Vita ya kisiasa baina ya Tanganyika na Zanzibar ipo wazi sasa

Nchi ya Zanzibar ina idadi ya watu 836,000 ina wabunge 80.

Mkoa wa Dar idadi ya watu 8,120,000 wabunge 13.

Uwalikolishi wa Zanzibar ni mkubwa sana ukilinganisha na idadi ya watu na ukubwa wa eneo.

Hao wabunge 80 wanajadili na kupiga kura hata kwa masuala ambayo si ya muungano.Mfano masuala ya kilimo,Tamisemi,Maji na nk.

Wazanzibari wana baraza lao la Wawakilishi ambalo Mtanganyika ni haramu kuingia huko kwakuwa wanajadili masuala yao ikiwemo kutunga sheria mbali mbali kama kumtambua Rais wa Zanzibar kama Mkuu wa nchi.Kutengeneza sheria ya uRaia wa Zanzibar na nk.
..tena kati ya hao 80,kuna Wabunge toka Baraza la Wawakilishi, nadhani wapo watano(5) eti kwa ajili ya kulinda MASLAHI ya Znz,kana kwamba hawa 75 hawawezi kulinda wala kutetea maslahi ya Znz..

Tunataka nasi Watanganyika tuwe na Wawakilishi ndani ya Baraza la Wawakilishi ili kulinda Maslahi ya Tanganyika..NDIO

Pia kwa umasikini wetu,hatuhitaji kuwa na wabunge 300+ , kwa kuanzia tupunguze hao 80 toka Znz, 20 tu WANATOSHA..huku Tanganyika wabunge wawili(02) kila mkoa..wakuchaguliwa na makundi maalumu,refer Rasimu ya Katiba ya Warioba...
TUNAPOTEZA FEDHA NYINGI SANA KWENYE UTAWALA!
 
Proof me wrong
I'm not certain of what credentials you expect me to bring forth so as to "prove" you wrong, ila I am well informed on the matter na Zanzibar pamoja na kuwa na immigration service ya kujitegemea, haina passport yake yakujitegemea. Iliyokuwepo ni ya miaka ya zamani kabla ya muungano. Na pia Zanzibar haina benki kuu yake as you say.
 
Kama upo uwezekano wa Mtanganyika kugombea ubunge Zanzibar au kuongoza nchi ya watu wa Zanzibar bila vizingiti vya kusheria muungano ungeeleweka.

Kama Mtanganyika angeweza kununua ardhi kama raia wa Tanzania huu muungano tusingeupigia kelele.

Kwani Raisi wa Zanzibar si Mtanganyika kutoka Mkuranga?

Kwani shida ni uzanzibari au uislamu?
 
Punguani mkubwa,Haki ipi wewe fukara wa nanyumbu umeikosa?

Rais ndio Huwa anatunga sheria za kufanya udalali? Au Serikali imejaa Watanganyika wangapi na Wazanzibar wangapi?

Huku ni kukosa akili
Nyumbu? Siyo.
Sikiliza chawa, Wazanzibari wanayo serikali yao,Katiba yao,Bunge lao na hata Mahakama yao.
Kumbe unaongeaongea hujui kitu chochote, hujui hata kuwa mkataba wa dipiwedi ulisainiwa halafu baadaye ukapelekwa bungeni kama kiinimacho.
Kwenye Muungano wazanzibari wana haki mara mbili, wakati haki ya Watanganyika iko mara moja, isitoshe kwanini Rais yuko obsesed na mali za Tanganyika wakati na Zanzibar kuna mali? Yeye si ndio Rais wa muungano?
 
Nchi ya Zanzibar ina idadi ya watu 836,000 ina wabunge 80.

Mkoa wa Dar idadi ya watu 8,120,000 wabunge 13.

Uwalikolishi wa Zanzibar ni mkubwa sana ukilinganisha na idadi ya watu na ukubwa wa eneo.

Hao wabunge 80 wanajadili na kupiga kura hata kwa masuala ambayo si ya muungano.Mfano masuala ya kilimo,Tamisemi,Maji na nk.

