Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Tangu March 28, 2020 alipoonekana Chato akinywa kahawa, hadi leo hajatoka. Pasaka kailia nyumbani, mwezi sasa unakaribia kukata akiwa likizo. Je, huwa ana likizo ya siku ngapi?

Ni jambo jema lakini katika hali kama hii, yeye kama namba moja inabidi awe mfano katika mapambano haya akiwa ikulu ya Dar es salaam kwasababu hajatangaza kuhamia rasmi Dodoma.

Tunakuomba uige kwa Mseven, kwa Kenyatta, pia kwa John Trump wa USA.

View attachment 1425111
😁😁😁🤣🤣
 
Kusema kweli mh Rais anafanya nini nyumbani?
Tumeshauriwa kuwa tufanye kazi tukiwa nyumbani zaidi. Kwanza kwa sasa hakuna tena wageni wengi kutoka ubalozi wowote. Watakuja na nini nasi tumefunga viwanja vyetu kwa International flights??
Kama ni hao wa jirani zetu kutoka visiwa pendwa vya marashi ya karafuu, hao si walipitia tu wakielekea doma?? Mpaka wamalize mishe zao doma naye atakuwa kesharudi dar
 
Mi namshauri Tundu Antipas Lissu aje faster hata kwa boti kabla huyo dingi hajarudi magogoni
 
Tangu March 28, 2020 alipoonekana Chato akinywa kahawa, hadi leo hajatoka. Pasaka kailia nyumbani, mwezi sasa unakaribia kukata akiwa likizo. Je, huwa ana likizo ya siku ngapi?

Ni jambo jema lakini katika hali kama hii, yeye kama namba moja inabidi awe mfano katika mapambano haya akiwa ikulu ya Dar es salaam kwasababu hajatangaza kuhamia rasmi Dodoma.

Tunakuomba uige kwa Mseven, kwa Kenyatta, pia kwa John Trump wa USA.

View attachment 1425111

Watu Wawili wanastahili Kuwawakilisha Wananchi wote 55+ Million waliopo Tanzania? Halafu hakuna Rais Mseven kama ulivyoandika hapa bali kuna Rais Museveni. Vilevile haijaandikwa mahala popote pale kwamba ni lazima Rais fulani amuige Rais mwingine hasa katika Kukabiliana na Janga hili baya la CORONA. Anaweza akawa kweli hajitokezi Kuzungumza na Wananchi ila akawa anatoa Maelekezo yake ya uhakika kwa Wasaidizi wake hao akina Majaliwa na Ummy na bado mambo yakawa yanaenda vile inavyotakiwa. Halafu Watanzania hatuhitaji Rais ajitokeze hovyo hovyo bali tunahitaji Mikakati Madhubuti ya Serikali kwa Kushirikiana na Wadau juu ya Kulikabili hili tatizo. Na tunaposema kuwa Rais hajitokezi hadharani Kipindi hiki cha hili Janga sidhani kama ni kweli au tunamtendea haki kwani hata hapa juzi kati tu alijitokeza akiwa huko aliko na Kuligusia hili Suala ( Janga ) na Kulitolea Ufafanuzi na hadi Maelekezo mapya. COVID-19 si ya Magufuli pekee bali ni ya Watanzania, wana Afrika Mashariki, wana Afrika na Ulimwengu mzima. Ni kweli Rais Dkt. Magufuli kama Binadamu anaweza akawa na Mapungufu yake ila nasi hasa ( Wanasiasa wa Upinzani ) na Wanaomchukia kwasababu zao / zetu tu Binafsi tumezidi Kumtupia Lawama na Kumshutumu kupita Kiasi.
 
Ulishaabiwa sisi tuna namna tofauti ya kushughulikia corona........
Kujificha chato nayo ni style yetu......
 
Wewe unaona anaongoza? Rais wetu ameamua tufe. Namchukia kuzidi kifani!
Hahaha! Wewe utakufa na presha kama corona haitakupitia.
Yaani huyo rais ndo kwanzaaa anaitafuta nusu ya miaka kumi!!
Wewe kwa hiyo roho yako NGOZI ITAKUBANA MPAKA ITACHANIKA. Yeye yupo sanaa.
 
Tangu March 28, 2020 alipoonekana Chato akinywa kahawa, hadi leo hajatoka. Pasaka kailia nyumbani, mwezi sasa unakaribia kukata akiwa likizo. Je, huwa ana likizo ya siku ngapi?

Ni jambo jema lakini katika hali kama hii, yeye kama namba moja inabidi awe mfano katika mapambano haya akiwa ikulu ya Dar es salaam kwasababu hajatangaza kuhamia rasmi Dodoma.

Tunakuomba uige kwa Mseven, kwa Kenyatta, pia kwa John Trump wa USA.

View attachment 1425111
Ushuzi mtupu

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Msimuonee bure rais jamani. Kovidi inatisha. Rais wa Nigeria ndugu Mohamadou Buhari naye kajificha pamoja na makamu wake. Haijulikani kama nao wamenasa kwasababu marehemu chief of staff Abba Kyari aliyefariki kwa kovidi alikutana nao alipotoka Ujerumani. Yani Safu ya viongozi wote wa juu wako Hibernation.

Hii kitu inatisha isikie tu, policcm hawezi kusaidia ni kujificha tu kwenye maandaki.
Tena Buhari na afya yake! Mungu amjalie afya asiiweke Naijeria katika majaribu
 
Back
Top Bottom