Vita ya kisiasa baina ya Tanganyika na Zanzibar ipo wazi sasa

hicho kitu hakipo, ni either 3 au watu wagawane mbao
Naomba tu ufafanue, hizo tatu ni za nini hasa!.
Bado tu huridhiki na EAC na SADC na sasa hizo zinazoitwa 'Tri-partite', sijui na matakataka mengi mengine? Haya yote ni ya nini kama siyo kuvuruga tu akili za watu.
 
Heshima sana wanajamvi,

Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ambao uliasisiwa na watu wawili ambao sasa hawapo, tena bila ridhaa ya wananchi wa pande zote mbili sasa unapitia katika msuko suko mkubwa.

Ni wazi Mwl Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume waliziunganisha zao Tanganyika na Zanzibar pasipo ridhaa za wananchi wa pande zote mbili.

Muungano wao (Nyerere & Karume) kwa hakika umejaa kasoro nyingi mno, kuubadili au kuufanyia marekebisho kutahitaji kuzifumua katiba za nchi zote mbili jambo ambalo kwa sasa ni vigumu sana.

Zanzibar wana serekali yao, wana bunge lao, wana wimbo wao wa taifa lao, wana bendera yao, wana uraia wao (Uzanzibari), wana mkuu wao wa nchi, wana ardhi yao (nchi) wana kila kitu chao.

Tanganyika hawana wimbo wa taifa, hawana mkuu wao wa nchi, hawana ardhi yao, hawana bendera yao, kifupi Tanganyika hawana chochote.

Kuna Taifa la Tanzania (JMT) ambalo limepora kila kitu cha nchi ya Tanganyika. Bendera? Wimbo wa taifa, Bunge.

Tanganyika haina mtetezi wa rasilimali zake eg misitu, ardhi, bandari.

Raia wa nchi ya Zanzibar anaiongoza Tanganyika kupitia mgongo wa Muungano anauza kila rasilimali ya Tanganyika bila huruma kwakuwa hazina mtetezi.

Watanganyika wameamka sasa lugha ya Mch. Mtikila na sasa Mheshimiwa Lissu imeanza kueleweka hadi ndani ya CCM. Ugomvi mkubwa wa Kinana, Makamba na wanaCCM wengi ni Tanganyika kutawaliwa na Rais kutokea nchi ya Zanzibar ambaye amekuwa dalali mkubwa wa kuuza rasilimali za Tanganyika.

Wanaoitaka Tanganyika sasa ni Watanganyika wote bila kujali mipaka ya vyama.

Ngongo kwasasa Mjini Magharibi.

Pia soma
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Marekani ili ungana kwa kura ya wananchi??

inaonekana hujui unachoongea
 
Huu mjadala nautaka sana, na ninajuwa wewe na mimi hatupo mbali mbali kuhusu hili swala la huu muungano wetu.
Nikukumbushe pia, siyo muda kitambo sana tumejadili haya haya; hasa kuhusu "waZanzibar kutoutaka muungano", jambo ambalo hatukuafikiana juu yake.

Msingi wangu wa kutaka serikali moja ni ule ule, uliokuwepo tangu kuasisiwa kwa muungano wenyewe. Lengo lilikuwa kufikia serikali moja baada ya hofu za "kumezwa" kufifia.
Hoja yangu ni kwamba hiyo hofu ya Zanzibar kumezwa haipo tena; kwani wengi wao tayari tunao hapa hapa Tanganyika. Hawa ni waTanzania, siyo waZanzibar tena.

Kelele za kikundi kidogo cha akina OMO na maJussa hakiwezi kamwe kuwa ndicho kiwe na uwezo wa kuamua hatma ya Tanzania.
Kwa bahati mbaya sana, CCM ndiyo imekuwa mlezi mkuu wa hiki kikundi na kusababisha hata waZanzibari walikokuwa tayari kuwa waTanzania kuanza kuwa na mashaka juu ya hatua hiyo. Kwa hiyo, kuondoka kwa CCM; kazi ambayo waTanzania sasa wapo ayari kabisa kuitekeleza kukiwepo na uongozi imara, hiyo ndiyo hatua muhimu itakayo tuelekeza kwenye serikali moja.
Serikali tatu, ni za nini tena! Miungano ya aina hiyo tuishiriki tukiwa huko kwenye EAC au huko SADC.

