la FA.

Kama atashindwa kuingia fainali ya FA ni wazi kuwa safari yake itauwa imewadia mapema zaidi ya inavyoelezwa, pia viongozi wa Simba wanaona ameshindwa kuinua viwango vya wachezaji wengi msimu huu.
Bila kuingilia mzozo kati ya Pablo na Chama, Pablo ndio kocha wa hovyo wa Simba katika kipindi cha miaka 4 iliyopita

Vv
 
Basi ngoja nitumie lugha ya kukuna na kupapasa...! Ndani ya misimu miwili, makocha watatu! Bado si haba. Mko vizuri.

Haya mambo tuliyazoea huku kwetu wakati tunakisuka kukosi chetu! Ila kwa sasa naona yamehamia kwenu.
Mtu mzima hovyo!!! Kumbe muliyazoea!!! Sasa cha ajabu ni nini?
 
Aende wapi tena! Kwani si tulikubaliana Pablo ameshawahi kuzifundisha Real Madrid na Getafe! Na hivyo tukimpa muda, ataigeuza timu yetu kuwa Real Madrid ya Bongo!

Mimi naona aendelee tu kubaki mpaka pale mkataba wake utakapokwisha.
Kweli huko kwenu wenye akili ni wawili tu Kama alivyosema fulani.
Huelewi kuwa Katika mikataba tunafungiana malengo ya kufikia? Usipoyafikia ya nini uendelee kugharimiwa?
 
Basi ngoja nitumie lugha ya kukuna na kupapasa...! Ndani ya misimu miwili, makocha watatu! Bado si haba. Mko vizuri.

Haya mambo tuliyazoea huku kwetu wakati tunakisuka kukosi chetu! Ila kwa sasa naona yamehamia kwenu.
kwani kishingo aliondoka msimu upi gomez?
Hebu nidanganye hapa nikuelewe
 
Simba wekeni tofauti pembeni, benchi la ufundi na wachezaji wote kwa ujumla ipambanieni timu tupate matokeo.
Dakika za majeruhi hizi Nguvu Mmoja.
 
Mimi nasema Kaze hafai kuwa hata mbeba mabegi klabuni kwetu akwende tu. Yaani ikitokea akapewa timu amalizie ligi hii Kama kocha mkuu Makolo wanabeba.
 
Pablo asipewe lawama kikosi kiboreshwe kwenye dirisha la usajili Pablo ni mwalimu mzuri sana sema tulifeli kwenye kusajili. Ni sawa na mtu unaetaka upikiwe vzr ilhali uliacha mia5 ya matumizi, kwa kikosi tulichokua nacho hta robo fainali shirikisho tulikua hatustahili
 
Kwa nini ulbadili ID?
Kwanini Jamiiforums wana Kitufe cha Change ID na tena wanaruhusu Kubadili ID Mara tano?

Endeleeni tu kuwa Wapumbavu kwa Kunihisi Mimi ni huyo Mume wenu mumpendae GENTAMYCINE.

Mimi ni MINOCYCLINE Tunu Kuu ya JF.
 
Gentanycin popoma! Umerudi tena, kwa ID nyingine...naomba mod waipige na hii BAN kama ile nyingine sijui imefutwa kabisa au ndio BAN ya mwaka mzima.
Siitwi GENTAMYCINE kama ambavyo Mpunbavu Wewe na Wenzako wengi hapa mnadhani ila naitwa MINOCYCLINE Tunu Kuu ya JamiiForums.

Inaonyesha huyo GENTAMYCINE Wenu akiwa BANNED hapa JamiiForums Wengi wenu ( ukiwemo Juha na Zuzu Mwandamizi Wewe ) huwa Unatajirika, unapanda Cheo Kazini, Miamala yako inasoma, unajazwa Mimba vizuri na Utahaira wako Unapungua au?
 
Back
Top Bottom