Hapa naandika kwa majonzi kwa kusikia jinsi Watanzania wenzetu wanavyougua Corona na wengine kupoteza maisha. Poleni nyote.
Kinachoumiza zaidi ni namna baadhi yetu tunavyoteteana hata kunapokuwa na uzembe kwenye hatua zinazochukuliwa kutulinda na Corona.
Kuna wanaosema Nahodha wetu ni shujaa, mwenye uthubutu na tupo salama ilhali abiria tunaona hatari iliyopo mbele yetu.
Nahodha wetu tunaambiwa yupo mapumzikoni. Je, tukisema kajitosa baharini na kutuachia chombo kielee kwenda kuzama tunakosea?
Corona bila lockdown itatumaliza, ilikuwa Arusha, Dar na Zanzibar hatukuona haja ya lockdown eti tutakufa njaa. Sasa tuna wagonjwa mikoani na hakuna kinachoonekana kufanyika, hatujaamua bado kulock maeneo yenye wagonjwa.
Tunafahamu kuwa hakuna dawa, chanjo, vifaa tiba, maabara za uchunguzi na vifaa vya kujikinga hasa kwa watoa huduma za afya.
Tuamini kuwa tupo salama? Tuamini kuwa Nahodha hajajitosa na kuacha chombo katikati ya mawimbi makali?