Ni matumaini yangu utaelewa msingi huu wa hoja yangu; na kusema kweli sidhani kuwa nitakuwa na hoja zaidi nje ya msingi huu katika majadiliano haya. Kwa hiyo naomba tusiyapanue sana bila ya sababu, kwa vile tunayo mambo mengine ambayo yanahitaji muda wetu.
Mkuu
Ni kweli Wazanzibar wengi wanaishi Tanganyika kama Watanzania. Hofu ya 'kumezwa' ilitakiwa imalizwe na waasisi , lakini historia inatueleza Nyerere na Karume hawakuwa pamoja kwasababu ya identity.

Muungano uliundwa kama ''marriage for convinience' kwa matumaini ya ''assimilation '' hilo halikutokea badala yake ufa unapanuka zaidi

Akina OMO si kikundi kidogo.
Mfano, Mbunge wa ACT kutoka kwa OMO alisimama Bungeni na kuukana Utanzania.
Hakuna! hakuna ! Mbunge hata mmoja wa Zanzibar aliyesimama na kumkemea.
Hakuna kiongozi wa SMZ aliyesimama na kumkemea, maana yake, kauli inaungwa mkono na Wazanzibar

Juzi, katibu mkuu wa Wizara ya watoto, jinsia na wazee SMZ amewaita watoto kutoka Tanganyika wahamiaji haramu. Hakuna kiongozi au Mzanzibar yoyote aliyekemea wakiwemo CCM na OMO team.
Hii maana yake ni kwamba wanaunga mkono '' uharamu wa Watanganyika'' kwa identity ya Uzanzibar

Identity ya Uzanzibar haiwezi kufutika, ina wafanya wasiwajibike na inawapa fursa.
Mfano, kauli ya '' Wazanzibar ni Watanzania na si kila Mtanzania ni Mzanzibar' inaeleza hivyo.

Tukiongelea muungano, gharama anazibeba Mtanganyika kwasababu wao ni Wazanzibar
Wakitaka ardhi wanatumia Utanzania lakini kwao ardhi ni ya Wazanzibar
Kuna nafasi za ajira maalumu kwa Wazanzibar na teuzi za siku hizi zinazingatia Uzanzibar kwa mambo ya Tng
Kuna mgao wa rasilimali za Tanganyika kwa Zanzibar kwasababu ya identity ya Uzanzibar
Juzi wameongeza pesa kwa wanafunzi wa High education kutoka Zanzibar kwasbabu ya Uzanzibar.
Pesa wanazopata HESLB ni za Tanganyika halafu wameongezewa kutoka Zanzibar kwasababu ya Uzanzibar

Mifano ni mingi, na katika muungano wanatumia identity ya Uzanzibar kunufaika.
Siyo akina OMO hata CCM Zanzibar wakitaka ku ''abuse'' wanatishia neno '' KERO'
Kwao identity ni mtaji na huwezi kuwanyang'nya kwa kuwa na serikali 1

Nchi zinaungana kwa ''mutual benefit''. Katika serikali 1 Tanganyika ina 'gain' nini? Katika serikali 2 Tanganyika inapata 'benefit' gani! Na bila muungano Tanganyika ina 'lose' nini!
Hivi huoni kwamba Serikali 3 ni '' favor and to the best interest ya Zanzibar'' !

Nitakwambia kitu kimoja cha kuudhi kidogo. Mgomo wa Wafanyabiashara wa Kariakoo unawagusa sana Watanganyika kuliko mgomo wa Wafanyabiashara wa boti za Zanzibar kuja Dar es salaam.
 
Mkuu, tuchukue ya msingi zaidi, tusikazie haya ya kuudhiana ndiyo tuyaweke mbele zaidi.

Haya yote uliyo weka hapa, tulisha yajadili; sasa tunayarudia t yale yale.

Ninakubaliana na wewe moja kwa moja, muungano uliasisiwa kwa misingi ya 'convenience'; upande mmoja ukitafuta kinga ya mwamvuli, huku upande wa pili ukiwa na dhamira ya kuuweka muungano wa kuipata nchi moja; watu wamoja. Kosa lilikuwa kwa Mwalimu Nyerere kudhani kwamba tawala zitakazo fuata zitakuwa na ushawishi na nguvu za kuendelea kuwabana watu wenye misimamo ya akina OMO Hii ilikuwa ni 'assumption' ambayo ni dhahiri ilikuwa na kasoro kubwa ndani yake. Sote tumeona, badala ya kundi hili la akina OMO kufifia, CCM imeendelea kulirutubisha zaidi wakitumia zile njia za "kero za muungano," moja baada ya nyingine.... Matokeo yake tukafikia kuwa na Zanzibar kuwa nchi kamili sasa.
Kwa hiyo, kama sasa tuna Zanzibar kama nchi, tunataka Tanzania ya nini tena, wakati muungano hapo tena; muungano ambao umeondolewa na uwepo wa Zanzibar kama nchi. Zanzibar haiungani na Tanzania kuwepo taifa la Tanzania!

Ukitaka kuwepo serikali tatu, inabidi uanze taratibu mpya za kuirudisha Tanganyika, ambayo italazimu kujadiliana na nchi ya Zanzibar kuunda muungano wao mpya. Huwezi kutumia 'Tanzania' ijadili makubaliano ya muungano na nchi ya Zanzibar kuunda muungano.
Kwa hiyo, hapa ni wazi ninakubaliana na wanao shauri kuuvunja muungano huu uliokwisha vunjwa na uwepo wa Zanzibar kama nchi. Kitakacho fuata baada ya kuuvunja, sishauri kuunda muungano tena ili kuwe na serikali tatu; miungano ya aina hiyo tayari tunayo kiaina kupitia hizi shirikiano tulizo nazo, kama EAC, SADC, n.k..

Sitajikita tena katika kujibu haya ya "kero", kama hizo za wafanya biashara wa Kariakoo, shutuma za mbunge 9binafsi) bungeni akiwasilisha yale yale tunayo yafahamu siku zote yanako tokea.
Ukimya wa viongozi wa CCM kwenye maswala haya, nalo kweli linahitaji kujibiwa? Hivi umesikia kiongozi yeyote akijibu hoja ya uwepo wa Tanganyika; na kero nyingi mbalimbali za upande huo wa Tanganyika kuhusu muungano? Ukimya huo toka CCM maana yake ni nini; kwamba na wao hawautaki muungano? Umemsikia nani akizungumzia swala lolote ukamwelewa vizuri?
 
Usijitoe ufahamu, structure ya Muungano ilivyowekwa ni kuwabembeleza Wazanzibar ambao hawajawahi uhitaji huo Muungano Bali Bara so ulisema hamtaki wawe Marais ni nonsense.
Acha bange wewe chawa!!!
Karume alihitaji muungano ili kujihakikishia usalama dhidi ya Sultani.

Haiwezekani Watanganyika wawe watumwa milele kisa kubembeleza wazanzibar.
Wazanzibar wanabembelezwa kwa lipi hasa?!!

Matokeo yake Tanganyika imegeuka shamba la bibi, so sad!
 
Mwalimu Nyerere kudhani kwamba tawala zitakazo fuata zitakuwa na ushawishi na nguvu za kuendelea kuwabana watu wenye misimamo ya akina OMO Hii ilikuwa ni 'assumption' ambayo ni dhahiri ilikuwa na kasoro kubwa ndani yake.
Nakubaliana nawe 100%. Nyerere alidhani misingi aliyoweka ni ya kudumu. Baada ya kizazi chake, viongozi waliofuata hawajali tena ule uadilifu , uaminifu na ushawishi aliokuwa nayo.

