Vita ya kisiasa baina ya Tanganyika na Zanzibar ipo wazi sasa

Vita ya kisiasa baina ya Tanganyika na Zanzibar ipo wazi sasa

Ni wajibu wetu sisi Watanganyika kuunganisha nguvu zetu bila kujali vyama, dini na kanda kuikomboa Tanganyika yetu kutoka mikononi mwa mkoloni mweusi anayeuza rasilimali zetu kwa kasi kama moto wa nyika.
Hakika
 
Wananchi wa kawaida wa Tanzania(Watanganyika na Wazanzibari) wanapenda muungano kwa kuwa unawapa fursa zaidi za kiuchumi.
Changamoto ni kwa wanasiasa ambao huweka maslahi yao binafsi mbele zaidi ya yale ya taifa.
Hata hivyo, wananchi wanatakiwa kujengewa uwezo wa kuwadhibiti wanasiasa kifikra na kivitendo kwa mustakabali mwema wa taifa.
Mkuu nadhani hapa uhalisia ni vice versa
 
Uhamiaji, Polisi, JWTZ, TISS ni Jamhuri ya Muungano. Hakuna Hati ya kusafiria ya Zanzibar.

Watawala wa Zanzibar walikasirika sana Magufuli aliposema kitambulisho kitakiwacho mtu anapoomba Hati ya kusafiria ni NIDA tu na cha Mzanzibari hakitakiwi.
Sahihi kabisa mkuu, asante.
 
Wanasiasa wa CCM Zanzibar wanapenda Muungano kama ulivyo kwa sababu unawapa uhakika wa kugawana vyeo
Raisi
Makamo
Mawaziri
Makatibu wakuu
Wakurugenzi
Wabunge
Wawakilishi na wengineo
 
Napo Rais alikuwa Mzanzibari ndio maana chokochoko zilikuwepo.

Hoja Iko wazi hamtaki Rais awe Mzanzibari,Sasa Kwa nini muwalazimishe Wazanzibar kwenye Muungano ambao hamuwezi kutenda Haki?
Usichofahamu ni kuwa hata Wazanzibari wenyewe hawataki muundo wa sasa wa serikali mbili wanataka serikali tatu ambazo zitawapa madaraka kamili ya Zanzibar yao, wanaokumbatia huu muungano upande wa Zanzibar ni kada ya viongozi wao ambao wananufaika wao binafsi na familia zao kwa mafao wanayopata.
 
Niliwahi kusikia kuwa JKN ilimbidi kuhangaikia kuungana na Zanzibar kama clause moja wapo kati ya nyingi tulizopewa na Richard Turnbull wakati wa kuhangaikia uhuru na wala haikuwa kwa mapenzi yake mwenyewe. Hivyo maslahi ya muungano hayapo kwa CCM tu, nadhani hata Uingereza inahusika.
Angalau sasa hapa kuna kichwa kinaweza kusikilizwa......
 
Usichofahamu ni kuwa hata Wazanzibari wenyewe hawataki muundo wa sasa wa serikali mbili wanataka serikali tatu ambazo zitawapa madaraka kamili ya Zanzibar yao, wanaokumbatia huu muungano upande wa Zanzibar ni kada ya viongozi wao ambao wananufaika wao binafsi na familia zao kwa mafao wanayopata.
Wao hawataki siku zote ila sio kwamba hawataki wasiongize Tzn kama nyie ambavyo hamtaki.
 
Mzee mwenzangu Ngongo nasikia hapa kijiweni zanzibari inajengeka haswa huko, kila sehemu?.
 
..sio kwamba hatutaki Raisi wa muungano toka Zanzibar.

..tunachotaka ni serikali ya Tanganyika, na muungano wa serikali 3.

..baada ya hapo hakutakuwa na shida ikiwa Raisi wa muungano atatoka Zanzibar.

MKuu hicho mbona ndio kilio cha Zanzibar kwa miaka mingi sana, na nyinyi ndio mumekuwa mikiwakebehi kuwa wanapenda kulialia
 
Wazanzibar nilishaawambia siku nyingi.ADUI YAO NI CCM.waanze kwanza kumtoa ccm zanzibar alafu ndo waanze kudai nchi ÿao.vinginevyo zitabaki kuwa kelele tu
 
watanganyika ni wabinafsi sana
Unaongeza tatizo palipo na tatizo mkuu. Ubinafsi wetu ni nini? Sipendi kutumia neno lako ila ukweli ni nyie ndio wabinafsi haswa, maana pamoja na mazonge yote ya huu muungano, angalau nyie mnafaidika na mambo kadhaa.

Nitajie kitu kimoja tu tunachofaidika nacho sisi waTanganyika (kama raia) kwenye huu muungano nami nitakuonesha mkaa mweupe.
 
MKuu hicho mbona ndio kilio cha Zanzibar kwa miaka mingi sana, na nyinyi ndio mumekuwa mikiwakebehi kuwa wanapenda kulialia

..muungano unalindwa na genge dogo la watawala toka Zanzibar na Tanganyika walioko CCM.

..lawama kuhusu muungano hazielekezwi mahala sahihi, na hicho ni kikwazo kikubwa ktk kudai muungano wa HAKI kwa pande zote.
 
Kwa hiyo unakubalina na hoja kwmaba kumbe shida sio Muungano bali Mzanzibari hatakiwi kuwa Rais? Kuna haja ya Muungano mpaka hapo?

..aina ya muungano ndio inasababisha Watanganyika wajisikie wanadhulumiwa ikiwa Raisi wa muungano atatoka Zanzibar.

..kuna haja ya muungano wa serikali 3 ambao utatenda HAKI kwa Tanganyika na Zanzibar bila kubagua.
 
Heshima sana wanajamvi,

Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ambao uliasisiwa na watu wawili ambao sasa hawapo, tena bila ridhaa ya wananchi wa pande zote mbili sasa unapitia katika msuko suko mkubwa.
Muungano huu hauna future.

Tunaambiwa yapo mambo ya muungano, iweje mtu asiye mtanganyika asimamie mambo ya Tanganyika yasiyo kwenye muungano!

Wanasheria wa Tanganyika watusaidie kututoa kwenye mkwamo huu.
 
Muungano huu hauna future.

Tunaambiwa yapo mambo ya muungano, iweje mtu asiye mtanganyika asimamie mambo ya Tanganyika yasiyo kwenye muungano!

Wanasheria wa Tanganyika watusaidie kututoa kwenye mkwamo huu.
Hili nalo neno.
 
Zanzibar hawataki muungano, wanaon'ganga'nia ni wabara na ndio maana mkampa urais mzanzibari ili kuwapoza, sasa vumilieni tu sindano iwaingie

Au kama vipi si muvunje tu muungano kwanini mnalazimisha?
Yaani mnaboaaaaa, kitu hamkitaki lakini bado mnakin'ganga'nia
Ajaaaabuuu kweli kweli
 
Back
Top Bottom