Vita ya kisiasa baina ya Tanganyika na Zanzibar ipo wazi sasa

Vita ya kisiasa baina ya Tanganyika na Zanzibar ipo wazi sasa

Heshima sana wanajamvi,

Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ambao uliasisiwa na watu wawili ambao sasa hawapo, tena bila ridhaa ya wananchi wa pande zote mbili sasa unapitia katika msuko suko mkubwa.

Ni wazi Mwl Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume waliziunganisha zao Tanganyika na Zanzibar pasipo ridhaa za wananchi wa pande zote mbili.

Muungano wao (Nyerere & Karume) kwa hakika umejaa kasoro nyingi mno, kuubadili au kuufanyia marekebisho kutahitaji kuzifumua katiba za nchi zote mbili jambo ambalo kwa sasa ni vigumu sana.

Zanzibar wana serekali yao, wana bunge lao, wana wimbo wao wa taifa lao, wana bendera yao, wana uraia wao (Uzanzibari), wana mkuu wao wa nchi, wana ardhi yao (nchi) wana kila kitu chao.

Tanganyika hawana wimbo wa taifa, hawana mkuu wao wa nchi, hawana ardhi yao, hawana bendera yao, kifupi Tanganyika hawana chochote.

Kuna Taifa la Tanzania (JMT) ambalo limepora kila kitu cha nchi ya Tanganyika. Bendera? Wimbo wa taifa, Bunge.

Tanganyika haina mtetezi wa rasilimali zake eg misitu, ardhi, bandari.

Raia wa nchi ya Zanzibar anaiongoza Tanganyika kupitia mgongo wa Muungano anauza kila rasilimali ya Tanganyika bila huruma kwakuwa hazina mtetezi.

Watanganyika wameamka sasa lugha ya Mch. Mtikila na sasa Mheshimiwa Lissu imeanza kueleweka hadi ndani ya CCM. Ugomvi mkubwa wa Kinana, Makamba na wanaCCM wengi ni Tanganyika kutawaliwa na Rais kutokea nchi ya Zanzibar ambaye amekuwa dalali mkubwa wa kuuza rasilimali za Tanganyika.

Wanaoitaka Tanganyika sasa ni Watanganyika wote bila kujali mipaka ya vyama.

Ngongo kwasasa Mjini Magharibi.

Pia soma
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Usinisemee sojakutuma use me jisemee mwenyewe.
 
Kama upo uwezekano wa Mtanganyika kugombea ubunge Zanzibar au kuongoza nchi ya watu wa Zanzibar bila vizingiti vya kusheria muungano ungeeleweka.

Kama Mtanganyika angeweza kununua ardhi kama raia wa Tanzania huu muungano tusingeupigia kelele.
Mwinyi mbona Ni rais kule.
 
Mkuu naomba usipumzike kwa muda kidogo, kuna machache ya kudadvua
Mwalimu pamoja na baadhi ya watu kumpachika 'udikteta', Kumwita Mwalimu dikteta, hili nasita sana kulikubali. Kuwa na uwezo wa ushawishi juu ya jambo, ndiyo, lakini siyo kuburuza wengine.
Hapana ! sikuamaanisha ni 'Dikteta' . Nilimaanisha katika Muungano ali force.
Kwanza, Uharaka bila kuuliza Wananchi. Pili, kuifuta Tanganyika na historia yake.
Tatu, kukabidhi mamlaka ya Tanganyika kwa 'Tanzania''. Nne kuzuia hoja kibeba kama ilivyokuwa kwa Jumbe, Shaaban Mloo, Maalim Seif, G55 na kamati luluki zilizofuata.
Tano kuufanya muungano kitu ''sacred' hadi leo kuzungumzia ni 'taboo' isipokuwa kwa Wazanzibar.
Inge amriwa kwenda kwenye serikali moja ndani ya miaka kumi au ishirini na juhudi zikafanywa iwe hivyo 'unequivocally', pasingekuwepo mtu wa kuthubutu kuleta tena kelele za kero na kutafuta kuvunja muungano huo.
Unasahau Scotland na UK licha ya miaka 300 ya kuungana. Wales nao wanadai.
Usisahau Quebec na Canada licha ya miaka 152 ya Kuungana
Usisahau Timor ilijitoa baada ya miaka zaidi ya 50 huku Eritrea ikijiondoa baada ya miaka zaidi ya 100
Kuna Biafra ya Ojuku na Ken Sorowiwa na fukuto linaendelea.
Nyerere alijifunza hakutaka kufuata njia hiyo ndiyo maana hakuharakisha! Tatizo lake ni muundo
Lakini sasa unaona hata Mwinyi anakagua vikosi vyake vya ulinzi! Wanalinda kitu gani hao? Zote hizo ni juhudi tu za kujionyesha kuwa wao ni nchi; na siku moja watawakaribisha waarabu kuleta majeshi yao hapo kukabiliana na majeshi yetu! Huu ndio upumbavu wetu mkubwa.
Nakubaliana na hoja ya '' deputy Commander in chief' , yote yametokea kwasababu ya kuendeleza Uzanzibar na mhusika alikuwa Kikwete aliyemruhusu OMO kubadili katiba yeye akitabasamu tu.

