Vita ya madawa ya kulevya aliyoanzisha Makonda ilikuwa ni “bosheni”?

Vita ya madawa ya kulevya aliyoanzisha Makonda ilikuwa ni “bosheni”?

jmushi1

Platinum Member
Joined
Nov 2, 2007
Posts
26,540
Reaction score
25,834
Wanajamvi, wakati mkuu wa mkoa wa Dar Makonda alipokuja na ile listi ya manguli wa madawa ya kulevya, nilijuwa tu ilikuwa ni “bosheni”

Nilisema kuna watu anawaondoa kwenye biashara ili baadhi ya wengineo wanufaike. Cha msingi hapa, ni ku create kundi rafiki la madawa hayo.

Kuna taarifa kuwa marekani imeitaja Dar es salaam kama center kubwa ya kupitisha madawa hayo. Je madawa hayo yanapitishwa kimkakati?

Nimejiuliza sana kuhusu hili, kwasababu kuna mataifa mengi tu ambayo serikali zake zimekuwa zikitumia madawa ya kulevya na biashara nyingine haramu ili kuweza kuziendesha serikali pamoja na kugharamikia mambo yao binafsi.

Taifa kama North Korea ni kinara wa biashara hizo kupelekea mataifa mengine. Kuna ambao ni pirates mfano Somalia nk
Wakati Makonda anayataja hayo majina, nilijiuliza sana kwasababu kingpins wenyewe hawakuwa wameguswa.

Sasa kama Makonda mwenyewe ni mtu influential hapa nchini kwetu, je haiwezekani ikawa ni dalili za kuwa ni mtu muhimu sana kwenye serikali?

Kuna wengi wanaodai kuwa marekani wanatafuta sababu. Na kuna watakaochokonoa suala la Pompeo kumpiga marufuku Makonda asikanyage marekani yeye na mkewe.

Sasa issue kama hii, ni wazi kuwa yeye watakuwa wanamuhusisha moja kwa moja maana ndo gavana wa jiji.

Hii hapa chini ndo listi au majina ya ma kingpins wa madawa ya kulevya waliotajwa na Makonda, ambapo gazeti la Mtanzania lilimpamba kwamba “amejitoa muhanga” kwenye vita ya madawa ya kulevya...

“Mkuu huyo wa mkoa aliwataja wasanii wanaodaiwa kutumia dawa za kulevya kuwa ni Khalid Mohamed marufu kama TID, Wema Sepetu, Rashidi Makwiro (Chidy Benz) na wengine akiwataja kwa jina moja moja Rachel, Sniper na Tito.

Makonda aliwataja watu wengine aliowanasa kuwa ni Said Masudi Lina ‘ Alteza’, Nassor Mohamed Nassor, Bakari Mohamed Khelif na aliyemtaja kwa jina moja la Omary”

Seriously? Nadhani aliwataja pia Mbowe na Gwajima amongst others...

Wengine waliotajwa na Makonda ni mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azzan ambaye alikuwa kipa wa timu ya wabunge na timu ya wabunge wa Simba wakati alipokuwa mbunge, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji.

Pia Makonda aliwataja watu 65 ambao alidai wanatakiwa kufika katika kituo cha polisi kwa ajili ya zoezi hilo la mahojiano katika kampeni yake ya kuendeleza kupambana na utumiaji na biashara ya dawa ya kulevya.

Majina mengine maarufu yaliyokuwepo katika orodha hiyo ni pamoja na mfanyabiashara maarufu wa nguo Hussein Pambakali, na wamiliki wa Slipway na Yatchy Club.

Sasa kama hii biashara imeongezeka baada ya vita vya Makonda, maneno yangu yale yanaanza kuonyesha ukweli wake.

Kwasababu kuna ambao wanashamgazwa na uwezo wa pesa wa Makonda nk. Wengine wanasema ni ufisadi dhidi ya kodi zetu nk.

Kuna term ambayo inatumika, “Narco-State”, ambapo kunakuwepo na watu wafanyabiashara wa madawa hayo ambao wanawezeshwa na serikali kama nilivyosema North Korea.

Lakini neno lenyewe lilianza kupata umaarufu kule Bolivia ambapo kwa mara ya kwanza, kulitokea mapinduzi ambayo yalifadhiliwa na biashara hiyo ya madawa ya kulevya.

Kwakifupi tu, hili suala siyo la kufumbia macho hata kidogo. Je wamarekani wenyewe wanaweza kutoa taarifa zaidi kuhusu walichokiona?

Certainly, kwasasa gavana wa Dar sidhani kama anakubaliana na taarifa hii ya wamarekani. Ila nachojuwa, ukiwepo kwenye listi ya wamarekani wanakuja kukunyakua kama wale tai wanavyonyakua.
 
Ngoja tuone Marekani ikiingiza mkono wake kwenye hili hali itakuwaje, maana Marekani ndio wenye vita vya kweli dhidi ya madawa ya kulevya sio sisi Waafrika wenye njaa ambao tuko tayari kuchukua hongo kubwa na kuwaacha wafanya biashara wa madawa ya kulevya wakitamba wakati madawa hayo yanakwenda kuathiri ndugu, watoto, jamaa na kizazi chetu na taifa kwa ujumla.

