Vita ya kisiasa baina ya Tanganyika na Zanzibar ipo wazi sasa

Vita ya kisiasa baina ya Tanganyika na Zanzibar ipo wazi sasa

Muungano huu hauna future.

Tunaambiwa yapo mambo ya muungano, iweje mtu asiye mtanganyika asimamie mambo ya Tanganyika yasiyo kwenye muungano!

Wanasheria wa Tanganyika watusaidie kututoa kwenye mkwamo huu.
Ila alivowepo mtanganyika akisimamia mambo ya zanzibar ilikuwa sawa?
Ref mzee mkapa 2001 alivyovamia Zanzibar na jeshi nakupiga watu hovyo bila ya rais wa zanzibar kufanya chochote
(Rais pale ni bosheni tu)
 
..muungano unalindwa na genge dogo la watawala toka Zanzibar na Tanganyika walioko CCM.

..lawama kuhusu muungano hazielekezwi mahala sahihi, na hicho ni kikwazo kikubwa ktk kudai muungano wa HAKI kwa pande zote.

Wazanzibari always wamedumu na msimamo wao kwenye suala la muungano katika mazingira yoyote, kwanini nyinyi huwa munalalamikia muungano Raisi anapokuwa Mzanzibari tu? mbona wakati wa JPM hamkuwa mkilalamika?
Nyinyi sio kama hamtaki muungano, bali hamtaki viongozi wa serikali watoke Zanzibar. Ni ubaguzi tu, munaojifichia kwenye mgongo wa matatizo ya Muungano.
 
Unaongeza tatizo palipo na tatizo mkuu. Ubinafsi wetu ni nini? Sipendi kutumia neno lako ila ukweli ni nyie ndio wabinafsi haswa, maana pamoja na mazonge yote ya huu muungano, angalau nyie mnafaidika na mambo kadhaa.

Nitajie kitu kimoja tu tunachofaidika nacho sisi waTanganyika (kama raia) kwenye huu muungano nami nitakuonesha mkaa mweupe.

Zanzibari imebanwa kisiasa na kiuchumi, na hapo ndipo kwenye tatizo kuu la huu muungano. Hawana mamlaka yoyote kwenye hayo mambo, wewe unataka kuleta story za nafasi za ukuu wa wilaya ama?
 
Unaongeza tatizo palipo na tatizo mkuu. Ubinafsi wetu ni nini? Sipendi kutumia neno lako ila ukweli ni nyie ndio wabinafsi haswa, maana pamoja na mazonge yote ya huu muungano, angalau nyie mnafaidika na mambo kadhaa.

Nitajie kitu kimoja tu tunachofaidika nacho sisi waTanganyika (kama raia) kwenye huu muungano nami nitakuonesha mkaa mweupe.

Ubinfasi wa watanganyika unaonekawa wazi mana kwanini Raisi wa JMT anapokuwa mtanganyika huwa hamlalamikii huu muungano? Kwanini mulalamike raisi akitokea upande wa Zanzibar tu? Mbona hatukuona Malalamiko kipindi cha JPM?
 
Zanzibari imebanwa kisiasa na kiuchumi, na hapo ndipo kwenye tatizo kuu la huu muungano. Hawana mamlaka yoyote kwenye hayo mambo, wewe unataka kuleta story za nafasi za ukuu wa wilaya ama?
Eti "hawana mamlaka YOYOTE kwenye hayo mambo"! Na kwanza unaposema imebanwa kisiasa na kiuchumi unamaanisha nini haswa mkuu? Sipingani asilimia mia na kauli yako ila from where I stand, kama mnaweza kuwa na bunge, serikali, na mfumo mzima wa siasa, what do you mean when you say mmebanwa kisiasa? Nani kawabana exactly?

Kwenye uchumi sawa kwakuwa hamna bank kuu ila napo kwa udogo wa eneo, ukubwa wa mapato pamoja na nyongeza mnayopokea kutoka serikali ya muungano, mngekuwa na viongozi wenye ufanisi sehemu kama Nungwi ni ya kuwekewa lami mwaka huu kweli!?

Sifa kuu yetu masikini ni kutafuta mtu wa kumlaumu kwa matatizo yetu ili kutafuta ahueni ya nafsi.

Najua umefika Bongo my brother, ni sehemu ngapi umeona raia hawana umeme kabisa na bado tunalazimika kuwahudumia rasilimali isiyotutosheleza hata sisi?

Wanafunzi wangapi wanakosa mikopo vyuoni ila bado board inalazimika kuwapa wanafunzi wa Zanzibar ili kuweka uwiano bila kujali kama mna board yenu inayojitegemea?

Ndugu zako wangapi wameajiriwa serikali yetu bila kudaiwa "kitambulisho cha mTanganyika mkazi"?

Humjui ndugu yako yeyote mwenye kiwanja bara ambacho serikali haitoamka siku moja na kuamua kumnyang'anya kihalali kabisa?
 
Heshima sana wanajamvi,

Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ambao uliasisiwa na watu wawili ambao sasa hawapo, tena bila ridhaa ya wananchi wa pande zote mbili sasa unapitia katika msuko suko mkubwa.

Ni wazi Mwl Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume waliziunganisha zao Tanganyika na Zanzibar pasipo ridhaa za wananchi wa pande zote mbili.

Muungano wao (Nyerere & Karume) kwa hakika umejaa kasoro nyingi mno, kuubadili au kuufanyia marekebisho kutahitaji kuzifumua katiba za nchi zote mbili jambo ambalo kwa sasa ni vigumu sana.

Zanzibar wana serekali yao, wana bunge lao, wana wimbo wao wa taifa lao, wana bendera yao, wana uraia wao (Uzanzibari), wana mkuu wao wa nchi, wana ardhi yao (nchi) wana kila kitu chao.

