Vita ya Uchumi haijawahi kuwa nyepesi, Hayati Magufuli aheshimiwe

Sijahitaji msaada wako mie,ninachotaka ujenge hoja ili ueleweke hata kwa wale wanao amini jpm alipigana vita ya kiuchumi.
It seems your comprehension skills are still learning to crawl. Don't worry, though, everyone learns at their own pace! Keep at it, and one day you'll get there. For now, let's stick to the basics, shall we?
 
🗼💐📜🎁🆒
 
Mkuu vita kiuchumi ipi? Na nani? Wapi? Kwa jeshi gani? Silaha zipi? Nyerere alipigana vita na Iddi amin wa Uganda.
 
Awamu ya sita ya kishetani imeondoa sheria iliyokua inalinda rasilimali zetu kwa kufuta kifungu kinachotaka mashauri yote kusikilizwa mahakama za ndani.

Awamu hii ya sita ndio inaongoza kwa kugawa ardhi yetu kwa matapeli ya kimataifa yanayojifanya wawekezaji.

Baada ya awamu hii kuisha na aliyepo kuondoka na mambo yake tutabakia sisi kulipa hasara za ujinga waliofanya waliopo sasa.
 
Viongozi style ya JPM, huwa wanafanikiwa mwanzon ila mbele lazima wakwame tu
 
tumia akili na uwe unafuatilia mambo
 

Wakuu hoja zenu wote ziko sahihi ila anaeunga mkono hoja ya vita ya kiuchumi yuko sahihi zaidi changamoto inakuja anakosa namna sahihi ya kuwakilisha hoja yake na anakosa mifano halisi ya kujazia hoja.

Hii yote ni kwasababu katika vita za kiuchumi mataifa mengi huwa wanatumia Taasisi za siri za usalama, na kama mnavyojua Taasisi za usalama watu wao wanakuaga ni selection of talented elites (Akili nyingi)... Yaani wanapiga tukio ambalo kiratiba liko mbele ya muda arafu limesukwa kwaustadi mkubwa kiasi kwamba raia wa kawaida akikutana na tukio hilo kwanza anakua too late, pili anahisi tukio hilo ni lakimazingara(nguvu za giza zimehusika). Yaani liko beyond na upeo wake wa fikra.

Sasa watu kama hawa wakija kwenye suala la ujasusi wa kiuchumi wanatumia mifumo mingi tu lakini moja ya mfumo wanaocheza nao kwa weledi na ustadi wa hali ya juu ni mfumo ulio katika sector ya sheria,

Wanapitia vizuri kabisa katiba na sheria ya nchi ambayo wameitarget then wanaenda specific kwenye vifungu vinavyohusu resource wanayoitaka wao, lazima watakutana na mwanya tu (weakness) hata wakikosa hiyo weakness watafanya namna tu kupata mazingira favourable kwao.

Baada ya hapo wazee wa kazi wanaingia kazini... Unasukwa mkataba konki ulioshiba(mama mkanye mwanao). My friend hiiiii!!! Kama unavyoona engine za magari zilivyosuka kwa weledi na ustadi mkubwa hadi gari inatembea basi ndio hivyo hivyo mkataba inasukwa na inakuja imepakwa asali kama chambo tu, Sasa wewe jichanganye ingia kwenye mkataba kama huo utakuja kushtuka tayari umeshachelewa na kila ukitafuta namna ya kujitoa vifungu vinakubana.

Na hawa watu hawawezi kuacha clue yoyote ambayo wewe unaweza kuitumia kama evidence mahakamani.

Hiyo kitaalamu tunaita "ulipo lala leo wenzako wameamkia jana kama sio mwaka jana" yaani unakua kama panya alienasa kwenye ule mtego ambao kuingia rahisi ila kutoka Sasa ndio changamoto, mpaka aje mwenye mtego.

Sisemi kwamba kung'amua njama kama hizi kunahitaji rocket science lakini umakini unahitajika na wala hakuna haja yakuharakisha mambo, kuna msemo unasema "ukiona unaitwa kwenye fursa basi ujue fursa ni wewe mwenyewe"
 
Mazee huwezi kukaa na kulialia na kusingizia vitu ambavyo ni dhahiri, hiyo ndiyo hoja ya wengi. Yaani ni kwamba, ukipewa nchi kuongoza, unatakiwa kujua kuwa kuna foreign spies wanaokuja kwa malengo mbali mbali (ikiwemo vita ya uchumi ambayo sahihi zaidi inaitwa ushindani wa nchi kwa nchi). Hii ni changamoto ya nchi zote duniani na siyo Tanzania tu. Kwa hiyo kama rais, badala ya kulia lia na kusema kila kitu ni vita ya uchumi, unatakiwa uongoze nchi yako kwenye ustawi huku ukiunda mifumo yenye ku-minimize hayo mambo.
 
aione Erythrocyte
 
Ni sahihi kabisa hata hivyo JPM alionyesha nia na alikua anachukua hatua kupunguza hizo harakati nchini kwetu,

Na pengine kutamka waziwazi na hadharani kwa uzalendo mkubwa ni moja ya mbinu ya kimkakati (nawaza tu).
 
Ni sahihi kabisa hata hivyo JPM alionyesha nia na alikua anachukua hatua kupunguza hizo harakati nchini kwetu,

Na pengine kutamka waziwazi na hadharani kwa uzalendo mkubwa ni moja ya mbinu ya kimkakati (nawaza tu).
Sio vita. Ni ushindani wa kiuchumi. Unatakiwa kutumia akili, sio nguvu. Kwa mfano, magufuli angemwita lisu, ampe jukumu fulani labda kusaidia nchi ktk masuala fulani ya kisheria. Badala yake alituma wasiojulikana wakafanye yasiyojulikana.
 
Nyie watu vita vya kiuchumi mnavijua kweli au propaganda za yule jamaa yenu wa chato.

Hebu katazame U.S - China trade war ndio ujue vita vya kiuchumi vipoje sio huu upuuzi wenu wa jamaa yule wa chato.

Tazama sasa magharibi na Russia wanavyo pigana kiuchumi

Hivyo ndivyo vita vya kiuchumi sio vya jamaa wa chato vya maneno ya majukwaani.

Unaita vita vya kiuchumi hata kiwazo hata kimoja cha kumiza kichwa hujapigwa hivi ni vichekesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…