Flano
JF-Expert Member
- Aug 7, 2019
- 5,446
- 14,880
Mkuu shida ni kwamba inapotokea mvutano wa pande mbili mara nyingi hua propaganda zinatawala kwa kila mtu kuvutia upande wake.Wanajeshi wa Amin walikuwa wanavuka mipaka mara nyingi tu. Mara hiyo walipovuka, Hans Pope kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya mkoa akawepo mpakani, wakati anakimbilia kupiga simu I think ni zile land line ndio wakampiga risasi ya paja. Walimchukua tangu hiyo 1971 wakampeleka Uganda na kwa vile ana asili ya kizungu, Iddi Amin alimtumia kwamba kielelezo cha kibaraka wa mabeberu wanaotaka kuiharibu Uganda. Aliuwawa 1972 na vita ilianza miaka sita baadae
Ila ukiwa na msimamo wa kati na kati inakua ni rahisi kuelewa zaidi.
Mkuu mimi ni mtanzania na ni mzalendo.
Tatizo linapotokea hua nnasimama na nchi yangu kwa hali yoyote na hata hili la vita ya kagera ningekua frontline kumng'oa Iddi Amini kwa hali yoyote.
Ila linapokuja suala la propaganda hua nnajilazimisha kukaa katikati ili kufahamu mambo kwa undani wake zaidi.
Siku Hans pope anapigwa risasi, wanajeshi wa Uganda waliopo mpakani walipotelea Tanzania, sisi tumeaminishwa(propaganda) wanajeshi wale walikua wamelewa chakari kutokana pombe hawakujielewa wakavuka boder na kuingia Tanzania.
Na wale wanajeshi waliompiga risasi Hans Pope walikua wamevuka mpaka na vifaru viwili kuja kuwakomboa wenzao waliokua wamelewa chakari na kupotelea ndani ya mipaka yetu.
Kwa mazingira kama hayo ukiwa makini ukaacha kuendeshwa na propaganda utajua kulikua na nini behind the scene.