Vita ya Kagera: Nimemaliza kutoa Mahari, Simu inaita naambiwa haraka niende Vitani

Vita ya Kagera: Nimemaliza kutoa Mahari, Simu inaita naambiwa haraka niende Vitani

Ikimaliza form six njoo nikuonyeshe infinix yangu ya mwaka 1972 hapa msange 😡😡😡😡
 
Ilikuepo kitu kinaitwa police message au police call
 
Wallah hili lilikuwa ni moja ya jaribu zito maishani mwangu. Baada ya kukata ile simu nlikuwa kama nimemwagiwa maji ya baridi. Nlinywea.... Nakumbuka mshenga na mjomba wangu walikuwa wa kwanza kuniuliza "Yusuf umepatwa na nini ?"

Nlianza kuwaza ina maana sasa yule binti nitamwoa au inakuaje? Mara tena simu ikaanza ku vibrate.....safari hii sikutaka hata kufikiria kupokea. Ili vibrate kama mara 20 hivi nikaona isiwe kesi ngoja nipokeee ila nijifanye nimelala naumwa.

Nilipopokea nilisabahiwa na tusi kwanza " we falah unajifikiria kupokea simu upo juu ya demu nini?"

Kabla.sijajibu rafiki yangu Majariwa aliendelea. " Mwanangu kaza matakoh....tunaondoka.wote kwenda Kagera Idd Amin kavamia Tz. Nawe jina lako limetAjwa katika wanaoondoka. Fanya fanya tusepe kesho"

Nlimshanga Majariwa anaongea kama jambo la kufurahisha wakati mwenzie ndo nimetoka kulipa mahari....nikawaza hapa nisije nikawa mahari nimewalipia watu wengine....sikuwa na namna. Nikarudi ndani ukweni nikiwa na mawazo mengi sana....

ITAENDELEA.....
Kumbe miaka ile kulikua na simu za mkononi eeh?
 
Samahani kama ntatoka nje ya mada mimi naomba nikuulize kipindi hicho vita ya kagera inaanza utakuwa na kumbukumbu katibu mkuu wizara ya ulinzi kwa wakati huo alikuwa nani?

Maana babu yangu mzaa mama inasemekana alikuwa na cheo hicho naomba nipate confirmation kwa yeyote anayejua system ya uongozi ilivyokuwa kipindi hicho najua wahenga mko na uwezo mkubwa wa kukumbuka.
 
Back
Top Bottom