Vita ya madaraka Makanisani ilivyoanzisha Kanisa halisi kutoka Siloam!

Vita ya madaraka Makanisani ilivyoanzisha Kanisa halisi kutoka Siloam!

Wachokonozi wako sahihi sena watu wanawapuuzia tu
Ukimsikiliza yule jamaa utagundua kuwa binadamu ni kitu dhaifu mno na ndo maana akina KIBOKO YA WACHAWI na MWAMPOSA wanaishi maisha mazuri kupitia shida za wengine,, its just a simple thing ila inahitaji knowledge kubwa.
 
Ukimsikiliza yule jamaa utagundua kuwa binadamu ni kitu dhaifu mno na ndo maana akina KIBOKO YA WACHAWI na MWAMPOSA wanaishi maisha mazuri kupitia shida za wengine,, its just a simple thing ila inahitaji knowledge kubwa.
Wafia dini hawamuelewi sema mi namuelewa sana anaongea vitu vina make sense kabisa
 
UMEWAHI kusikia kanisa liitwalo KANISA HALISI LA MUNGU BABA? Wanavaa nguo nyeupe kanisa zima, ibada zao nyingi zinarushwa STAR TV?Hawataji jina MUNGU wala YESU wao wanaita CHANZO HALISI 😁Hapa nakuletea historia fupi ya kiongozi huyo maarufu kwa jina la ELISHA ELIYA MIAKA 1000 (anaandika michuzi blog)

Rusomo ambaye baadae alijulikana kwa jina la Elisha Eliya Miaka1000 akiwa na matatizo mbalimbali ambapo aliombewa na kufunguliwa kisha akajiunga na huduma ya Siloam Bible School ambapo alifundishwa utumishi.

Wakati tayari akiwa kuhani wa kanda ya Dar es Salaam Miaka 1000 alisaliti kiapo cha utumishi, kwani baada ya kiongozi mkuu wa huduma hiyo kutwaliwa na kabla ya mchakato wa kumpata kiongozi mwingine, yeye alijivua safu ya ukuhani na akajipa cheo cha Mzeituni, Mpaka Mafuta, Mzee wa Siku, Wakili wa Mungu, mungu aliyetuma wote, baba wa uzao, baba halisi nk.

Mpaka aliacha kabisa imani aliyoikuta Siloam na aliazimia kupora thamani, uzuri na kibali cha kusanyiko la Siloam akiwa kwenye majengo ya Siloam.

Aliwapindua waumini kwa kuingiza mafundisho yaliyoacha maswali na hadithi za Kanisa Halisi la Mungu baba. E. E. Miaka1000 alitumia mbinu mbalimbali za kuvuruga safu za makuhani mikoani ambapo aliwashawishi waungane naye kusaliti maono ya mwanzilishi wa Huduma.

Ili kuhalalisha mapinduzi hayo alitunga Katiba yake akitaka kusajili The Pool of Siloam Church lakini haikupitishwa na Serikali kwa kuwa hakuwa mmoja wa viongozi wa Kikatiba. Hivyo, alizalisha mzozo ili Serikali ifute usajili halali wa Siloam Ministry InternationaI.

Hata hivyo hilo nalo halikufanikiwa.

Hivyo yeye na kundi lake la waumini aliofanikiwa kuwashaiwishi katika vituo mbalimbali waliendelea kutumia mali na majengo ya SMI kufanyia ibada na kuondoka na sadaka.


Serikali, viongozi na makuhani waaminifu walijitahidi kunusuru mgogoro huo lakini Miaka 1000 alikataa utengamano kwa madai kuwa yeye ni mungu na hawezi kujadiliwa, kuhojiwa wala kushauriwa.

WAUMINI WAKE MJE HAPA 😂😂😂TUNA KIKAO
Uwendawazimu kama uwendawazimu mwingine..
 
hilo sio kanisa, ni cult ya munuo, mchaga mmoja wa bombang'ombe aliyekuwa anasali lutheran akaamua kufungua kituo chake. ni kanisa la kupumbavu kuliko yote kwasababu hata wanachoongea hawakijui, na wanachofanya hawakijui. na mpaka leo wanaamini munuo alikuwa mbadala wa Yesu, na alipaa wakati alikufa kwa kuugua tetenas akakalishwa mochwari pale lugalo walipoona ataoza wakaenda kuzika kule njia ya bagamoyo. hawa ndio wakristo pekee duniani wanaoamini Damu ya Yesu na Jina la Yesu vimepungua nguvu, haviokoi tena, mapepo na mashetani yameshazoea nguvu za JIna na Damu ya Yesu, hivyo wanapoomba wanaomba kwa mungu baba. pia, munuo aliwaaminisha kwamba yeye alishapigana na shetani na alishamuua shetani, wanaamini hadi leo kwamba shetani alishakufa na aliuawa na mtume Munuo. ajabu yake, shetani bado yupo anaendelea kuwatawala na kuwadanganya. kati ya uwongo uliowahi kuanzishwa kidini, huu wa hawa jamaa ni wa kwanza. ajabu sana.
 
Back
Top Bottom