Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Mwalimu Nyerere Hakukaa Ikulu
Alikua anakaa nyumbani kwake masaki.
Ikulu alikua anaenda mara mojamoja
Unataka kunifundisha historian ya nchi hii?Mwl.Nyerere ndiye aliyeishi Magogoni kwa muda Mrefu kulikoni wote.Hill LA kuishi Msasani halipo official, na ndiyo maana alijenga Chamwino,na pia Katiba IPO wazi kuhusu makazi ya Rais.
Naomba ujibu hoja ya Mh.alikuwa akifanya nini Chato?Ilikuwa ni likizo,mapumziko au alikimbia moto wa kaugonjwa.
 
Likizo ya pasaka
 

Uliandika hii mada kufuata upepo wa kisiasa kutaka kuwaaminisha watu serikali haina uwezo au imeshindwa kutulinda wananchi. Mh Rais anazidi kuonyesha ushujaa wake na umakini mkubwa hakika tutavuka salama
 
Ninachokiona kwa sasa umaarufu wa Magufuli umeshuka vibaya sana na kwenye Uchaguzi mkuu kama wasipouchafua basi anguko kuu laja swali ni je watakubali kuachia hatamu?

Au itatubidi turumie njia nyingine ili tuwang'oe ccm waliong'ang'ania madaraka

You are a living legend
 
Mimi simfananishi na nahodha wa chombo mimi namfananisha na dereva wa bajaji ambae ameona simba mbele yake ameachia usukani na kukimbilia siti ya nyuma yaani amekimbia majukumu yake.
Unaweza kufuta huu uchafu chief
 
Chato ishakuwa ni kanchi kengine au ufalme mwingine ndani ya Tanzania.....!!!
Madikteta ni tatizo sana kwa tawala za Kiafrika.
Tafsri tu, hata mwendawazimu anatafsiri zake! Umejitahidi na hongera Kwa mawazo hayo! Ila wenye Ubongo ambao bado unafanya kazi 100% wao wanaiona chatto ni kama sehemu nyingine yoyote hapa nchini!
 
Sasa hivi ndiyo wanataka kuamka,Kila moja anaanza kushangilia.Nahodha ameanza kuonyesha dalili ya kurudi chomboni kushika Usukani.Ni wazo la hekima kuongoza chombo ukishika usukani hata kama pana mawimbi makali kiasi gani.
Kuongoza nchi siyo lelemama,one mistake unaleta madhara makubwa.Tuelekeze katika taratibu zote za kisayansi zilizothibitishwa kuokoa RAIA.COVID is for real,we Tanzanians are not exceptional. We suffer like the rest humans.
Wizara husika ziwajibike tuokoe Watanzania dhidi ya hili janga.Tuache siasa nyepesi za mabeberu na kutuonea kwao here kuingia kwetu uchumi wa kati chini.
Nahodha acha visingizio,ongoza chombo kwa kufuata dira na siyo vinginevyo!
 
Mawimbi yamerejea kwa kasi,Nahodha anadaiwa kashika usukani barabara lakini tunashuhudia chombo kinavyopigwa na dhoruba tunapata hofu hasa kwa kuwa usukani hauonekani kushikwa na mhusika.Tunawashuhudia wasaidizi wake wakipishana kutoa kauli,tatizo ni kuwa wananena kwa lugha na hakuna mkalimani wa hizo lugha.
Tunauliza,Yu wapi Nahodha?
 
Jamani watanzania wenzangu huyu mdudu yupo. Anaejua hizo dalili hapati shida.

Ndugu yangu ameondoka kimasihara. Na nyumba nzima iliugua ila sema waliwahi hosptal.

Huyu ndugu yetu alipuuza wakati tunahisi ndiye alieipeleka nyumbani.

Yaliyompata hadi umauti.
Alirudi saa tano usiku akamwambia mke wake anajisika kifua kinawaka Moto halafu anajisikia Kama malaria. Ilipofika saa Tisa usiku hali ikazidi kuwa mbaya.

Wakamkimbiza dispensary ya karibu, alikaa pale mpaka asubuhi, Madaktari wakamwekea mashine ya kupumua wakati wakati vipimo vinaendelea. Ghafla saa 10 tunaambiwa anatakiwa anahamishiwe Amana hospital. Tukauliza vipimo vonasema anaumwa nini? Wanasema hii ni nemonia. Ukiuliza nemonia ipi ya zamani au ya Sasa? Hatukupata jibu.

Na yeye mwenyewe anaongea. Nasikia alikuwa akiitoa ile mpira aiuliza fasta, ijue huyu mdudu alivyo na Moto.

Pale Amana alikaa siku tatu akatutoka. Mungu ampumzishe kwa amani.
 
Pole kwenu,Nina marafiki waliondokea kwa kuzimika umeme kabla jenereta haijawekwa mafuta tukawa hatunao.Hali ni mbaya ila haturuhusiwi kunena ukweli.Tumezika wengi.
 
Pana mchungaji anawadanganya waumini eti huu ni ugonjwa wa wenye hela.Eti masikini awafi corona,nikasema Mungu amsamehee tu alijui anenalo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…