Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Lissu si ndio Mgombea wenu wa uraisi au ni Membe?
Wetu Mimi na nani? Hivi mkiulizwa mnaongoza nchi huku mmefumba macho utasemaje?
Kwa taarifa yako Mimi ni abiria wa chombo kinachoenda mrama kwa sababu Nahodha kajitosa,hayo ya Mh.Lissu ni hoja nyingine.

Acha ramli,tusaidiane kumrejesha Nahodha wetu.Kama hataki kazi tuliyompatia atujulishe rasmi tumtafute Nahodha wa ukweli.

Ni bora hats asingekiondoa chombo Bandarini 2015 kama alikuwa anajifahamu yeye mawimbi hayamudu.
 
Badala atoe hotuba nzito ajibu maswali ya waandishi kama wenzetu tujue tumejipanga kiasi gani yeye anang'ang'ana tupurey kwani viongozi wetu wadini hawatuambii tupureyi.

Aje na majibu ya kitaalamu tunatokaje maana mwenzie kakomaa na bakuli sijui hana mia ya kufanya yanayotakiwa kufanywa!! Nunueni mavipimo,maventilators, mabarakoa nk. mtuambie tunazo ngapi na zinahitajika ngapi!!

Huwezi jisifu kununua midege keshi na kuporomosha mireli alafu likija tatizo/zahama unapiga kimya huku unapitisha bakuli!! Nisawa na unajenga maghorofa na unanunua mindinga mikali alafu ukiumwa unakimbilia kupitisha bakuli huku huonekani na husemi binafsi umejitahidi kiwango gani!

Marekani sijaskia wakihangaika na what's up watu wameongea mini au fesibuku wao wanakomaa namambo yamsingi!! Sisi hatutaki MTU kutoa maoni eti ni watatu tuu ndowaseme kyaah!! Kweli tusali hii ngoma ishamnaniliu nahodha
 
Upuuzi mwingine bhana. Alafu kesho mtu kama wewe atakuja bishana na mtu kuwa oooh, urais ni taasisi.
hivi waziri mkuu ambaye alikabidhiwa rasmi hii ishu tena laivu hatukuona? Akaunda timu yake ya kuongoza juu ya hii ishu. Au ishu ni jamaa aoneoane tu ktk tv.? Dah!
Wazir mkuu alienda kwenye daraja kule moro akaamua ya kuamua . Baada ya muda na raisi akaenda na kuamua ya kuamua kwenye hili ana muamini Pm kwakuwa linaua?
Jitafakari na uwe na kumbukumbu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kirengased,
Nimefarijika kiasi kwa sababu sisi baadhi ya abiria tusiosinzia safarini tulimwona Nahodha akichupa majini muda mfupi baada ya dhoruba kuanza kukitingisha chombo,

tumeweza kuwaamsha waliokuwa wamesinzia na sasa wanafahamu kuwa chombo hakina Nahodha ndiyo maana tunatakiwa kujadili kwa dharura;Je,tumtafute Nahodha wa Ukweli mwenye Ujuzi, Weledi na Ujasiri wa kukifikisha Chombo chetu Bandarini sasa?

Mjadala Huu unalengo la kukinusuru chombo chetu(Tanzania),kipo mikononi mwa Nahodha na Mabaharia mahiri?Tujipange maana Corona yaweza kuwa kipimo cha kutambuana kwa rangi zetu halisi kati ya Viongozi na Watawala.

MJADALA UENDELEE tutafute mbinu bora,salama na yenye ufanisi kujikinga na Corona-Kubaki nyumbani ni muhimu mno(StaySafe at your Home).
 
Gellangi,
Mtu mjinga ndio anatoa hoja ya kijinga. Unapokuwa kiongozi na ukakasimu madaraka kwa watu unaowaamini, unakaa unatulia unaangalia wanavyochapa Nazi huku unatoa ushauri wa hapa na pale.

Kwa taarifa yako na wajinga wengine kama wewe, wasaidizi wa Naodha wako imara na Naodha katulia tu. Na hii inadhihirisha namna gani Naodha alivyo thabiti.
 
Msechu na Nasibu kila kukicha wanatupigia kelele, mara nahodha wetu ni jembe, baba lao . Kumbe ni njaa inawasumbua, hakuna lolote la maana ni hovyo kabisaaaaa
 
sweettablet,
Kisheria Unahodha haukaimishwa hovyo hovyo,unakaimisha wakati wa mawimbi na kushika usukani chombo kikitulia majini?

Huo Unahodha ni bora tukampatia hiyo kaimu kama anasifa,kama hana tupo Watanzania zaidi ya 50milioni tutachambua moja wetu atuongozee chombo chetu kitie nanga salama.

Tuchukue hatua.
 
Kisheria Unahodha haukaimishwa hovyo hovyo,unakaimisha wakati wa mawimbi na kushika usukani chombo kikitulia majini?Huo Unahodha ni bora tukampatia hiyo kaimu kama anasifa,kama hana tupo Watanzania zaidi ya 50milioni tutachambua moja wetu atuongozee chombo chetu kitie nanga salama.
Tuchukue hatua.
Nani kasema kakaimisha? Unavijua vyeo vya melini na kazi zake. Unamfahamu First Officer, Second Officer? Unafikiri huwa wanakaimishwa unahodha kisa tu nahodha kapumzika? Kama hujui, uliza weweeee!!!
 
Nyie mifano yenu si mnatoa kwa Trump? Haya Trump kila siku yuko on air akitolea ufafanuzi janga kwa wamarekani.
Trump kila siku yupo kwenye TV akiimba taarab na kuwasuta waandishi wa habari. Usiku anakesha Twitter akiwachamba magavana wanaomtaka atume vifaa na dawa kwenye majimbo yao.

Trump huyu ninayemwona siyo wa kutolea mfano kabisa. Inawezekana kuna mwingine.
 
Ninachokiona kwa sasa umaarufu wa Magufuli umeshuka vibaya sana na kwenye Uchaguzi mkuu kama wasipouchafua basi anguko kuu laja swali ni je watakubali kuachia hatamu?

Au itatubidi turumie njia nyingine ili tuwang'oe ccm waliong'ang'ania madaraka
November hakuna uchaguzi.
 
Nahodha tuliyenaye hafai. Tena akitelekeza chombo hapo labda twaweza pona. Kwa nahodha huyu, bora chombo bila nahodha maana upepo hauna chuki na mtu. Nahodha kajaa chuki na roho mbaya kama nyoka
 
mi sitaki utani nambieni Rais yuko wapi sisi ndiyo tumemwajiri mbona hayuko kazini
Mnataka aje Dar? Akipata korona akifa sasa mtaongozwa na nani? Mwacheni akajifiche mpaka Korona iishe aje awaongoze vizuri.
 
Upuuzi mwingine bhana. Alafu kesho mtu kama wewe atakuja bishana na mtu kuwa oooh, urais ni taasisi.
hivi waziri mkuu ambaye alikabidhiwa rasmi hii ishu tena laivu hatukuona? Akaunda timu yake ya kuongoza juu ya hii ishu. Au ishu ni jamaa aoneoane tu ktk tv.? Dah!
1978 kwenye vita vya kagera sokoine akiwa Prime Minister alikabidhiwa majukumu mengi ila Nyerere alikuwa anatoa update kila siku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Solution ya kupunguza kasi ya usambaaji wa ugonjwa huu siyo ya kisisa bali ni ya kitaalam; hata kama Rais angesimama mbele ya TV kila siku ili aonekane kama ambavyo Trump anavyofanya kila siku bila kuwa njia ya kitabibu ya kuudhibiti, bado ugonjwa utaendelea kusambaa tu kama ambavyo inavyoonekana kwa marekani; na iwapo rais atawaachia watalamu wakaudhibitui bila yeye mwenyewe kupiga kelel kwenye maTV kama ambayo Korea ya kusini ilifanya, ugonjwa utathibitika. Wakati mweningine ni bora Rais asisimame jukwani au kwenye TV kabisa kwa sababu anaweza kuonekana kama anaingiza siasa.

Lockdown ni njia mojawapo, lakini pia kunatakiwa kuwa na upimaji wa jumla kutengansiha walioambukizwa na wazima; huwezi kulock jamii yote kwani kuna mahitaji wanayohitaji ili kuendesha maisha yao kama vili kununua chakula. Ila ukishatengansiaha wagonjwa wote kutoka wazima, na kuadhibiti sehemu maalumu tu, utasaidia sana kupunguza kasi. Unaposubiri mtu aonyehse dalaili ndipo unapokuwa unaruhusu ugonjwa uendelee kusambaa.

Wakati wa kipindupingu miaka hiyo ya themanini na tisini, karantini zilikuwa zinasimamiwa na wakuu wa wilaya na gonjwa lilidhibita; siyo kweli kuwa kila sehemu lazima raisi awepo. Mojawapo ya matatizo ya magufuli ni kule kuonekana katika sehemu zote.
 
Upuuzi mwingine bhana. Alafu kesho mtu kama wewe atakuja bishana na mtu kuwa oooh, urais ni taasisi.
hivi waziri mkuu ambaye alikabidhiwa rasmi hii ishu tena laivu hatukuona? Akaunda timu yake ya kuongoza juu ya hii ishu. Au ishu ni jamaa aoneoane tu ktk tv.? Dah!
anazungumzia lockdown siyo Waziri mkuu, kwani PM ana uwezo wa kuamuru city lockdown?
Mataga mna taabu kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom