Mkuu naomba usipumzike kwa muda kidogo, kuna machache ya kudadvua
Mwalimu pamoja na baadhi ya watu kumpachika 'udikteta', Kumwita Mwalimu dikteta, hili nasita sana kulikubali. Kuwa na uwezo wa ushawishi juu ya jambo, ndiyo, lakini siyo kuburuza wengine.
Hapana ! sikuamaanisha ni 'Dikteta' . Nilimaanisha katika Muungano ali force.
Kwanza, Uharaka bila kuuliza Wananchi. Pili, kuifuta Tanganyika na historia yake.
Tatu, kukabidhi mamlaka ya Tanganyika kwa 'Tanzania''. Nne kuzuia hoja kibeba kama ilivyokuwa kwa Jumbe, Shaaban Mloo, Maalim Seif, G55 na kamati luluki zilizofuata.
Tano kuufanya muungano kitu ''sacred' hadi leo kuzungumzia ni 'taboo' isipokuwa kwa Wazanzibar.
Inge amriwa kwenda kwenye serikali moja ndani ya miaka kumi au ishirini na juhudi zikafanywa iwe hivyo 'unequivocally', pasingekuwepo mtu wa kuthubutu kuleta tena kelele za kero na kutafuta kuvunja muungano huo.
Unasahau Scotland na UK licha ya miaka 300 ya kuungana. Wales nao wanadai.
Usisahau Quebec na Canada licha ya miaka 152 ya Kuungana
Usisahau Timor ilijitoa baada ya miaka zaidi ya 50 huku Eritrea ikijiondoa baada ya miaka zaidi ya 100
Kuna Biafra ya Ojuku na Ken Sorowiwa na fukuto linaendelea.
Nyerere alijifunza hakutaka kufuata njia hiyo ndiyo maana hakuharakisha! Tatizo lake ni muundo
Lakini sasa unaona hata Mwinyi anakagua vikosi vyake vya ulinzi! Wanalinda kitu gani hao? Zote hizo ni juhudi tu za kujionyesha kuwa wao ni nchi; na siku moja watawakaribisha waarabu kuleta majeshi yao hapo kukabiliana na majeshi yetu! Huu ndio upumbavu wetu mkubwa.
Nakubaliana na hoja ya '' deputy Commander in chief' , yote yametokea kwasababu ya kuendeleza Uzanzibar na mhusika alikuwa Kikwete aliyemruhusu OMO kubadili katiba yeye akitabasamu tu.
Sikubaliani kuhusu Jeshi la Waarabu! Hakuna historia ya Waarabu kuvamia nchi nyingine.
Nadhani unahusisha Uarabu na Uislam ndio hoja inayoelezwa kutisha watu ikiongozwa na akina Lukuvy.
Tuna mpaka na nchi 8 , zenye matatizo! . Kwanini tunadhani Zanzibar ni tishio!
Hakuna Jeshi la Mwarabu na hapa ndipo upumbavu wetu ulipo, fear of unknown.
Fear of unknown inaletwa na 'misinformatio na disinformation' kuhadaa umma!
Watu wamekuwa na 'Paranoia'' hata kukimbia vivuli vyao. Seriosly! mwarabu alete jeshi! ilitokea wapi
Uwepo wa hao wote hakutishii usalama wetu na muungano wetu bila ya kuchokozana nao.
Una maana USA na nchi za magharibi si tatizo! well, mwaka 1982 Katika kesi ya akina Mbogoro, Tamim, Kadego, na wenzao wakitetewa na Murtaza Lakha! meli za Uingereza zilikuwa bahari ya Hindi. Hilo si tishio?
JokaKuu Pascal Mayalla
Ngoja nimalize, lakini siyo kwa kukutia aibu wewe au kukusuta, na wengine, wote wanaokimbilia urahisi wa kuvunja muungano..., kwamba 'inadvertently', nyote mnashirikiana na akina OMO katika kazi hiyo hiyo moja. Maana yake ni kwamba wote wanaokimbilia kwenye kuvunja muungano kwa sababu moja au nyingine, ni kundi hilo hilo moja, liwe Zanzibar, au liwe Tanganyika, lengo lenu ni moja'Naomba unielewe kuwa hii si hukumu, mkuu wangu Nguruvi3, ni mjadala tu!
Nasimama na ''Mama Tanganyika'' ndiyo maana nasema for the best interest ya Zanzibar, serikali 3 zitawasaidia.
Kwanini nasimama na Tanganyika, maswali yangu nitayarudia hapa chini.
Serikali ni moja tu, na muungano ni wa aina ile ile ya kichina na Hongkong, au na Taiwan utakapopatikana.
Na kama utapenda, ngoja nikukumbushe huo muungano wa wamarekani wenyewe. Ninaelewa wazi unajua nini kilitokea hadi wakawa na muungano walio nao leo. Hawakusubiri kubembelezana na kuhakikisha kila mmoja wao ameukubali muungano. Hata leo hii utapita sehemu wapo wasiokubali kuwa katika muungano huo, baada ya miaka yote hii na kupata maendeleo waliyo nayo leo. Sembuse sisi hapa?Nadhani hili sasa tulipumzishe hapa.
Kwanini tutumie muda na rasilimali nyingi kuwalazimisha Wazanzibar? Hebu tusaidie haya
1. Washawishi Watanganyika kwanini tunahitaji Muungano , uwe wa muundo wowote. Kwanini tuhaitaji
2. Kwa muundo wa Serikali 2 , Tanganyika inafadika na nini !
3. Kwa serikali 1, Tanganyika itafaidika na nini
4. Kwa serikali 3 Tanganyika inapata nini !
5. Ikiwa muungano utavunjika, Tanganyika itapoteza nini!