Vita ya Uchumi haijawahi kuwa nyepesi, Hayati Magufuli aheshimiwe

Vita ya Uchumi haijawahi kuwa nyepesi, Hayati Magufuli aheshimiwe

Mama nae utasemaje ?
Mama ameiga kutoka kwa JPM chato imekuwa Kizimkazi. Na sukuma gang imekuwa wazanzibari huoni ? Ulikuwa hausomi post zangu huko juu nilikuwa naelezea kuwa JPM ndio chanzo cha ukabila na mpasuko serikalini. Pia Rais atakyefuatia baada ya Mama atafanya kama JPM.
 
Naomba uilinganishe Msoga na Chato kwanza. Kuhusu ukabila naomba uje na facts ya Rais ambae alijaza kabila lake katika baraza la mawaziri kumshinda JPM. Naomba tu uje na Baraza la mawaziri tu hapo sijagusa wakuu wa wilaya na mikoa. Turudi kwenye miradi chunguza kwa nini watu wanajenga reli ? kusafirisha watu au Mizigo ? Unaongea na Engineer ndugu yangu sio mwanasiasa kila miradi lazima ifanyike feasibility study. Hauwezi kujenga reli kwa ajili ya kusafirisha watu na hela ikarudi. Reli ya kwanza ilijengwa kwenda Zambia kwa ajili ya kuiongezea nguvu bandari. Hio SGR ya Mwanza haiwezi kurudisha hela ndio maana mradi huo hauwezi isha leo wala kesho ? Hauwezi kuweka tawi la banki kwenye wilaya ambayo mapato yake yapo chini sana ? Haya basi tuachane na hilo vipi kuhusu vile viwanja vya N.H.C ambavyo JPM alipitisha lami, maji na umeme? Walio nunua wamejenga ? Hizo ni hela zimetumika hapo. Eti treni ya umeme SGR mpaka Mwanza aisee ERB na CRB tulikuwa tunacheka sana kwenye vikao[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]. Yaani mtu unaanza Treni wakati mradi wa Bwawa la umeme haujaanza. Ukiwa haujasoma JPM utamwona mtu mwenye akili sana.



Kwahiyo kwa hoja hii na wewe unajisimamisha katika kundi la wasomi??!


Huoni aibu?!
 
Mama ameiga kutoka kwa JPM chato imekuwa Kizimkazi. Na sukuma gang imekuwa wazanzibari huoni ? Ulikuwa hausomi post zangu huko juu nilikuwa naelezea kuwa JPM ndio chanzo cha ukabila na mpasuko serikalini. Pia Rais atakyefuatia baada ya Mama atafanya kama JPM.
Sawa
 
Kwahiyo kwa hoja hii na wewe unajisimamisha katika kundi la wasomi??!


Huoni aibu?!
Nioneshe sehemu niliotumia kujigamba kuwa msomi. Wasomi wa nchi yetu wengi ni wa makaratasi. Hadi Prof alithubutu kukiita chuo kilichompa nafasi ya kusoma na kupata P.H.D jalálani. Akamuita Rais Mheshimiwa Mungu Tanzania tunazalisha wasomi kweli ? Je vyuo vyetu vimefanya tafiti ngapi hivi karibuni na kushirikiana na vyuo gani vinajvyojulikana kimataifa ? Naomba uje ulete facts unatumia hisia kulazimisha uongo kuwa ukweli. Rais unayemtetea angekaa chini na ajiulize anataka nini na anatakiwa afanye nini. Sasa mbadala yake alikurupuka kiasi cha kuipitisha Tanzania katika matukio ambayo Kenya, Uganda na Rwanda ilishapitia. Ukabila unaanza kimasihara unakuja kushtuka mambo yameshaharibika kabisa.
 
Akili ndogo una comply na mabeberu wanakomba Nchi watu wako wanaishi kimaskini ukiondoka tunasema ulikuwa mzalendo sana, boosheet
 
Tunachotaka ni maendeleo yenye tija.