Sote tumeona, badala ya kundi hili la akina OMO kufifia, CCM imeendelea kulirutubisha zaidi wakitumia zile njia za "kero za muungano," moja baada ya nyingine.... Matokeo yake tukafikia kuwa na Zanzibar kuwa nchi kamili sasa.
Kwa hiyo, kama sasa tuna Zanzibar kama nchi, tunataka Tanzania ya nini tena, wakati muungano hapo tena; muungano ambao umeondolewa na uwepo wa Zanzibar kama nchi. Zanzibar haiungani na Tanzania kuwepo taifa la Tanzania!
Absolutely
Ukitaka kuwepo serikali tatu, inabidi uanze taratibu mpya za kuirudisha Tanganyika, ambayo italazimu kujadiliana na nchi ya Zanzibar kuunda muungano wao mpya. Huwezi kutumia 'Tanzania' ijadili makubaliano ya muungano na nchi ya Zanzibar kuunda muungano.
Hapana, Mzee Warioba na Tume yake waliweka wazi. Zanzibar ina structure kamili, inayotakiwa ni Tanganyika.
In fact Tanganyika ipo kinachotakiwa ni kutambuliwa. Ukiondoa mambo 11 ambayo sasa ni 9 ya Muungano yaliyobaki ni ya Tanganyika. Bunge linashughulikia 98% mambo ya Tanganyika.
Ikiwa Serikali 3 ni muafaka, process haina tatizo. Kinacholeta tatizo ni '' political will''

Nilishangaa awamu hii ya SSH Wizara ya madini ya Tanzania ilisaini MoU na Wizara ya madini ya Zanzibar.
Unaweza kuona tatizo lilipo, hata viongozi ni sehemu ya CCM na OMO! nani alinde muungano uliojifia tayari!
Kwa hiyo, hapa ni wazi ninakubaliana na wanao shauri kuuvunja muungano huu uliokwisha vunjwa na uwepo wa Zanzibar kama nchi. Kitakacho fuata baada ya kuuvunja, sishauri kuunda muungano tena ili kuwe na serikali tatu; miungano ya aina hiyo tayari tunayo kiaina kupitia hizi shirikiano tulizo nazo, kama EAC, SADC, n.k..
Yes ndio maana nilisema '' it's to the best interest of Zanzibar to defend the Union'' kwa serikali 3 kama wanataka.
Kinyume cha hapo tukutane EAC, SADC n.k.
Ukimya wa viongozi wa CCM kwenye maswala haya, nalo kweli linahitaji kujibiwa? Hivi umesikia kiongozi yeyote akijibu hoja ya uwepo wa Tanganyika; na kero nyingi mbalimbali za upande huo wa Tanganyika kuhusu muungano? Ukimya huo toka CCM maana yake ni nini; kwamba na wao hawautaki muungano? Umemsikia nani akizungumzia swala lolote ukamwelewa vizuri?
Neno!
 
Labda nimalizie mjadala huu; au niamshe mjadala mzima upya kwa hili swala la uwepo wa serikali moja, ambalo namsisitizia kila mara mkuu 'JokaKuu kila ninapo msoma akidai serikali tatu. Na kwa bahati nzuri au mbaya sijapata joto kutoka upande wako kuhusu jambo hili.

Kwa kuwa lengo tokea mwanzo lilikuwa ni kuundwa kwa nchi moja na serikali moja; na tukitambua kelele za nchi ya Zanzibar inatoka wapi na inadaiwa hasa na nani (kundi la akina Jusa), ambao hata siku moja hawa huwezi kuwabadili waachane na mawazo hayo...
Hong Kong ipo pale kama mfano. Eneo hilo hadi hii leo wamo wasio jitambulisha kuwa wao ni sehemu ya China. Taiwan iko njiani, hakuna atakayezuia sehemu hiyo kuwa sehemu ya China. Leo hii hapo Taiwan ukisikiliza serikali ya kisiwa hicho na baadhi ya raia, utafikiri kwamba eneo hilo haitatokea hata siku moja liwe sehemu ya China. Hao ndio akina OMO wetu hapa leo.
Tunahitaji tu uongozi wenye dhamira hiyo ya kuwa na nchi moja basi. Maswala mengine ya kubembelezana yatashughulikiwa na wakati.

Ukiniita dikteta juu ya hili, ni sawa tu. Lakini najuwa zipo njia nyingi za kuwashawishi wananchi pande zote mbili kuupa uhalali muungano huo. Ni swala tu la kuwapata viongozi walio tayari kuifanya kazi hiyo; kama tunavyo himiza sasa hivi kuwapata viongozi wa kusimamia uwepo wa Tanganyika yetu.

