Vita ya U-IGP yaweza kuwa imechangia kukamatwa viongozi wa CHADEMA?

Vita ya U-IGP yaweza kuwa imechangia kukamatwa viongozi wa CHADEMA?

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Barua iliyopostiwa mtandaoni juzi na admin wa Police Tanzania kwenye mtandao wa X inaonyesha kusainiwa na Kamoshna Awadhi Juma Haji tofauti na barua nyingine zinazotolewa na Msemaji rasmi wa Polisi David Misime.

Nini kimesababisha Mtu anayehisiwa kuyataka madaraka ya IGP atoe statement badala ya Msemaji rasmi? Je si kujipendekeza Kwa mheshimiwa Rais ili IGP aliyepo aonekane dhaifu?

Tunakumbuka wakati wa IGP Simon Sirro ilianza hivi hivi majungu na maafisa kujipendekeza Ikulu Hadi mmoja akatamka Wazi anautaka uIGP akanyang'anywa uRPC Kagera.

Ni wakati wa Mh Rais kupima kama hizi tetesi zina ukweli na kujiepusha hawa wanaomsababishia aonekane kiongozi katili wakati Wameficha agenda ya Siri nyuma ya pazia.

Je, tetesi hizi zilizozagaa mitandaoni zina ukweli au watu wameamua kuzua kama ulivyo ushabiki wa Simba na Yanga?

20240812_220745.jpg
20240812_220748.jpg
 
Jeshi siyo chama cha Siasa hufanyi chochote hadi alie juu yako aruhusu kama amesaini Awadh ujue anamamlaka hiyo huenda jambo hilo liko chini ya kamisheni anayoongoza yeye, siyo barua zote zinasainiwa na msemaji
Asante Mkuu, lakini Mimi nimeweka kama swali. Lini Taarifa nyingine ilitolewa na kamishna yeyote tofauti na Msemaji rasmi? Kwani matukio ya jinai mbona hayatokewi na kamishna wa jinai yanatolewa na Misime?
 
Mods nisaidieni kuweka alama ya kuuliza kwenye kichwa cha habari.
 
Hii barua ya Awadhi kwa vyovyote vile ilikuwa na baraka za IGP, lkn kuna amri toka juu ya kutengua katazo la polisi.

Pia ninadhani hata tamko la katibu mkuu wa ccm limeanzia kwenye vikao vya ndani. Nchimbi hajakurupuka tu na kunena aliyoyanena. Kwani yeye haogopi yaliyomkuta Kinana? Huyu bibi siyo mtu.

Bibi ameiona hatari kubwa mbele kisiasa kwa kuwakamata wafuasi na viongozi wa chadema, hivyo akatanabaisha kuwa waachiwe.

Ndiyo maana unaona chama kinajikanyaga na polisi wanajitafuna.
 
Asante Mkuu, lakini Mimi nimeweka kama swali. Lini Taarifa nyingine ilitolewa na kamishna yeyote tofauti na Msemaji rasmi? Kwani matukio ya jinai mbona hayatokewi na kamishna wa jinai yanatolewa na Misime?
Kwenye page za polisi barua kibao zimesainiwa na ma RPC pia kwahiyo siyo msemaji tu anaesain taarifa
 
Asante Mkuu, lakini Mimi nimeweka kama swali. Lini Taarifa nyingine ilitolewa na kamishna yeyote tofauti na Msemaji rasmi? Kwani matukio ya jinai mbona hayatokewi na kamishna wa jinai yanatolewa na Misime?
Awadhi si ni mzee wa oparwsheni na mafunzo na hayo ndio katika mambo yake huyo ama mimi sielewi
 
Back
Top Bottom