Wazanzibari wana baraza lao la Wawakilishi ambalo Mtanganyika ni haramu kuingia huko kwakuwa wanajadili masuala yao ikiwemo kutunga sheria mbali mbali kama kumtambua Rais wa Zanzibar kama Mkuu wa nchi.Kutengeneza sheria ya uRaia wa Zanzibar na nk.
Nchi ni Nchi na mkoa ni mkoa
Kihadhi haziwezi kuwa sawa bandugu 🙌
 
Wazanzibar wanaona Kama wanatukomoa Tanganyika Ila Tanganyika itakapoamka wanaweza kuchinja viongozi wao
Hakuna mambo ya kuchinjana hapa !
Marehemu Karume alisemaga tangu Enzi hizo kwamba huu Muungano ni kama mtu amevaa koti, ukiona limekubana unalivua tu na maisha yanaendelea kama kawaida !😅🙌👍
 
Heshima sana wanajamvi,

Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ambao uliasisiwa na watu wawili ambao sasa hawapo, tena bila ridhaa ya wananchi wa pande zote mbili sasa unapitia katika msuko suko mkubwa.

Ni wazi Mwl Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume waliziunganisha zao Tanganyika na Zanzibar pasipo ridhaa za wananchi wa pande zote mbili.

Muungano wao (Nyerere & Karume) kwa hakika umejaa kasoro nyingi mno, kuubadili au kuufanyia marekebisho kutahitaji kuzifumua katiba za nchi zote mbili jambo ambalo kwa sasa ni vigumu sana.

Zanzibar wana serekali yao, wana bunge lao, wana wimbo wao wa taifa lao, wana bendera yao, wana uraia wao (Uzanzibari), wana mkuu wao wa nchi, wana ardhi yao (nchi) wana kila kitu chao.

Tanganyika hawana wimbo wa taifa, hawana mkuu wao wa nchi, hawana ardhi yao, hawana bendera yao, kifupi Tanganyika hawana chochote.

Kuna Taifa la Tanzania (JMT) ambalo limepora kila kitu cha nchi ya Tanganyika. Bendera? Wimbo wa taifa, Bunge.

Tanganyika haina mtetezi wa rasilimali zake eg misitu, ardhi, bandari.

Raia wa nchi ya Zanzibar anaiongoza Tanganyika kupitia mgongo wa Muungano anauza kila rasilimali ya Tanganyika bila huruma kwakuwa hazina mtetezi.

Watanganyika wameamka sasa lugha ya Mch. Mtikila na sasa Mheshimiwa Lissu imeanza kueleweka hadi ndani ya CCM. Ugomvi mkubwa wa Kinana, Makamba na wanaCCM wengi ni Tanganyika kutawaliwa na Rais kutokea nchi ya Zanzibar ambaye amekuwa dalali mkubwa wa kuuza rasilimali za Tanganyika.

Wanaoitaka Tanganyika sasa ni Watanganyika wote bila kujali mipaka ya vyama.

Ngongo kwasasa Mjini Magharibi.

Pia soma
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Kama ni lawama basi sisi wenyewe ndo wakujilaumu maana aliye leta haya mamno ya mungano ni mtu toka bara(JKN) na sasa wazanzibari wanatutawala kwahiyo tutulie dawa ituingie
 
Nyie mnapiga kelele tu hamna mnachujua mnaongozwa na chuki kuliko huo uhalisia wa muungano. Kule Sudan ilikuwa rahisi kugawana vipande vya archi kutokana na nini??? Alafu jiulize kwann uamsho walivyokuwa wanakataa muungamo mnliwaita magaidi wemetumwa na western
 
Hakuna mambo ya kuchinjana hapa !
Marehemu Karume alisemaga tangu Enzi hizo kwamba huu Muungano ni kama mtu amevaa koti, ukiona limekubana unalivua tu na maisha yanaendelea kama kawaida !😅🙌👍
Kuna sehemu nimeongelea kuchinjana, kile ni kisiwa ambacho kinameguka Kila siku au hufahamu mpango wa UNESCO kukihifadhi, Kama wanakosa Had mchanga wa kujengea unategemea nini
 
Kama ni lawama basi sisi wenyewe ndo wakujilaumu maana aliye leta haya mamno ya mungano ni mtu toka bara(JKN) na sasa wazanzibari wanatutawala kwahiyo tutulie dawa ituingie
Niliwahi kusikia kuwa JKN ilimbidi kuhangaikia kuungana na Zanzibar kama clause moja wapo kati ya nyingi tulizopewa na Richard Turnbull wakati wa kuhangaikia uhuru na wala haikuwa kwa mapenzi yake mwenyewe. Hivyo maslahi ya muungano hayapo kwa CCM tu, nadhani hata Uingereza inahusika.
 
Yes naweza kukubaliana na wew japo sina hakika kama hao mabeberu wanafaidika mpaka sasa
 
Halafu huyu Mama kutoka nchi ya Zanzibar (In Lissu voice) kakuta Watanganyika wanaunganishiwa umeme wa REA kwa 27,000 huku Tanganyika kauondoa wakati huo huo kasamehe deni la Umeme nchi ya Zanzibar!.
 
Watanganyika ni wapumbavu sana, Wana watu zaidi ya milioni 60 lakini wanatawaliwa na nchi isiyo na watu hata milioni 2 na ubaya huyo mtu anafanya exploitation za mali zao maana anajua baada ya mda atarudi zao kwao kama wakoloni walivyofanya.
Na ubaya ni kwamba kuna watu wenye mamlaka na nafasi wako wanachekeana na kumsapot mali zetu natural resources zikiuzwa na kutaifishwa.
Ujinga wa kiwango cha SGR
 
Halafu huyu Mama kutoka nchi ya Zanzibar (In Lissu voice) kakuta Watanganyika wanaunganishiwa umeme wa REA kwa 27,000 huku Tanganyika kauondoa wakati huo huo kasamehe deni la Umeme nchi ya Zanzibar!.
Ni ujuha wa hali ya juu Baada ya mkoloni kuitawala tanganyika sasa ni zamu ya mzanzibar.
No wonder nchi za jirani wanawashangaa watanganyika.
 
I'm not certain of what credentials you expect me to bring forth so as to "prove" you wrong, ila I am well informed on the matter na Zanzibar pamoja na kuwa na immigration service ya kujitegemea, haina passport yake yakujitegemea. Iliyokuwepo ni ya miaka ya zamani kabla ya muungano. Na pia Zanzibar haina benki kuu yake as you say.
Uhamiaji, Polisi, JWTZ, TISS ni Jamhuri ya Muungano. Hakuna Hati ya kusafiria ya Zanzibar.

Watawala wa Zanzibar walikasirika sana Magufuli aliposema kitambulisho kitakiwacho mtu anapoomba Hati ya kusafiria ni NIDA tu na cha Mzanzibari hakitakiwi.
 
Heshima sana wanajamvi,

Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ambao uliasisiwa na watu wawili ambao sasa hawapo, tena bila ridhaa ya wananchi wa pande zote mbili sasa unapitia katika msuko suko mkubwa.

Ni wazi Mwl Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume waliziunganisha zao Tanganyika na Zanzibar pasipo ridhaa za wananchi wa pande zote mbili.

Muungano wao (Nyerere & Karume) kwa hakika umejaa kasoro nyingi mno, kuubadili au kuufanyia marekebisho kutahitaji kuzifumua katiba za nchi zote mbili jambo ambalo kwa sasa ni vigumu sana.

Zanzibar wana serekali yao, wana bunge lao, wana wimbo wao wa taifa lao, wana bendera yao, wana uraia wao (Uzanzibari), wana mkuu wao wa nchi, wana ardhi yao (nchi) wana kila kitu chao.

Tanganyika hawana wimbo wa taifa, hawana mkuu wao wa nchi, hawana ardhi yao, hawana bendera yao, kifupi Tanganyika hawana chochote.

Kuna Taifa la Tanzania (JMT) ambalo limepora kila kitu cha nchi ya Tanganyika. Bendera? Wimbo wa taifa, Bunge.

Tanganyika haina mtetezi wa rasilimali zake eg misitu, ardhi, bandari.

Raia wa nchi ya Zanzibar anaiongoza Tanganyika kupitia mgongo wa Muungano anauza kila rasilimali ya Tanganyika bila huruma kwakuwa hazina mtetezi.

Watanganyika wameamka sasa lugha ya Mch. Mtikila na sasa Mheshimiwa Lissu imeanza kueleweka hadi ndani ya CCM. Ugomvi mkubwa wa Kinana, Makamba na wanaCCM wengi ni Tanganyika kutawaliwa na Rais kutokea nchi ya Zanzibar ambaye amekuwa dalali mkubwa wa kuuza rasilimali za Tanganyika.

Wanaoitaka Tanganyika sasa ni Watanganyika wote bila kujali mipaka ya vyama.

Ngongo kwasasa Mjini Magharibi.

Pia soma
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Wananchi wa kawaida wa Tanzania(Watanganyika na Wazanzibari) wanapenda muungano kwa kuwa unawapa fursa zaidi za kiuchumi.
Changamoto ni kwa wanasiasa ambao huweka maslahi yao binafsi mbele zaidi ya yale ya taifa.
Hata hivyo, wananchi wanatakiwa kujengewa uwezo wa kuwadhibiti wanasiasa kifikra na kivitendo kwa mustakabali mwema wa taifa.
 
Back
Top Bottom