Wakuu hoja zenu wote ziko sahihi ila anaeunga mkono hoja ya vita ya kiuchumi yuko sahihi zaidi changamoto inakuja anakosa namna sahihi ya kuwakilisha hoja yake na anakosa mifano halisi ya kujazia hoja.
Hii yote ni kwasababu katika vita za kiuchumi mataifa mengi huwa wanatumia Taasisi za siri za usalama, na kama mnavyojua Taasisi za usalama watu wao wanakuaga ni selection of talented elites (Akili nyingi)... Yaani wanapiga tukio ambalo kiratiba liko mbele ya muda arafu limesukwa kwaustadi mkubwa kiasi kwamba raia wa kawaida akikutana na tukio hilo kwanza anakua too late, pili anahisi tukio hilo ni lakimazingara(nguvu za giza zimehusika). Yaani liko beyond na upeo wake wa fikra.
Sasa watu kama hawa wakija kwenye suala la ujasusi wa kiuchumi wanatumia mifumo mingi tu lakini moja ya mfumo wanaocheza nao kwa weledi na ustadi wa hali ya juu ni mfumo ulio katika sector ya sheria,
Wanapitia vizuri kabisa katiba na sheria ya nchi ambayo wameitarget then wanaenda specific kwenye vifungu vinavyohusu resource wanayoitaka wao, lazima watakutana na mwanya tu (weakness) hata wakikosa hiyo weakness watafanya namna tu kupata mazingira favourable kwao.
Baada ya hapo wazee wa kazi wanaingia kazini... Unasukwa mkataba konki ulioshiba(mama mkanye mwanao). My friend hiiiii!!! Kama unavyoona engine za magari zilivyosuka kwa weledi na ustadi mkubwa hadi gari inatembea basi ndio hivyo hivyo mkataba inasukwa na inakuja imepakwa asali kama chambo tu, Sasa wewe jichanganye ingia kwenye mkataba kama huo utakuja kushtuka tayari umeshachelewa na kila ukitafuta namna ya kujitoa vifungu vinakubana.
Na hawa watu hawawezi kuacha clue yoyote ambayo wewe unaweza kuitumia kama evidence mahakamani.
Hiyo kitaalamu tunaita "ulipo lala leo wenzako wameamkia jana kama sio mwaka jana" yaani unakua kama panya alienasa kwenye ule mtego ambao kuingia rahisi ila kutoka Sasa ndio changamoto, mpaka aje mwenye mtego.
Sisemi kwamba kung'amua njama kama hizi kunahitaji rocket science lakini umakini unahitajika na wala hakuna haja yakuharakisha mambo, kuna msemo unasema "ukiona unaitwa kwenye fursa basi ujue fursa ni wewe mwenyewe"