Nimalize na jambo lisilo husiana na mada. Mag3 ni nadra sana namwona maeneo haya siku hizi; kama ilivyo kwa wewe mku Nguruvi3. Enzi zile za mijadala humu JF, watu hawa walikuwa ni ngozo muhimu ya mijadala humu; na kwa bahati nzuri nilijikuta nikiwa sehemu ya upande wao mara kwa mara.
Ni hayo tu.
 
Heshima sana wanajamvi,

Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ambao uliasisiwa na watu wawili ambao sasa hawapo, tena bila ridhaa ya wananchi wa pande zote mbili sasa unapitia katika msuko suko mkubwa.

Ni wazi Mwl Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume waliziunganisha zao Tanganyika na Zanzibar pasipo ridhaa za wananchi wa pande zote mbili.

Muungano wao (Nyerere & Karume) kwa hakika umejaa kasoro nyingi mno, kuubadili au kuufanyia marekebisho kutahitaji kuzifumua katiba za nchi zote mbili jambo ambalo kwa sasa ni vigumu sana.

Zanzibar wana serekali yao, wana bunge lao, wana wimbo wao wa taifa lao, wana bendera yao, wana uraia wao (Uzanzibari), wana mkuu wao wa nchi, wana ardhi yao (nchi) wana kila kitu chao.

Tanganyika hawana wimbo wa taifa, hawana mkuu wao wa nchi, hawana ardhi yao, hawana bendera yao, kifupi Tanganyika hawana chochote.

Kuna Taifa la Tanzania (JMT) ambalo limepora kila kitu cha nchi ya Tanganyika. Bendera? Wimbo wa taifa, Bunge.

Tanganyika haina mtetezi wa rasilimali zake eg misitu, ardhi, bandari.

Raia wa nchi ya Zanzibar anaiongoza Tanganyika kupitia mgongo wa Muungano anauza kila rasilimali ya Tanganyika bila huruma kwakuwa hazina mtetezi.

Watanganyika wameamka sasa lugha ya Mch. Mtikila na sasa Mheshimiwa Lissu imeanza kueleweka hadi ndani ya CCM. Ugomvi mkubwa wa Kinana, Makamba na wanaCCM wengi ni Tanganyika kutawaliwa na Rais kutokea nchi ya Zanzibar ambaye amekuwa dalali mkubwa wa kuuza rasilimali za Tanganyika.

Wanaoitaka Tanganyika sasa ni Watanganyika wote bila kujali mipaka ya vyama.

Ngongo kwasasa Mjini Magharibi.

Pia soma
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Tanganyika ndio Tanzania.
Tanganyika imevaa koti la Tanzania
Tanganyika ina kila kitu ndio iloitawala Zanzibar.
Hata katiba ya Tanzania ni Katiba ya Tanganyika iliyo tiwa virka kufanyawa ya Tanzania.
Sherhe ya uhuru wa Tanganyika ndio sherehe ya Uhru wa Tanzania.
Tikijuwa fika kuwa Tanzania haikutawaliwa na imezaliwa 26 April.

Shukrani
 
Naomba tu ufafanue, hizo tatu ni za nini hasa!.
Bado tu huridhiki na EAC na SADC na sasa hizo zinazoitwa 'Tri-partite', sijui na matakataka mengi mengine? Haya yote ni ya nini kama siyo kuvuruga tu akili za watu.

Suluhisho la huu Muungano ni kuvunjwa tu mkuu, hauwezi ku work, uliletwa kibaba na waasisi ila haukukubalika wala hauwezi kukubalika.
Kuhusu Serikali tatu ndio maoni ya wengi ambao wanahisi ndio suluhisho la matatizo, ila kiupande wangu ni kuvunjwa tu. Ni bora tuishi majirani wema kuliko kulazimisha udugu kwa nguvu ambao unaweza kuja kutuletea madhara makubwa baadae.
 
Labda nimalizie mjadala huu; au niamshe mjadala mzima upya kwa hili swala la uwepo wa serikali moja, ambalo namsisitizia kila mara mkuu 'JokaKuu kila ninapo msoma akidai serikali tatu. Na kwa bahati nzuri au mbaya sijapata joto kutoka upande wako kuhusu jambo hili.

Kwa kuwa lengo tokea mwanzo lilikuwa ni kuundwa kwa nchi moja na serikali moja; na tukitambua kelele za nchi ya Zanzibar inatoka wapi na inadaiwa hasa na nani (kundi la akina Jusa), ambao hata siku moja hawa huwezi kuwabadili waachane na mawazo hayo...
Hong Kong ipo pale kama mfano. Eneo hilo hadi hii leo wamo wasio jitambulisha kuwa wao ni sehemu ya China. Taiwan iko njiani, hakuna atakayezuia sehemu hiyo kuwa sehemu ya China. Leo hii hapo Taiwan ukisikiliza serikali ya kisiwa hicho na baadhi ya raia, utafikiri kwamba eneo hilo haitatokea hata siku moja liwe sehemu ya China. Hao ndio akina OMO wetu hapa leo.
Tunahitaji tu uongozi wenye dhamira hiyo ya kuwa na nchi moja basi. Maswala mengine ya kubembelezana yatashughulikiwa na wakati.

Ukiniita dikteta juu ya hili, ni sawa tu. Lakini najuwa zipo njia nyingi za kuwashawishi wananchi pande zote mbili kuupa uhalali muungano huo. Ni swala tu la kuwapata viongozi walio tayari kuifanya kazi hiyo; kama tunavyo himiza sasa hivi kuwapata viongozi wa kusimamia uwepo wa Tanganyika yetu.

Nimalize na jambo lisilo husiana na mada. Mag3 ni nadra sana namwona maeneo haya siku hizi; kama ilivyo kwa wewe mku Nguruvi3. Enzi zile za mijadala humu JF, watu hawa walikuwa ni ngozo muhimu ya mijadala humu; na kwa bahati nzuri nilijikuta nikiwa sehemu ya upande wao mara kwa mara.
Ni hayo tu.

Hakuna njia ya kuwashawishi wazanzibari kuwa na Serikali moja, Ikiwa mbili hamuzitaki.
Hio ipo very logic hawawezi kukubali kupotea.
 
Labda nimalizie mjadala huu; au niamshe mjadala mzima upya kwa hili swala la uwepo wa serikali moja, ambalo namsisitizia kila mara mkuu 'JokaKuu kila ninapo msoma akidai serikali tatu. Na kwa bahati nzuri au mbaya sijapata joto kutoka upande wako kuhusu jambo hili.

Kwa kuwa lengo tokea mwanzo lilikuwa ni kuundwa kwa nchi moja na serikali moja; na tukitambua kelele za nchi ya Zanzibar inatoka wapi na inadaiwa hasa na nani (kundi la akina Jusa), ambao hata siku moja hawa huwezi kuwabadili waachane na mawazo hayo...
Hong Kong ipo pale kama mfano. Eneo hilo hadi hii leo wamo wasio jitambulisha kuwa wao ni sehemu ya China. Taiwan iko njiani, hakuna atakayezuia sehemu hiyo kuwa sehemu ya China. Leo hii hapo Taiwan ukisikiliza serikali ya kisiwa hicho na baadhi ya raia, utafikiri kwamba eneo hilo haitatokea hata siku moja liwe sehemu ya China. Hao ndio akina OMO wetu hapa leo.
Tunahitaji tu uongozi wenye dhamira hiyo ya kuwa na nchi moja basi. Maswala mengine ya kubembelezana yatashughulikiwa na wakati.

Ukiniita dikteta juu ya hili, ni sawa tu. Lakini najuwa zipo njia nyingi za kuwashawishi wananchi pande zote mbili kuupa uhalali muungano huo. Ni swala tu la kuwapata viongozi walio tayari kuifanya kazi hiyo; kama tunavyo himiza sasa hivi kuwapata viongozi wa kusimamia uwepo wa Tanganyika yetu.

Kuhusu 'udikteta' mbona Nyerere amejaribu ! ''Wanafunzi '' akina Mkapa , Warioba n.k wakajaribu.
Nguvu ile ya ''udikteta'' inakuwa 'diluted' kwasababu ya kizazi na ukosefu wa misingi imara, Serikali 2 ikiwemo

'' Adulteration' ya muungano Ilianza na akina Kikwete kuchekacheka katiba ikivunjwa na Zanzibar '' wakijitoa ''
Leo Rais wa JMT anasimamia MoU na Rais wa Zanzibar ! I mean Tanzania na Zanzibar, ishara ya kifo- muungano

Kuhusu Taiwan na Hong Kong mazingira ni tofauti na hali yetu na Zanzibar
Taiwan kama sikosei ndiko wanasema '' where east meets west' . Ni eneo la kiusalama kutokana na ''polarity'
China inalipa gharama si kwa mapenzi bali kwa usalama. Hong Kong pia na zote, zina uwezo wa kujitegemea

Kwetu, sababu za kiusalama tulizoambiwa hazipo. Tuna US military base kubwa hapo Mombasa
Tuna US Embassy kubwa Sub Sahara , tuna China kule deep sea n.k.

Tuna resources chache zipelekwe mikoa mipya wa Simiyu, Njombe au Geita ili ziendelee kuchangia pato la Taifa na sikumoja tusikie zime piku Dar na K'njaro. Huo ndio uwekezaji tunaohitaji na si ubembelezaji.

Wazanzibar wana machaguo haya '' cut and run or submit to 3 tier system''

Watanganyika hawana chaguo, wana majibu
1. Serikali 2 ' failed system''
2. Serikali 3 ' wata benefit na nini''
3. Serikali 1 'wata gain nini''
4. Vunja Muungano '' wata lose nini''
 
Kuhusu 'udikteta' mbona Nyerere amejaribu ! ''Wanafunzi '' akina Mkapa , Warioba n.k wakajaribu.
Nguvu ile ya ''udikteta'' inakuwa 'diluted' kwasababu ya kizazi na ukosefu wa misingi imara, Serikali 2 ikiwemo
Hapana. Katika hili natoa a 'firm NO'.
Mwalimu pamoja na baadhi ya watu kumpachika 'udikteta', ukweli ni kwamba alipenda mijadala ya hoja na uamzi utokane na hoja hizo. Pamoja na kwamba wakati wake hawakuwepo wasomi wengi, lakini waliokuwepo hao wachache walijitahidi kushiriki katika kutoa mawazo tofauti kabisa na ilivyo sasa wakati huu tunapojiona tunao wasomi na waelewa wa mambo wengi. Siku hizi kinachojaliwa zaidi ni maslahi ya kibinafsi.
Kumwita Mwalimu dikteta, hili nasita sana kulikubali. Kuwa na uwezo wa ushawishi juu ya jambo, ndiyo, lakini siyo kuburuza wengine.

Ni hivi mkuu Nguruvi: Mwalimu wakati ule angekazia sana na kuweka juhudi za muungano uende hatua zote kwa haraka, na panapo lazimika kutumia kila njia hata kuburuza iwe hivyo, leo hii tungekuwa tofauti na tulivyo sasa. Hao akina Othman wangekuwa wanapiga kelele, ndiyo, lakini wasingekuwa na njia za kuurudisha nyuma muungano uliokuwa umefikia hatua za mwisho. Leo hii hata HongKong wafanye nini, hawana njia yoyote ya kukinasua kisiwa hicho. Hali itakuwa hivyo hivyo na Taiwan.

Inge amriwa kwenda kwenye serikali moja ndani ya miaka kumi au ishirini na juhudi zikafanywa iwe hivyo 'unequivocally', pasingekuwepo mtu wa kuthubutu kuleta tena kelele za kero na kutafuta kuvunja muungano huo.

Ujue, ucheleweshaji huo wa kufikia huku tunako kuzungumzia sasa ni hatua hizo hizo za kutomhusisha Mwalimu na udikteta.
Kuhusu Taiwan na Hong Kong mazingira ni tofauti na hali yetu na Zanzibar
Taiwan kama sikosei ndiko wanasema '' where east meets west' . Ni eneo la kiusalama kutokana na ''polarity'
China inalipa gharama si kwa mapenzi bali kwa usalama. Hong Kong pia na zote, zina uwezo wa kujitegemea
'Model' ni hiyo hiyo hata hapa kwetu. Hii inatambulika kuwa ni "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", nchi moja, 'indivisible'. Sehemu yoyote ya muungano isichewe na mtu yeyote. Tena sisi tayri tulikuwa katika hali nzuri kabisa kuwashinda hao waChina. Lakini sasa unaona hata Mwinyi anakagua vikosi vyake vya ulinzi! Wanalinda kitu gani hao? Zote hizo ni juhudi tu za kujionyesha kuwa wao ni nchi; na siku moja watawakaribisha waarabu kuleta majeshi yao hapo kukabiliana na majeshi yetu! Huu ndio upumbavu wetu mkubwa.
Kwetu, sababu za kiusalama tulizoambiwa hazipo. Tuna US military base kubwa hapo Mombasa
Tuna US Embassy kubwa Sub Sahara , tuna China kule deep sea n.k.
Uwepo wa hao wote hakutishii usalama wetu na muungano wetu bila ya kuchokozana nao. 'At least' kulinda 'sovereignty' yetu ingekuwa ni sababu kubwa na muhimu kabisa kuwatia aibu ya kutuvamia. Hivyo visheria wamevitunga wao.
Wazanzibar wana machaguo haya '' cut and run or submit to 3 tier system''

Watanganyika hawana chaguo, wana majibu
1. Serikali 2 ' failed system''
2. Serikali 3 ' wata benefit na nini''
3. Serikali 1 'wata gain nini''
4. Vunja Muungano '' wata lose nini''
Ngoja nimalize, lakini siyo kwa kukutia aibu wewe au kukusuta, na wengine, wote wanaokimbilia urahisi wa kuvunja muungano..., kwamba 'inadvertently', nyote mnashirikiana na akina OMO katika kazi hiyo hiyo moja. Maana yake ni kwamba wote wanaokimbilia kwenye kuvunja muungano kwa sababu moja au nyingine, ni kundi hilo hilo moja, liwe Zanzibar, au liwe Tanganyika, lengo lenu ni moja'
Naomba unielewe kuwa hii si hukumu, mkuu wangu Nguruvi3, ni mjadala tu!

Serikali ni moja tu, na muungano ni wa aina ile ile ya kichina na Hongkong, au na Taiwan utakapopatikana.
Na kama utapenda, ngoja nikukumbushe huo muungano wa wamarekani wenyewe. Ninaelewa wazi unajua nini kilitokea hadi wakawa na muungano walio nao leo. Hawakusubiri kubembelezana na kuhakikisha kila mmoja wao ameukubali muungano. Hata leo hii utapita sehemu wapo wasiokubali kuwa katika muungano huo, baada ya miaka yote hii na kupata maendeleo waliyo nayo leo. Sembuse sisi hapa?

Nadhani hili sasa tulipumzishe hapa.
 
Hakuna njia ya kuwashawishi wazanzibari kuwa na Serikali moja, Ikiwa mbili hamuzitaki.
Hio ipo very logic hawawezi kukubali kupotea.
China aliwashawishi na nini HongKong?
WaZanzibar wasiokuwa na msemaji wa kuwasemea unawajumuisha kuwa wanasemewa na kikundi ambacho miaka yote tokea muungano uwepo ndio leo wawe wasemaji wao?
 
Suluhisho la huu Muungano ni kuvunjwa tu mkuu, hauwezi ku work, uliletwa kibaba na waasisi ila haukukubalika wala hauwezi kukubalika.
Kuhusu Serikali tatu ndio maoni ya wengi ambao wanahisi ndio suluhisho la matatizo, ila kiupande wangu ni kuvunjwa tu. Ni bora tuishi majirani wema kuliko kulazimisha udugu kwa nguvu ambao unaweza kuja kutuletea madhara makubwa baadae.
Hata siku moja haitatokea upate muungano utakao kubaliwa na kila mtu ndani ya nchi yoyote. Natumaini utanielewa ninacho kisema hapa.
 
Back
Top Bottom