Sikubaliani kuhusu Jeshi la Waarabu! Hakuna historia ya Waarabu kuvamia nchi nyingine.
Nadhani unahusisha Uarabu na Uislam ndio hoja inayoelezwa kutisha watu ikiongozwa na akina Lukuvy.

Tuna mpaka na nchi 8 , zenye matatizo! . Kwanini tunadhani Zanzibar ni tishio!
Hakuna Jeshi la Mwarabu na hapa ndipo upumbavu wetu ulipo, fear of unknown.

Fear of unknown inaletwa na 'misinformatio na disinformation' kuhadaa umma!
Watu wamekuwa na 'Paranoia'' hata kukimbia vivuli vyao. Seriosly! mwarabu alete jeshi! ilitokea wapi
Uwepo wa hao wote hakutishii usalama wetu na muungano wetu bila ya kuchokozana nao.
Una maana USA na nchi za magharibi si tatizo! well, mwaka 1982 Katika kesi ya akina Mbogoro, Tamim, Kadego, na wenzao wakitetewa na Murtaza Lakha! meli za Uingereza zilikuwa bahari ya Hindi. Hilo si tishio?
JokaKuu Pascal Mayalla
Ngoja nimalize, lakini siyo kwa kukutia aibu wewe au kukusuta, na wengine, wote wanaokimbilia urahisi wa kuvunja muungano..., kwamba 'inadvertently', nyote mnashirikiana na akina OMO katika kazi hiyo hiyo moja. Maana yake ni kwamba wote wanaokimbilia kwenye kuvunja muungano kwa sababu moja au nyingine, ni kundi hilo hilo moja, liwe Zanzibar, au liwe Tanganyika, lengo lenu ni moja'Naomba unielewe kuwa hii si hukumu, mkuu wangu Nguruvi3, ni mjadala tu!
Nasimama na ''Mama Tanganyika'' ndiyo maana nasema for the best interest ya Zanzibar, serikali 3 zitawasaidia.
Kwanini nasimama na Tanganyika, maswali yangu nitayarudia hapa chini.
Serikali ni moja tu, na muungano ni wa aina ile ile ya kichina na Hongkong, au na Taiwan utakapopatikana.
Na kama utapenda, ngoja nikukumbushe huo muungano wa wamarekani wenyewe. Ninaelewa wazi unajua nini kilitokea hadi wakawa na muungano walio nao leo. Hawakusubiri kubembelezana na kuhakikisha kila mmoja wao ameukubali muungano. Hata leo hii utapita sehemu wapo wasiokubali kuwa katika muungano huo, baada ya miaka yote hii na kupata maendeleo waliyo nayo leo. Sembuse sisi hapa?Nadhani hili sasa tulipumzishe hapa.
Kwanini tutumie muda na rasilimali nyingi kuwalazimisha Wazanzibar? Hebu tusaidie haya
1. Washawishi Watanganyika kwanini tunahitaji Muungano , uwe wa muundo wowote. Kwanini tuhaitaji
2. Kwa muundo wa Serikali 2 , Tanganyika inafadika na nini !
3. Kwa serikali 1, Tanganyika itafaidika na nini
4. Kwa serikali 3 Tanganyika inapata nini !
5. Ikiwa muungano utavunjika, Tanganyika itapoteza nini!
 
Hivi ni Othman aliyebadilisha katiba ya Zanzibar? Mbona role ya CCM Zanzibar chini ya Amani na Sheni inapuuzwa?

Muundo uliopo unawahakikishia CCM Zanzibar kuendelea kufaidi utawala bila ya kubeba gharama za kuulinda utawala wenyewe. Jeshi Polisi na Usalama wa Taifa hawagharamikii wao
 
Hivi ni Othman aliyebadilisha katiba ya Zanzibar? Mbona role ya CCM Zanzibar chini ya Amani na Sheni inapuuzwa?

Muundo uliopo unawahakikishia CCM Zanzibar kuendelea kufaidi utawala bila ya kubeba gharama za kuulinda utawala wenyewe. Jeshi Polisi na Usalama wa Taifa hawagharamikii wao
Hii si agenda ya OMO, Wazanzibar CCM na wasio na vyama wanaungana.Katiba ilibadilishwa aliyeongoza ni Karume. Matokeo yake nchi ya Zanzibar kuingia makubaliano(MoU) ya ushirikiano na nchi ya Tanzania

CDF Ret. Mabeyo aliwahi kusema '' ... hili la Rais wa Zanzibar kupigiwa mizinga 21 linatatiza sana jeshini''
Mkuu wa majeshi ni mmoja lakini ana ''Commander in Chief' wawili, Tanzania na Zanzibar!

Rais Mwinyi anauza visiwa Zanzibar, Katiba inasema Rais wa JMT ni mdhamini wa Ardhi na ndiye ,kwa kushirikiana na Wazanzibar wataigawa nchi kwa maeneo ya utawala n.k. Je hicho ndicho kinatokea?

Waziri mkuu ni kiongozi wa serikali Bungeni anaweza kutoa kauli kwa niaba ya Tanzania.

Rais na Makamu wake wakiwa hawapo kwa udhuru wowote anayeongoza baraza la mawaziri ni Waziri mkuu na mmoja wa Wajumbe ni Rais wa Zanzibar. Waziri mkuu anaweza kutoa kauli ya Tanzania lakini hana mamlaka Zanzibar
 
Tanganyika ndio Tanzania.
Tanganyika imevaa koti la Tanzania
Tanganyika ina kila kitu ndio iloitawala Zanzibar.
Hata katiba ya Tanzania ni Katiba ya Tanganyika iliyo tiwa virka kufanyawa ya Tanzania.
Sherhe ya uhuru wa Tanganyika ndio sherehe ya Uhru wa Tanzania.
Tikijuwa fika kuwa Tanzania haikutawaliwa na imezaliwa 26 April.

Shukrani
Hahahaha! This kinda makes sense😂
 
China aliwashawishi na nini HongKong?
WaZanzibar wasiokuwa na msemaji wa kuwasemea unawajumuisha kuwa wanasemewa na kikundi ambacho miaka yote tokea muungano uwepo ndio leo wawe wasemaji wao?

mkuu mentality za kidikteta zinakusumbua kichwani mwako
 
Hapana. Katika hili natoa a 'firm NO'.
Mwalimu pamoja na baadhi ya watu kumpachika 'udikteta', ukweli ni kwamba alipenda mijadala ya hoja na uamzi utokane na hoja hizo. Pamoja na kwamba wakati wake hawakuwepo wasomi wengi, lakini waliokuwepo hao wachache walijitahidi kushiriki katika kutoa mawazo tofauti kabisa na ilivyo sasa wakati huu tunapojiona tunao wasomi na waelewa wa mambo wengi. Siku hizi kinachojaliwa zaidi ni maslahi ya kibinafsi.
Kumwita Mwalimu dikteta, hili nasita sana kulikubali. Kuwa na uwezo wa ushawishi juu ya jambo, ndiyo, lakini siyo kuburuza wengine.

Ni hivi mkuu Nguruvi: Mwalimu wakati ule angekazia sana na kuweka juhudi za muungano uende hatua zote kwa haraka, na panapo lazimika kutumia kila njia hata kuburuza iwe hivyo, leo hii tungekuwa tofauti na tulivyo sasa. Hao akina Othman wangekuwa wanapiga kelele, ndiyo, lakini wasingekuwa na njia za kuurudisha nyuma muungano uliokuwa umefikia hatua za mwisho. Leo hii hata HongKong wafanye nini, hawana njia yoyote ya kukinasua kisiwa hicho. Hali itakuwa hivyo hivyo na Taiwan.

