Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ni mpotoshaji. God will punish you.
techcabal.com
Kiufupi Elon Ndio katia timu na amesha launch satellites kibao kwa ajili ya hili ,hawa waseng£ wanaooona raia ni kama misukule wao wa kuwakamua.tu wajisikiavyo litaisha na wataisoma namba tu ,ni suala la muda
Huyu mmarekani anamean business ,na atatengeneza pesa kweli kweli ,si masikhara , suala la internet coverage Africa kinahitajika sana
Una akili ila jina sasa.Maskini wengi wanadhani Starlink inawahusu. Hata ikiletwa leo watakaomudu gharama za Starlink ni wachache mno. Starlink hawana bundles za buku. Unalipia kwa mwezi sio chini ya laki. Na pia lazima ununue vifaa vyao ni zaidi ya Tsh 2m. Starlink iliingia Zambia mapema ila hadi leo raia wengi hawaitumii internet yao. Kwa Tanzania ni bei tu ya bundles zishuke ndo suluhisho. Starlink sio suluhisho
Internet sio anasa kwa sasa ni lazima hata watumishi wa umma wanajaza majukumu yao kwenye mfumoThed weld dwellers bana FANYENI kazi nyie acheni kuendekeza na kupenda anasa. Internet ni anasa tu kwenu kuchat chat na madem na umbea mtandaoni.
Hii nchi unaweza kusafiri zaidi ya kilomita 500 ukakutana na maripori manene yasiondelezwa yapoyapo tu kizembe. Nendendo huko mkayasafishe mjishughulishe.
Jerry komaa hapo hapo kama Nape.
Panueni wigo mpana.
LETE MZUNGU! VIMBA!View attachment 3080053
View attachment 3080054
Ushahidi huo hapo, na link pia hiyo hapo.
![]()
Starlink introduces $15 kit rental plan to woo Kenya users
Kenyan customers interested in renting the Starlink kit, which costs $350 (KES 45,000), will pay a one-time activation fee of $21.techcabal.com
Kesho nataka niingie border hpo nitafute kifaa changu! Nipige biashara! Naweka mtaani hapa!Nataka niagize ivo vifaa apo kenya nifunge nyumban kwangu nina uhakik apa nilipo nitatumia bila shida na hakuna atakaeona akanichoma kwa wenyewe nchi😄
Acha kuwaponza watu wewe. Maeneo ya watu unaita mapori?Hii nchi unaweza kusafiri zaidi ya kilomita 500 ukakutana na maripori manene yasiondelezwa yapoyapo tu kizembe. Nendendo huko mkayasafishe mjishughulishe.
Ziendelee kalala kuna siku zitakuta kumekuchaAliyekuwa waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye aliwahi kusema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na taasisi za kimataifa, Tanzania inashika nafasi ya sita kwa Bara la Afrika kwa kuwa na gharama za chini za bando “vifurushi” huku ikishika nafasi ya 50 Duniani kwa gharama ya chini ya data.
Nape alitoa ufafanuzi huo wakati aliposhiriki kipindi cha Power Breakfast on Saturday cha Clouds TV na redio, Agosti 20, 2022 jijini Dar es Salaam ambapo alisema na kudai kuwa bei ya data kwa wastani wa 1GB ni Dola 1.71 sawa na shilingi 3990. Maneno ya Nape yalikuwa “Tanzania kuwa miongoni mwa Mataifa yenye gharama za chini za mawasiliano haimaanishi kuwa itapunguza malalamiko kwa kuwa uchumi wetu haufanani na wananchi wengi wana kipato cha chini”.
View attachment 3079455
Nape alidai kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kufanya tathmini ya gharama za uwekezaji, utunzaji na usafirishaji wa data kila baada ya miaka minne na tathmini nyingine inafanyika mwaka huu ili kupata uhalisia wa gharama za bando kama zitapanda au kushuka.
Aidha, Nape aliweka wazi kuwa Serikali imeruhusu ushindani kwa kuweka mazingira wezeshi ya kuwa na kampuni nyingi zinazotoa huduma za mawasiliano ambapo huduma ya vifurushi ni huduma ya ziada inayotolewa na makampuni hayo na kuleta unafuu wa gharama za mawasiliano.
View attachment 3079456
Kama ni mfuatiliaji wa mtandao na habari za ulimwengu basi ni wazi umepata kuona viongozi wa Safaricom Kenya wakikutana na kitu kizito sana kutoka kwa Elon Musk, dharau zao sasa zimekuwa majuto kwao kwa kile ambacho Starlink wamekuja kuwapatia nafuu ya gharama za mtandao ndani ya Kenya. Kwa taarifa za wazi kutoka mtandao wa X unadai kuwa mtu anaweza kufurahia mtandao kwa gaharama ya 40657.50 sawa na dola 15 za kimarekani.
Safaricom kwa sasa hawana ujanja tena kwa kile ambacho kinaendelea ndani ya Kenya, ni Safaricom ambao walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea na kiburi kikubwa, huduma mbovu kupita maelezo na kuzima mtandao kwa maagizo ya serikali. Starlink anakuja katika Wakati ambao wakenya wengi wamechoshwa kupita maelezo. Kwa sasa sijui utamwambia nini Mkenya aendelee kutumia huduma za mtandao kutoka Safaricom Wakati ameona kuna nafuu kubwa sana ya kutumia Starlink.
View attachment 3079457
Mageuzi haya yasiishie tu ndani ya Kenya bali Starlink fanya hima na Tanzania mje ili mitandao yetu hii ipate kujifunza na kukaa kwa adabu! Mara kadhaa gharama za bando zimekuwa zikipanda tu bila mpangilio wowote wa msingi huku TCRA akiwa kimya kama haoni kinachoendelea. Starlink akija Tanzania atatuonesha wapi panavuja na wapi kuna tatizo kabsa ndani ya hizi kampuni za mawasiliano.
Je unadhani Starlink akija Tanzania, utaendelea kununua bando la wiki kila siku au utahamia Starlink bila hata kuaga mtandao wako?
Hakuna poti lisilomilikiwa.Ukitska ujue mmiliki jidanganye kujipeleka kama hujafurushwa kama mvamizi.Mengi tu nenda huko Nyarugusu ushuhudie mwenyewe.
Ni kweli kabsa! Wanaona ni threat kwa pesa na uwekezaji waoStarlink kuja Tanzania ni ngumu sana kwa sababu viongozi wengi, wana HISA katika makampuni ya mawasiliano, short and clear.
Rais wetu auvunje mzizi wa fitina ili Watanzania tufaidike na revolution speed and super telecom services!
Aliyekuwa waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye aliwahi kusema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na taasisi za kimataifa, Tanzania inashika nafasi ya sita kwa Bara la Afrika kwa kuwa na gharama za chini za bando “vifurushi” huku ikishika nafasi ya 50 Duniani kwa gharama ya chini ya data.