Ni upuuzi na dharau kutuambia watanzania kua unaenda kutafuta wawekezaji huku nchin kwako hujaandaa facilities za uwekezaji. Huo ni ushamba. Hii hupelekea waje wawekezaji ambao ni matapeli wapige dili tu. hamna kingine. Real investors wanaangalia mazingira ya uwekezaji kama umeme wa uhakika, sera za kibiashara zisizobadilikabadilika zenye tija kwa wote.

Ni upuuzi na dharau kutuambia sababu za kwa nin miradi ya ki mkakati haiendele mara sijii crane ya kuinua gate haipo hadi iagizwe ulaya, mara maji hayatoshi kwenue bwawa ( kipindi hiki ni masika ) mara maji yamebadili mkondo ndio maana mgao wa umeme na blablabla

Tunataka maendeleo yenye tija kwa wote na sio maendeleo kwa wapiga dili tu.

Sukari imekuja lakin bei bado haishuki.

Dola haipo mara sababu ya korona mara vita ya ukrain na sasa kule midle east. Yaan duuhh.
 
Habari JF, vita ya Uchumi kuanzia mitaani, mirathi na makazini hata iwe ndogo haijawahi kuwa nyepesi na haijawahi acha mtu salama.

Ukiwa kiongozi wa juu nchi za Africa huwa hakuna vita nyepesi ya uchumi sababu unakuwa unapigana watu wa ndani ya nchi lakini pia na mataifa ya nje.

Magufuli pamoja na mapungufu yake yote alieonyesha jitihada katika kupambana hii vita ndani ya nchi lakini pia nje ya kwa kupitia mikataba mibovu mbali mbali na kuivunja ingawa wimbi la kesi za kushindwa kimataifa limeongezeka. Kwanini hizi kesi ni kipindi hiki? Kuna watu wana nufaika na hizi kesi?

Ukimsikiliza hapa mwalimu Nyerere kuna kitu unaweza elewa.

View attachment 2900394

Lakini JPM mwenyewe mara kadhaa kaongea kwa uchungu sana.
View attachment 2900408

Kwa kifupi kabla hatujalaumu kwa yote tuliyopitia Awamu ya Tano au Tunayopitia awamu Hii cha kwanza jiulize unaweza vaa hivyo viatu na ukapigana na Mafisadi na Mabeberu?

Binafsi huwa namlaumu Magufuli kwa kitu kimoja tu, kutotuletea Katiba Mpya.

Tumuache mzee wetu apumzike kwa Amani.​
Uko sahihi sana
 
Hiyo dhana ya ''vita ya uchumi'' ni moja ya vitu ambavyo Magufuli alifanikiwa kuwaaminisha wafuasi wake na mpaka kesho bado wataendelea kumsujudia. Ni kama vijijini, watu maskini wanavyoaminishwa na waganga au wenyewe kwa wenyewe kuwa umaskini wao unatokana na husda, vijicho na ulozi wanavyofanyiwa na maadui zao. Unakuta mtu ana nyumba ya nyasi na watoto 15, fedha yake yote inaishia kwa waganga kwa kuamini kuwa magonjwa, umaskini na kila aina ya masahibu yake yanatokana na kijicho cha maadui.
Soma kuhusu economic hit man ndani ya nchi utaelewa
 
sababu wanazotoa sasa;
utasikia CORONA ndio chanzo cha haya yote, Vita ya Russina vs Ukraine ndiyo sababishi ya haya, Mvua imekuwa nyingi sukari ikaadimika, na umeme tunashindwa kuzalisha nduzo zinadondoka na nyaya kukatika, Mara ooh sisi sio kisiwa Nchi zilizoendelea wanafanya haya...ghafla oooh huwezi kuiga nchi zilizoendelea maana wale wapo mbele sana kimaendeleo na kiteknolojia.. Yaani nchi yetu hata Mungu atusamehe vipi bado uongozi tunaouweka ni TATIZO la kila jambo yaani
Umeniudhi na hiyo sentensi ya mwisho ungejua ungerekebisha mapema hiyo sentensi.
 
Back
Top Bottom