Inge amriwa kwenda kwenye serikali moja ndani ya miaka kumi au ishirini na juhudi zikafanywa iwe hivyo 'unequivocally', pasingekuwepo mtu wa kuthubutu kuleta tena kelele za kero na kutafuta kuvunja muungano huo.

Ujue, ucheleweshaji huo wa kufikia huku tunako kuzungumzia sasa ni hatua hizo hizo za kutomhusisha Mwalimu na udikteta.
'Model' ni hiyo hiyo hata hapa kwetu. Hii inatambulika kuwa ni "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", nchi moja, 'indivisible'. Sehemu yoyote ya muungano isichewe na mtu yeyote. Tena sisi tayri tulikuwa katika hali nzuri kabisa kuwashinda hao waChina. Lakini sasa unaona hata Mwinyi anakagua vikosi vyake vya ulinzi! Wanalinda kitu gani hao? Zote hizo ni juhudi tu za kujionyesha kuwa wao ni nchi; na siku moja watawakaribisha waarabu kuleta majeshi yao hapo kukabiliana na majeshi yetu! Huu ndio upumbavu wetu mkubwa.
Uwepo wa hao wote hakutishii usalama wetu na muungano wetu bila ya kuchokozana nao. 'At least' kulinda 'sovereignty' yetu ingekuwa ni sababu kubwa na muhimu kabisa kuwatia aibu ya kutuvamia. Hivyo visheria wamevitunga wao.
Ngoja nimalize, lakini siyo kwa kukutia aibu wewe au kukusuta, na wengine, wote wanaokimbilia urahisi wa kuvunja muungano..., kwamba 'inadvertently', nyote mnashirikiana na akina OMO katika kazi hiyo hiyo moja. Maana yake ni kwamba wote wanaokimbilia kwenye kuvunja muungano kwa sababu moja au nyingine, ni kundi hilo hilo moja, liwe Zanzibar, au liwe Tanganyika, lengo lenu ni moja'
Naomba unielewe kuwa hii si hukumu, mkuu wangu Nguruvi3, ni mjadala tu!

Serikali ni moja tu, na muungano ni wa aina ile ile ya kichina na Hongkong, au na Taiwan utakapopatikana.
Na kama utapenda, ngoja nikukumbushe huo muungano wa wamarekani wenyewe. Ninaelewa wazi unajua nini kilitokea hadi wakawa na muungano walio nao leo. Hawakusubiri kubembelezana na kuhakikisha kila mmoja wao ameukubali muungano. Hata leo hii utapita sehemu wapo wasiokubali kuwa katika muungano huo, baada ya miaka yote hii na kupata maendeleo waliyo nayo leo. Sembuse sisi hapa?

Nadhani hili sasa tulipumzishe hapa.
Mkuu 'Nguruvi3', huu mjadala nafikiri tumeufikisha mahali tusipoweza kuongeza thamani zaidi juu ya majadiliano yetu kwa sasa. Tutarejea tu humo humu tulimo kwisha pitia kwa kutumia mifano tofauti tu kukazia tuliyo kwisha elezana mwanzo.
Kwa mfano: tunapotumia mifano ya Wales, Scotland, Ireland Kaskazini na England yenyewe, halafu tuifananishe na Zanzibar nchi kamili ndani ya muungano, hapo nakosa mantiki yake ni nini hasa!

Kuwataja waarabu, kidogo hili linanistua kutoka kwako na kuingiza dini ndani yake. Inanishangaza kidogo kwa mtu mwenye upeo kama wako kufanya 'association' ya namna hiyo ya jambo hilo. Vinchi kadhaa vya kiarabu vyenye ukwasi mwingi, kama UAE na Qatar na wengineo leo hii wanafahamika kuchochea migogoro maeneo mbalimbali ya dunia; lakini hilo unaona haliwezi kutokea hapa?
Lakini napenda unielewe vizuri, mimi siyo muumini wa usalama wa Tanzania kutegemea kuikumbatia Zanzibar. Sijawahi hata mara moja kuiweka maanani dhana hii.

Ninakubaliana nawe juu ya Kikwete na ushiriki wake katika kuudhoofisha muungano. Hapo ndipo palipoanzia kuimarika kwa kundi lisilo penda muungano, na kuwapa ujasiri wa kuongeza juhudi. Samia, ni dhahiri kabisa kaja kumaliza kazi ya kuua muungano. Huyu ndiye alimaliza kero nyingi zilizokuwa zikidaiwa na hao wasiopenda muungano. Kazi hii aliifanikisha sana alipokuwa Makamu wa Rais. Magufuli ni kama alikuwa haoni chochote upande huo. Kiuhalisia Magufuli hakuwa na ukaribu wowote juu ya muungano. Bila shaka leo hii tungeweza kusema ni mmoja wa viongozi ambao muungano kwao uwepo usiwepo ni sawa tu.

