Hili la serikali 1 umelirudia sana, huenda kuna hoja. Tujadili kidogo
1. Ikiwa sasa hivi Wazanzibar hawataki hata hizo 2 hiyo moja unawezaje kuwaeleza?
2. Serikali 1 ni kwa masilahi gani ya Tanganyika? Kwamba bila Zanzibar , Tanganyika ina kipi cha kupoteza!
JokaKuu
Huu mjadala nautaka sana, na ninajuwa wewe na mimi hatupo mbali mbali kuhusu hili swala la huu muungano wetu.
Nikukumbushe pia, siyo muda kitambo sana tumejadili haya haya; hasa kuhusu "waZanzibar kutoutaka muungano", jambo ambalo hatukuafikiana juu yake.
Msingi wangu wa kutaka serikali moja ni ule ule, uliokuwepo tangu kuasisiwa kwa muungano wenyewe. Lengo lilikuwa kufikia serikali moja baada ya hofu za "kumezwa" kufifia.
Hoja yangu ni kwamba hiyo hofu ya Zanzibar kumezwa haipo tena; kwani wengi wao tayari tunao hapa hapa Tanganyika. Hawa ni waTanzania, siyo waZanzibar tena.
Kelele za kikundi kidogo cha akina OMO na maJussa hakiwezi kamwe kuwa ndicho kiwe na uwezo wa kuamua hatma ya Tanzania.
Kwa bahati mbaya sana, CCM ndiyo imekuwa mlezi mkuu wa hiki kikundi na kusababisha hata waZanzibari walikokuwa tayari kuwa waTanzania kuanza kuwa na mashaka juu ya hatua hiyo. Kwa hiyo, kuondoka kwa CCM; kazi ambayo waTanzania sasa wapo ayari kabisa kuitekeleza kukiwepo na uongozi imara, hiyo ndiyo hatua muhimu itakayo tuelekeza kwenye serikali moja.
Serikali tatu, ni za nini tena! Miungano ya aina hiyo tuishiriki tukiwa huko kwenye EAC au huko SADC.
Ni matumaini yangu utaelewa msingi huu wa hoja yangu; na kusema kweli sidhani kuwa nitakuwa na hoja zaidi nje ya msingi huu katika majadiliano haya. Kwa hiyo naomba tusiyapanue sana bila ya sababu, kwa vile tunayo mambo mengine ambayo yanahitaji muda wetu.