Nani aliwanyima hivyo unavyo andika hapa hivi unajua unacho ongea au unaropoka ?
Vita vya kiuchumi unavijua wewe au unaropoka tu kwa kelele za wanasiasa.
Nchi hamna mnacho zalisha cha kujitosheleza unasema tulikuwa na vita vya kiuchumi mkipigwa vita vya kiuchumi nyie na kisarafu chenu kisicho na thamani yoyote si mtaanza kula majani.
Hamna hoja. Nilidhani huwa wanakuja na silaha kupora. Kumbe ni tamaa za viongozi wetu ndiyo zinasababisha haya yote? Sasa unalia nini?
Wakuu mnafikiri kwanini tunashidwa kuzalisha vyakujitosheleza na ziada, Hapa tuzungumzie mazao ya kimkakati na industry zinazohitaji capital na mobilization kubwa achana na single individual ambao scale yao ya uzalishaji haina impact kwa taifa. eg. Sukari, ngano, mafuta ya kula, hata nishati.
Yaani kila awamu makosa ni yale yale.
Nakili ya kwamba sisi wa Africa tunachangamoto zetu lakini si kwa level hizi, pia mimi mwenyewe sipendi kuona mtu analalamika tu na kuwatupia watu lawama kwa mambo ambayo ni wajibu wake yeye kuyatekeleza, ni ujinga kama sio upumbavu.
Lakini mbali na hizo changamoto tulizonazo kama wa Afrika, wajanja wanaishi na sisi humo humo wanatumia udhaifu wetu kama fursa kupitia uishawishi wa kidiplomasia na nguvu ya kiuchumi walionayo ni rahisi sana kuhadaa viongozi wetu, na kumbuka yupo madarakani under pressure anahitaji support kuendelea kubaki.
Na ukikataa wenzako wanakula ukitafakari unagundua hakuna ulichofanya maana ulichopigania wezako wanakigawa maisha yanaendelea ila wewe unakua umejiweka kwenye angle mbaya, na wakikuamulia wanakuchafua kwa propaganda ile iwe fundisho kwa wazalendo waliobakia(discourage). Yaani unakufa maskini na skendo juu.👇👇👇
Mikataba wanaandaa wao, wanawaletea viongozi wenu wasome. Haiandaliwi na wanasheria wenu.
Kabla ya kuleta huo mkataba Kuna kua na Ile tunaita chachandu. Utasikia rais kaenda kule Leo kesho kutwa kaenda kule Tena. Hata mara kumi kabla ya huo mkataba kuandikwa. Wanampa na chake kabisa. Akikataa anakua sio mwenzao.
Kipindi hicho wanakua na watu wao wa kuwapa ABC. Watafatilia nani kasababisha ukatae na Kwa nini. Unajikuta upo katika risk kubwa.
Wasiowajasiri hukubali kuepusha shari Ili maisha yaendelee na familia zao zineemeke. Watu kama JPM hawakubali.
Kwenye vita ya uchumi hawapandikizwi viongozi tu, kila sector ambayo ni potential kunakua na agent wao hasa hasa hizi sector ambazo moja kwa moja zinashikilia uchumi wa nchi mfano. Nishati, wafanyabiashara wakubwa wa bidhaa muhimu ie, vyakula. Sasa hawa kuna michezo hua wanaicheza kwa kufuata maelekezo kuhakikisha nchi haiwi stable katika uzalishaji at the same time wanalinda soko la bidhaa zao kutoka nje ya nchi ambako ndio kwa wenyewe(mabeberu) Kwahiyo wao wanarisha raia wao wanapata ajira kupitia mnyororo wa thamani sisi tunatumia kwa gharama kubwa tunaishia kurumbana vijiweni.
Vita vya kiuchumi achia warusi, wachina, Iran, NK , Venezuela at least Zimbabwe akiongea Nita muelewa.
Mbinu mbalimbali hua zinatumia Kulingana na aina(nature) ya nchi na level ya maendeleo na ushawishi ilipofikia nchi husika.
Namna USA wanavyod-deal na mchina au mrusi ni tofauti watakavyo deal na sisi huku. Inaonekana sisi sio stubborn saana hivyo haina haja ya kutumia nguvu kubwa.
Nb vita ya kiuchumi kati ya USA na China hata sisi huku tunahusika kwa maana maslahi yao mapana yaliyopo kwetu huku yako rehani. Hii kasheshe sisi tukiwa bado tunapambania masrahi mapana ya nchi yetu. Kumbe wezetu wana masrahi yoa mapana juu ya nchi yetu (ukanda wetu).