Swala la nchi kuungana siyo la lelemama, ndiyo maana unaona tunaona matukio ya hivi sasa kama vita ya Urusi na Ukraine. Njia sahihi ya kupunguza hizi purukushani, hasa zinazo anzia ndani ya nchi ni kuimarisha uchumi wa nchi, ili wananchi waone manufaa ya kuungana kwenyewe.
Marekani na ukubwa wake huo, na kuwa na majimbo mengi yenye utajiri tofauti; lakini husikii kelele za watu kutaka kujitoa, isipokuwa wale wachache, kama akina OMO wetu hapa.

Natamani kuzungumzia nafasi na umuhimu wa uongozi (kiongozi mkuu) kama Mwalimu katika kuongoza na kuelekeza taifa kwenye lengo maalum; lakini hili ngoja niliache lilivyo kwa sasa.

Mwisho, ifahamike natetea muungano na serikali moja. Hii haina maana sipendi Tanganyika iwepo kama nchi inayojitosheleza yenyewe bila ya muungano wa kiini macho wa serikali tatu Ni bora kuuondoa muungano moja kwa moja kuliko kujifanya tuna muungano wa aina hiyo. Huu wa serikali mbili wakati kukiwa na nchi huru ya Zanzibar hata siwezi kuuelezea ni kitu gani hiki.
 
mkuu mentality za kidikteta zinakusumbua kichwani mwako
Sina muda wa kupoteza na hayawani kama wewe; lakini kama unataka lete tu maombi nami nitatenga muda maalum tushughulike na huo ukichaa unaokusumbua
 
Kwa mfano: tunapotumia mifano ya Wales, Scotland, Ireland Kaskazini na England yenyewe, halafu tuifananishe na Zanzibar nchi kamili ndani ya muungano, hapo nakosa mantiki yake ni nini hasa!
Mantiki ni kukuonyesha hata miaka 50,100 au 300 ikiwa muungano haukujengwa katika maridhiano ni tatizo.
Hili nilikuwa najibu hoja kwamba Mwalimu alisubiri muda upite ili 'assimilation' itokee tuelekee serikali 1.
Kuwataja waarabu, kidogo hili linanistua kutoka kwako na kuingiza dini Inanishangaza k kufanya 'association' ya namna hiyo ya jambo hilo. Vinchi kadhaa vya kiarabu vyenye ukwasi mwingi, kama UAE na Qatar na wengineo kuchochea migogoro maeneo ya dunia; haliwezi kutokea hapa?
Nchi za kiarabu zina siasa za influence mashariki ya kati. Mathalani, Iran ni superpower baada ya Iraq. Kwanini? Kwasababu imeipuku Saudi Arabia. Inatokea hivyo kwasababu ya Shia na Sunni.

Kama Saudi Arabia ilivyo na influence kwa Yemen, ndivyo Iran ilivyo kwa Qatar.
Influence inatengeneza makundi kama Houthi, Hamas, Fatah, Hezbollah, ISIS, Brotherhood, Sufi n.k.
Anayechochea ni nchi za magharibi, Wagawe uwatawale kwasababu ya 'black gold''
Ni nadra nchi za kiarabu kuingilia vinchi masikikini vya Afrika kwasababu hakuna cha kupata.

Kuna hisia za ajabu sana! ikiwa unahofia Waarabu Zanzibar kwanini usihofu uwepo wao Mombasa?

Kuhusu Zanzibar kuna hisia zinafichwa fichwa lakini zinajulikana. Mh Lukuvi alisema wazi .
Haya yapo hayahitaji microscope na wala si siri, tusijifanye majuha wakati yanaongelewa hapa jamvini.

Na kukuthibitishia , hakuna mtu anayetetea kwanini Tanganyika itumie rasilimali nyingi kuibembeleza Zanzibar! Jibu jepesi litakuwa ''kwa usalama'' Usalama upi? kwanini si Malawi, Zambia, Rwanda au Kenya.
Ninakubaliana nawe juu ya Kikwete na ushiriki wake katika kuudhoofisha muungano. Hapo ndipo palipoanzia kuimarika kwa kundi lisilo penda muungano, na kuwapa ujasiri wa kuongeza juhudi. Samia, ni dhahiri kabisa kaja kumaliza kazi ya kuua muungano. Huyu ndiye alimaliza kero nyingi zilizokuwa zikidaiwa na hao wasiopenda muungano. Kazi hii aliifanikisha sana alipokuwa Makamu wa Rais. Magufuli ni kama alikuwa haoni chochote upande huo. Kiuhalisia Magufuli hakuwa na ukaribu wowote juu ya muungano. Bila shaka leo hii tungeweza kusema ni mmoja wa viongozi ambao muungano kwao uwepo usiwepo ni sawa tu.
Magufuli alikuwa 'pragmatic' , alijiuliza input and output ya Muungano. JPM hakukubaliana na kero zisizo na mantiki. Kwa mfano, kuacha bidhaa hafifu na za magendo kuingia kupitia Zanzibar ni kuinyima mapato Tanganyika iliyobeba muungano. Hakukubali deni la bilioni 60 za umeme lisamehewe tu kwa Uzanzibar.

JPM alitaka kuona Zanzibar inawajibika na kuwa mshirika, si mzigo kama ilivyo sasa ikiishi kwa hoja za ''kero''

SSH akiwa VP alikataliwa mengi ya muungano na JPM . Baada ya kifo ameyafanya kwa kasi kuliko Marais wote akiwemo Nyerere ! kulikoni? Amewafurshisha akina OMO na ni ''watetezi' wakimsifia! wanajua anadhoofisha muuungano! Kikwete, Karume na Samia wamedhoofisha muungano na ku upeleka ukingoni '
Mwisho, ifahamike natetea muungano na serikali moja. Hii haina maana sipendi Tanganyika iwepo kama nchi inayojitosheleza yenyewe bila ya muungano wa kiini macho wa serikali tatu Ni bora kuuondoa muungano moja kwa moja kuliko kujifanya tuna muungano wa aina hiyo. Huu wa serikali mbili wakati kukiwa na nchi huru ya Zanzibar hata siwezi kuuelezea ni kitu gani hiki.
Ni muumini wa ''Mama Tanganyika'' ikiwa kuna haja ya muungano wanatakiwa kuomba ni Wazanzibar!
Serikali 3 ni afadhaki kwao , Tanganyika haina kupoteza hata kama muungano haupo kabisa.
 
Serikali waharakishe ujenzi wa daraja la kutoka Dar es salaam kwenda Unguja ili tuone movement za mabasi na magari ya mizigo yakipishana usiku na mchana muungano uwe imara zaidi.
 
Mantiki ni kukuonyesha hata miaka 50,100 au 300 ikiwa muungano haukujengwa katika maridhiano ni tatizo.
Hili nilikuwa najibu hoja kwamba Mwalimu alisubiri muda upite ili 'assimilation' itokee tuelekee serikali 1.
Mwalimu" hakusubiri" kama unavyo sema. Huo muungano ulio anzishwa haukuwa ndiyo ngazi ya mwisho; ulitakiwa kuendelezwa na kuboreshwa hadi ufikie ngazi ya serikali moja.
Sijui "maridhiano" ni yapi hasa unayo yazungumzia wewe; kuwashirikisha raia wote katika uamzi? Kwani hilo haliwezekani kufanywa katika hatua zilizo pangwa wakati muungano ukiendelea kujengwa kama huu ambao ulikuwa ujenzi wake unaendelea? Lakini kama maridhiano unayolenga ni kuwamaliza akina OMO na kila mwenye sababu za kuto utaka muungano, hilo ni jambo lisilowezekana mahali popote.
Ni nadra nchi za kiarabu kuingilia vinchi masikikini vya Afrika kwasababu hakuna cha kupata.
Sudan, Somalia ni mifano michache ya kuanzia katika awamu mpya hii. Hayo unayozungumzia wewe ni maswala kongwe kabisa.
Mafuta na gesi kama raslimali tegemewa za nchi hizi zenye pesa nyingi kuliko wanavyoweza kujuwa namna ya kuzitumia, umuhimu wake utaendelea kupungua, tena kwa haraka sana katika miaka michache inayo kuja. Nchi hizi sasa zinatafuta njia mbadala za kuendelea kulinda utajiri na hadhi ya hizo nchi. Njia iliyo wazi mbele yao ni kujiingiza kwenye hizi nchi maskini kiakili, lakini tajiri sana kimali asili kama Tanzania. Unapokuwa na viongozi wasiokuwa na uwezo wa kutambua athari zinazoweza kutokana na uingiaji makubaliano kiholela kama wanavyo fanya hawa wa kwetu, ni dhahiri taifa linaandaliwa kwenda kwenye migogoro.
Kuna hisia za ajabu sana! ikiwa unahofia Waarabu Zanzibar kwanini usihofu uwepo wao Mombasa?
Hii haijawahi kuwa hofu yangu hata siku moja, na nimeeleza huko nyuma, hata kuhusu hiyo habari inayo enezwa siku zote kuhusu shinikizo la nchi za Magharibi kuundwa kwa muungano wetu. Sijawahi kukubaliana na dhana hiyo. Na hata sasa sihofii waarabu kuwa Zanzibar kivile; kwa hiyo msisitizo huu sioni umuhimu wake. Ndiyo maana nasema, mjadala unapokwenda kwenye mizunguko kiasi hiki, inakuwa inapoteza maana yake, kwa sababu tunarudia yale yale, hata kama tunatumia maneno tofauti na mifano tofauti.
Kuhusu Zanzibar kuna hisia zinafichwa fichwa lakini zinajulikana. Mh Lukuvi alisema wazi .
Haya yapo hayahitaji microscope na wala si siri, tusijifanye majuha wakati yanaongelewa hapa jamvini.
Yaleyale, tunarudiarudia tu. Kwani Lukuvi akisema, ndiyo ieleweke kuwa anawasemea waTanganyika wote? Kule OMO akisema, au yule mbunge akiropoka, ndiyo tujue ni waZanzibar wote wamesemewa?
SSH akiwa VP alikataliwa mengi ya muungano na JPM . Baada ya kifo ameyafanya kwa kasi kuliko Marais wote akiwemo Nyerere ! kulikoni? Amewafurshisha akina OMO na ni ''watetezi' wakimsifia! wanajua anadhoofisha muuungano! Kikwete, Karume na Samia wamedhoofisha muungano na ku upeleka ukingoni
Nakubaliana nawe juu ya haya.
Ni muumini wa ''Mama Tanganyika'' ikiwa kuna haja ya muungano wanatakiwa kuomba ni Wazanzibar!
Serikali 3 ni afadhaki kwao , Tanganyika haina kupoteza hata kama muungano haupo kabisa.
Hata siku moja sitaikana Tanganyika, lakini kama kuna muungano wa kupatikana taifa moja la Tanzania chini ya serikali moja inayowafanyia kazi waTanzania wote kwa haki, hilo ni muhimu zaidi kwangu kuliko kuwa na muungano kiini macho tu wa serikali tatu ilimradi tu Tanganyika irudi.
 
Serikali waharakishe ujenzi wa daraja la kutoka Dar es salaam kwenda Unguja ili tuone movement za mabasi na magari ya mizigo yakipishana usiku na mchana muungano uwe imara zaidi.
Nje ya mada.

Umewahi kujiuliza gharama za huo ujenzi au umeamua kuandika bila ushirikiano na ubongo.
 
Tunabishana na wakazi wanaoishi kwenye kifusi halafu wanaita ni inchi. Upuuzi.
 
Imekuwa ikinikwaza kuona baadhi ya watu Kwa manufaa Yao wamekuwa wakidai kwamba Tanganyika na Zanzibar ni nchi moja.

Huwezi kuwa Mzanzibar afu ukawa na uzalendo Kwa Tanganyika na kinyume chake maana ulio ukweli hizi ni nchi mbili tofauti na hazijawahi kuungana katika Nyanja nyingine yoyote Zaid ya upande wa siasa.

Tofauti na CCM kuna nini kingine kipo Tanganyika na Zanzibar in common?

Haifai na si afya Kwa mtanganyika kupewa mamlaka Mamkubwa ya kimaamuzi kuhusu Zanzibar na kinyume chake.

Mbena kuwa mkuu wa Wilaya ya chakechakw si Sawa na wala mpemba kuwa mkurugenzi wa halmashaur ya mpimbwe huku Katavi si Sawa.
 
Back
Top Bottom