Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Nahodha kasema tusali siku tatu....
Lakini bado hajatoa muongozo baada ya siku tatu tufanye nn?....

Kiukweli naona meli inakwenda mrama lkn nahodha hana habari....

Nahodha kanywa mataputapu, kalewa chakari....
Wasaidizi wake wa chombo nao wamelewa zaidi ya nahodha...

Nani atakiokoa chombo?

Au tuzame tu mana wengine hatuna cha kupoteza???
 
Mimi napendekeza kusiwe lockdown ila unapotoka mkoa mmoja kwenda mwingine vipimo vitumike vya kubaini ugonjwa tunapo panda na kushuka kwenye vyombo vya usafiri 'Corona ni hatari inauwa na kuharibu uchumi'
Tatizo liko kwenye "upimaji na uhakika wa hivyo vipimo mkuu" bado lockdown ya mkoa kwa mkoa au kanda kwa kanda inahitajika.

Tusijihadae kwa kukwepa kisichokwepeka bali kila mmoja wetu atimize wajibu wake ili sote tuwe salama.
 
Gellangi,

Watu kama nyie mko wengi hasa humu JF. Mnaongea sana ujinga mpaka mnabore. Ummy Mwalimu anateseka, manurse na madaktari nk. Wanahangaika. Unashindwa hata kuwapongeza unaleta upumbavu wako hapa.

Anza kujilinda. Watu kama nyie ndo wasambazaji. Sijui unawazaga kutumia kiungo gani. Wakati huu wa corona Hakuna shujaaa. Kuongoza nchi yenye nicampoomp like you Ni kazi sana.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo liko kwenye "upimaji na uhakika wa hivyo vipimo mkuu" bado lockdown ya mkoa kwa mkoa au kanda kwa kanda inahitajika...
Tusijihadae kwa kukwepa kisichokwepeka bali kila mmoja wetu atimize wajibu wake ili sote tuwe salama.
Leo nilibahatika kupanda daladala jirani yangu alikuwa anakula, nikamwambia kwa ugonjwa huu wa corona siyo vizuri kula kwenye daladala 'tulikuwa kwenye kiti cha nyuma cha coaster' akasema sawa lakini bado aliendelea kula bagia zake hapa tunajifunza kwamba watu wengi hawana elimu ama nikuishi kwa mazoea
 
Tangu March 28, 2020 alipoonekana Chato akinywa kahawa, hadi leo hajatoka. Pasaka kailia nyumbani, mwezi sasa unakaribia kukata akiwa likizo. Je, huwa ana likizo ya siku ngapi?

Ni jambo jema lakini katika hali kama hii, yeye kama namba moja inabidi awe mfano katika mapambano haya akiwa ikulu ya Dar es salaam kwasababu hajatangaza kuhamia rasmi Dodoma.

Tunakuomba uige kwa Mseven, kwa Kenyatta, pia kwa John Trump wa USA.

93862664_665499170912444_5196215558286082048_o.jpg
 
Kama anavyo mwoga Kwa wapinzani ndivyo alivyo na Kwenye corona pia huyu Mzee ni mwoga wa kila kitu ndiyo maana alivaa mavazi ya jeshi akijifanya kamanda kumbe ni sungusungu Tu....

Kwenye ishu ngumu kama Corona tukimpima raisi wetu dhidi ya Marais wengine wa Africa mashariki utaona jinsi magu alivyopwaya
 
Back
Top Bottom