Tanganyika hawana wimbo wa taifa, hawana mkuu wao wa nchi, hawana ardhi yao, hawana bendera yao, kifupi Tanganyika hawana chochote.

Kuna Taifa la Tanzania (JMT) ambalo limepora kila kitu cha nchi ya Tanganyika. Bendera? Wimbo wa taifa, Bunge.

Tanganyika haina mtetezi wa rasilimali zake eg misitu, ardhi, bandari.

Raia wa nchi ya Zanzibar anaiongoza Tanganyika kupitia mgongo wa Muungano anauza kila rasilimali ya Tanganyika bila huruma kwakuwa hazina mtetezi.

Watanganyika wameamka sasa lugha ya Mch. Mtikila na sasa Mheshimiwa Lissu imeanza kueleweka hadi ndani ya CCM. Ugomvi mkubwa wa Kinana, Makamba na wanaCCM wengi ni Tanganyika kutawaliwa na Rais kutokea nchi ya Zanzibar ambaye amekuwa dalali mkubwa wa kuuza rasilimali za Tanganyika.

Wanaoitaka Tanganyika sasa ni Watanganyika wote bila kujali mipaka ya vyama.

Ngongo kwasasa Mjini Magharibi.

Pia soma
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Karume Wala hakuutaka muungano,baada ya mapinduzi, ambayo hayakuwa mipango ya karume Bali watu nje ya Zanzibar,karume hakuwa na askari wa kumlinda Bali askari 300 toka Tanganyika,akaambiwa aungane na bara au askari wataondolewa,akaenda bara na mwanasheria wake,alikua na madevu Kama ada ya wazanzibar kufuga ndevu,akaambiwa akanyoe,aliporudi toka salon akakuta mkataba umesainiwa,yaani alitoka Zanzibar Hadi bara kwenda kunyoa,baada ya hapo karume alionesha wazi kitoutaka muungano,aliyeing'ang'ania ndiye anayejua umuhimu wake, maana alinukuliwa alisema ningeweza ningevisukuma visiwa vya Zanzibar mbali na Tanganyika'
 
Ubinfasi wa watanganyika unaonekawa wazi mana kwanini Raisi wa JMT anapokuwa mtanganyika huwa hamlalamikii huu muungano? Kwanini mulalamike raisi akitokea upande wa Zanzibar tu? Mbona hatukuona Malalamiko kipindi cha JPM?
Ubinafsi huo unatokana na nini? Tungekuwa na serikali yetu ya Tanganyika pia, tungelalama?

Long story short, sisi raia wa Tanganyika kwa wingi wetu hatuutaki muungano kama ambavyo nanyi pia hamuutaki, pengine hatuutaki mara tatu zaidi yenu. Wenye faida nao wapo wametulia huko wanakula A/C.

Mngekuwa ni watu wenye utu japo kidogo mngeonyesha kutambua kuwa angalau nyie mnafaidika na mengi tofauti na sisi tusiofaidika na LOLOTE.
 
Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili tofauti kila moja ina Rais wake, jeshi lake, bendera yake, wimbo wa Taifa lake, benki kuu yake , passport yake, je bado tu hamuelewi?
Wewe mama kabla ya kuandika hiki ulichoandika ulifikiria sawa sawa?
Zanzibar Ina jeshi lake?
Zanzibar Ina benki kuu yake?
Zanzibar ina passport yake?

Si ajabu ukasema pia inatumia sarafu yake.

Moja ya kitu cha ajabu nilichosoma wiki hii Ni hiki, na bado tunalaumu sasa hivi elimu yetu imeshuka
 
Walipofuta tu uzi uliokuwa ukisema
"LENGO NI KUKITWAA HAKA KAENEO"
basiiii nikajua kabisa nimewagusa,
Huo ni ukweli na utabki ukweli daima, kwamba lengo ni kuimeza na kuimiliki na kuitawala Zanzibar baada ya kushindwa kuitawala kiujanja ujanja.

Kama hamna lengo hilo msingefuta ule uzi, ili tuone changamoto zipo wapi, lakini kwa kuufuta mumedhihirisha kabisa lengo lenu

Mtafuta hapa tu kwenye jukwaa, lakini ndani ya mioyo yetu hamuwezi na hamtaweza kamwe
 
Walipofuta tu uzi uliokuwa ukisema
"LENGO NI KUKITWAA HAKA KAENEO"
basiiii nikajua kabisa nimewagusa,
Huo ni ukweli na utabki ukweli daima, kwamba lengo ni kuimeza na kuimiliki na kuitawala Zanzibar baada ya kushindwa kuitawala kiujanja ujanja.

Kama hamna lengo hilo msingefuta ule uzi, ili tuone changamoto zipo wapi, lakini kwa kuufuta mumedhihirisha kabisa lengo lenu

Mtafuta hapa tu kwenye jukwaa, lakini ndani ya mioyo yetu hamuwezi na hamtaweza kamwe
Mods kufuta post kunahusiana vipi na kutawala/kutwaa huko unaposema?
Kwamba wewe kuweka post ni kikwazo kwa wanaotaka kufanya hivyo?
 
Hapo patamu Rais wa Zanzibar ni Mzanzibar,Rais wa Tanganyika ni Mzanzibar !.

Nchi mbili zote zinaongozwa na Raia kutoka nchi moja ya Zanzibar.Tanganyika hakuna watu wa kuongoza Tanganyika.

Hapa tatizo ni katiba mbovu ambayo imeizika Tanganyika.
Kuna mambo mtu ukisoma huku unabaki na maswali
Kwa jinsi ulivyojibu unakibaliana na alichosema kwamba Zanzibar Ina jeshi lake? Ina benki kuu yake? Na Ina passport yake?
 
Back
Top Bottom