ᴱᵛᵉʳʸᵇᵒᵈʸ ˡᵒᵛᵉˢ ᵃ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ [emoji377]
 
Very well said!👏🏽
 
Hata Mimi nilipoona listi hiyo ikiwajumuisha pia mtumishi wa Mungu, Mchungaji Gwajima na kiongozi wa kambi ya upinzani, Freeman Mbowe, nilijua hakika hiyo listi ni "bosheni"
Unaweza kuta kuna ambao wanayapitisha with impunity. Na siwezi kushangaa zama hizi ukiunga mkono juhudi hauguswi. Hapo ndipo nilikata tamaa na utawala huu. Yani kuna watu hawagusiki hata iweje. Unaweza kuta kuna mambo mengi tusiyoyafahamu nyuma ya pazia.

Halafu hiyo pesa ya kununua wapinzani (kama ni kweli), inatoka wapi?
 
Nitakupa jibu baada ya kuvaa jezi ya GSM kesho wakati wa mechi zamani tulikuwa tunavaa ya quality group ya MANJI.TUNA BOSS MPYA na jezi mpya ila hela ni zile zile.Hii biashara bwana.........wacha tuangalie mpira kwanza halafu KOFFI OLOMIDE na muziki wake baadaye
 
Bashite alikwenda South Africa baada ya mapambano yake ya madawa ya kulevya na alipiga picha na Daudi Kanyau mmoja wa ma don wa biashara hiyo ambae amehamia South.

Ile picha yake na Daudi Kanyau ilileta maswali mengi yasiyo na majibu.
 
Bashite alikwenda South Africa baada ya mapambano yake ya madawa ya kulevya na alipiga picha na Daudi Kanyau mmoja wa ma don wa biashara hiyo ambae amehamia Soutt.

Ile picha yake na Daudi Kanyau ilileta massaliteit mengi yasiyo na majibu.
Hebu iweke ile picha kama naikumbuka, walionekana wakipeana mkono pembeni yao alikuweko msichana anaesemekana ni mke wa kaCat.

ᴱᵛᵉʳʸᵇᵒᵈʸ ˡᵒᵛᵉˢ ᵃ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ [emoji377]
 
IMG_4918.JPG

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Picha hiyo hapo huyo tall ndio kanyau mwenyewe haya endelea

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Bashite alikwenda South Africa baada ya mapambano yake ya madawa ya kulevya na alipiga picha na Daudi Kanyau mmoja wa ma don wa biashara hiyo ambae amehamia South.

Ile picha yake na Daudi Kanyau ilileta maswali mengi yasiyo na majibu.
Ile list ya Makonda kukosekana majina ya Daudi Kanyau na Kinje Ngombale ilikuwa utani kabisa
 
Jamaa wanapendana tu jamani au walikutan ghafla tu!! mbona hata LE MUTUZ na KINJEKITLE na GSM na hao kwenye picha ni marafiki kwahyo ina maana wote wanapiga vita biashara ya madawa au!!
Kwahiyo kumbe hakuwaweka kwenye listi kwasababu wanapendana?🤦🏾‍♂️
 
Bashite alikwenda South Africa baada ya mapambano yake ya madawa ya kulevya na alipiga picha na Daudi Kanyau mmoja wa ma don wa biashara hiyo ambae amehamia South.

Ile picha yake na Daudi Kanyau ilileta maswali mengi yasiyo na majibu.
Labda walikubaliana ushirikiano wa kuiptishia Dar. We unadhani kwanini watu wanajiuliza sana kuhusu mahusiano yake na rais?
 
Nitakupa jibu baada ya kuvaa jezi ya GSM kesho wakati wa mechi zamani tulikuwa tunavaa ya quality group ya MANJI.TUNA BOSS MPYA na jezi mpya ila hela ni zile zile.Hii biashara bwana.........wacha tuangalie mpira kwanza halafu KOFFI OLOMIDE na muziki wake baadaye
Hahaha! Boss mpya ila ela zile zile! Enzi zile Yanga wana Gulamali na Simba Dewji, enzi za kina Mohamed Mwameja Simba kila mchezaji na mpira wake huko safarini.
 
Kiasi fulani imepunguza maana zamani unga ulikuwa unauzwa hadharani ila Sahv unga unauzwa kwa kifichoooo.....

Hakuna kijiwee kilichokuwa nguli cha kuuza madawa ya kulevya kama pale kinondoni zamani duka la maimartha pale unga ulikuwa unauzwa hadharani, muuzaji anakuambia pale na kwenda kwa shift naingia saa 12 mpk saa 4,narudi tena saa 5 mpk 8,.......

Kiukweli hii biashara ni ngumu sana kuifuta kwa asilimia 100...hata ulaya na marekani upo, Indonesia Malaysia nchi zna sheria ngumu lkn unga upo..... Kinachofanyika ni kuwa punguza kasi tu wauzaji

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom