Vita ya UKRAINE ukilinganisha na IRAQ inaonyesha Ukatili wa US/NATO na upendo wa Urusi

Vita ya UKRAINE ukilinganisha na IRAQ inaonyesha Ukatili wa US/NATO na upendo wa Urusi

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Kipigo cha Iraq wakuu kilikuwa ni cha kikatili sana.

Ziliruka ndege mamia juu ya Anga Siku ya kwanza zikadondosha mabomu kama mvua Baghdad. Hata sisimizi wa Iraq walijua kuna wanadamu katili.

Uchunguzi wa UN ulipuuzwa. Anapigwa MTU bila kuonyesha uhalali wa upigwa. Na dunia nzima ilishangilia.

Hakukuwa na MTU anayetoa taarifa za kinachoendelea isipokuwa mpigaji tu.

URUSI.
Amepigana kiupendo sana.
Anagawa vyakula.
Mashambulizi yake ni ya kudonoadonoa tangu mwanzo.

Licha ya Kuwa nchi yeye ndege nyingi duniani za kivita ukiacha US lakini hajampiga vzr kwa kishindo maana anaupendo.

Wakuu tusiwadharau warusi wangefanya tunavyotaka wafanye tena kwa kushtukiza vita hivi vingeisha kwa Siku NNE tu.

Naomba kutumia fursa hii kumpongeza Putin. Hao wazungu wangemuacha Putin ampe adamu Ukraine kwa sayansi na sanaa aliyoipaga Wenda wote tungependa vita. Maana angepigwa vizuri na damage kidogo tu.

Hawa wanaopenyeza silaha na wajeshi kuharibu equilibrium ya vita wa nataka Putin aonekane ni Katili kama wao.

Putin ni MTU Mwema sana.
Tumuombee maisha marefu
 
Kipigo cha Iraq wakuu kilikuwa ni cha kikatili sana.

Ziliruka ndege mamia juu ya Anga Siku ya kwanza zikadondosha mabomu kama mvua Baghdad. Hata sisimizi wa Iraq walijua kuna wanadamu katili...
Punguza uongo kijana. Japo napenda kuandika kwa kina ili kumuelimisha mtu lakini wewe sitafanya hivyo Bali nitakujibu kwa kifupi Sana.

Marekani haikuingiza ndege Nchini Iraq kuanzia siku ya Kwanza mpaka ya nne.

Siku ya 1 : Marekani alirusha Makombora ya Tomahawk Missiles kutoka kwenye Destroyers Zilizokuwa Maditeranian Sea. Siku hiyo ya Kwanza,Marekani alirusha Makombora zaidi ya 1500 ndani ya Iraq ili kuharimu Mifumo ya Ulinzi wa Anga wa Iraq (Air Defence Systems)

Siku ya Pili : Marekani ilirusha Makombora ya Standard Missiles-6(SM6) ili kuharibu Underground Millitary Storage Facilities. Zaidi ya Makombora 120 ya SM6 yalipigwa Nchini Iraq.

Siku ya 3 : Marekani aliingiza Ndege za Kivita 40 Aina ya F-18A Falcon,Zilirudi 29 TU Kwenye Kambi ya Jeshi la Marekani iliyoko Kuwait,Zingine 11 zilitunguliwa na Mifumo ya Ulinzi wa Anga wa Iraq. Hapo ndipo Marekani ikaamini kumbe Bado Iraq ina Mifumo ya Ulinzi wa Anga ambayo Bado inafanya kazi Licha ya Mashambulizi Makali ya Manowari za Marekani. Wazo lililokuwa ni Kuli-SATURATE Anga la Iraq kwa Mizinga ya Masafa Marefu.

Siku ya 4 : Marekani alituma ndege za Kivita 120 Aina ya B-52,F-15,B-1B na Ndege nne za B-2. Baada ya Anga la Iraq kuzidiwa ndipo Saddam Hussein akaviamuru vikosi vyake Virushe SCUD MISSILES Nchini Israel. Lengo la Kufanya hivyo ni Kuilazimisha Israel iingie Vitani dhidi ya Iraq.

Kipindi hicho mwaka 2003 Israel ilikuwa na uaduwi na nchi Nyingi za Kiarabu,hivyo Endapo Israel ingeliingia Vitani,Basi Nchi za Kiarabu zingeliingia Kumsaidia Saddam Hussein na Hilo ndilo lilikuwa Lengo la Saddam Hussein kuishambulia Israel. Intelligence ya Marekani ililijua Hilo,hivyo ili kuzuia Vita kuwa kuwa Mashariki ya Kati,Basi Marekani ilipeleka Washauri wa kijeshi 300 na Mifumo 6 ya PAC-3 Nchini Israel ili kuzuia Israel isijibu mashambulizi Bali Ijikinge TU dhidi ya Makombora ya Iraq.
 
Punguza uongo kijana. Japo napenda kuandika kwa kina ili kumuelimisha mtu lakini wewe sitafanya hivyo Bali nitakujibu kwa kifupi Sana.

Marekani haikuingiza ndege Nchini Iraq kuanzia siku ya Kwanza mpaka ya nne...
Kulikua na ndege si chini ya 500 zilizoingia Iraq kuisambaratisha Iraq na kuifanya magofu ya kushangaza
 
Punguza uongo kijana. Japo napenda kuandika kwa kina ili kumuelimisha mtu lakini wewe sitafanya hivyo Bali nitakujibu kwa kifupi Sana.

Marekani haikuingiza ndege Nchini Iraq kuanzia siku ya Kwanza mpaka ya nne...
hii fix kuliingia mamia ya ndege tena zilipiga tu bila kuangalia wanapopiga wale WAUAJI

PUT IN kapigana VITA kama yupo HARUSINI jamaa kapigana kiungwana mnoooo
 
US na NATO wanavyombo vya habari vyenye nguvu duniani, hivyo wanaweza kuitangazia dunia kuwa 6 ni 9 na dunia ikakubali na ikaimba nao pamoja.....Ila Rusia yupo kupunguza kama sio kukomesha huo upotoshaji
 
Hivi ni Kwa nini silaha zote za Wahalifu na magaidi Duniani ni AK 47?

Kuna nchi mpaka watoto na Wanawake wamiliki Bunduki aina ya AK 47.

Inaelekea Kuna nchi inaziuza hizo silaha Kwa Wahalifu kama karanga .

Hizi ngozi nyeupe sio rafiki Kwa kiumbe yeyote hata siku Moja mbele ya maslahi yao.

Lakini hata hivyo Marekani ni nchi ya Pili au ya tatu Duniani yenye Waafrika wengi baada ya Nigeria. Kwa hiyo Wamarekani ni ndugu zetu. Tutasimama nao zaidi mana ndugu zetu waafrika wapo wengi kule.

Sio Uarabuni Wala Israel Wala China Wala India Wala Urusi ambapo wanaishi waafrika wanaofikia hata Mili Tano. Ni wabaguzi na hawana habari kabisa kama mtu mweusi naye ni binadamu anayefaa kupata hata ajira kwenye majeshi yao.

Urusi tunaishabikia TU kama simba mana hakuna namna Kwa sababu upende usipende urusi ni baba lao na anagawa mkongoto mpaka Kwa ndugu zake wa Ukrein. Wanauana wenyewe Kwa wenyewe.

Achana nao hawana msaada wowote zaidi ya kutuuzia silaha za kuuana na kukandamizana TU mana anajua waafrika na waarabu ni wapumbavu wanaopenda ngono TU kuliko maisha yao.
 
Punguza uongo kijana. Japo napenda kuandika kwa kina ili kumuelimisha mtu lakini wewe sitafanya hivyo Bali nitakujibu kwa kifupi Sana.

Marekani haikuingiza ndege Nchini Iraq kuanzia siku ya Kwanza mpaka ya nne...

Weka source official ya haya maelezo.

Maana Mimi source ni mwenyewe nilikuwa nafuatilia kwa radio na TV kuanzia mwanzo nikaacha pale mamia ya magari ya kivita yalipomalizia Kazi baada ya ndege kusafisha njia.

Niliona scene Moja madege yakidondosha mabomu mengi tena yakiwa juu sana.

Lakini tunakubaliana kabla ya vita vya ardhini Iraq ilikiwa imeogeshwa bomu za kutosha.

Hiki kitu kingefanyika Ukraine Kazi ingeisha Siku NNE tu.

Putin Muungwana sana.
 
Hivi ni Kwa nini silaha zote za Wahalifu na magaidi Duniani ni AK 47 ?
Kuna nchi mpaka watoto na Wanawake wamiliki Bunduki aina ya AK 47.
Inaelekea Kuna nchi inaziuza hizo silaha Kwa Wahalifu kama karanga ....
Sina upande Mkuu. Na kushabikia ugomvi wa Urusi na Ukraine ni kama kushabikia ugomvi wa Mke na Mme sababu wanajua wao sisi wengi hatujui.

Hata zikisemwa hazina mashiko ya kuhalalisha hicho kinachoendelea
 
US na NATO wanavyombo vya habari vyenye nguvu duniani, hivyo wanaweza kuitangazia dunia kuwa 6 ni 9 na dunia ikakubali na ikaimba nao pamoja.....Ila Rusia yupo kupunguza kama sio kukomesha huo upotoshaji
Media za magharibi hasa zile maarufu tunazozifahamu ziko more independent katika kukusanya, kuripoti na kuchambua taarifa. Wakati mwingine hata makosa yanayofanywa na serikali za mataifa husika utayakuta yakiripotiwa ama kujadiliwa na hizohizo media za ndani.

Sasa, nenda upande wa pili! Gazeti dogo tu likiripoti jambo lolote baya la serikali ama kukosoa mwenendo wa kiutawala na sera za serikali husika, kesho yake hulioni mtaani. Wewe ungependa dunia itegemee habari za kutoka TASS ama RT?
 
Urusi anajua vzr Ukraine kuliko US alivyoijua Iraq ya Sadam. Angesema Putin atumie approach ile dunia nzima ingeandamana kumkamata Putin anyongwe.

Na Approach hii US wangeitumia Iraq hadi Leo Saddam angekuwa hai au angekufa kifo cha asili kama Mullar mtalibani.

Maana vita vingehamia mitaani informal ambavyo US wangeshindwa kujua tofauti ya nesi, mkulima, house girl , mwanajeshi etc.

Mfano hadi kwenye chekechea Ukraine zinakutwa silaha za kutungulia ndege. Mama mmoja wa nyumbani tu anajisifu kadungua ndege tatu za Urusi kwa zile misaada ya Uingereza. Wananchi na wanajeshi haijulikani nani ni nani.

Somalia case study (Black Hawk down), US walikimbia maana ilikuwa ni kama Ukraine wanachi na wanajeshi haijulikani nani ni nani.

Hii Urban War ni ngumu labda uamue kufyeka pori ili uue nyoka mmoja.
 
Media za magharibi hasa zile maarufu tunazozifahamu ziko more independent katika kukusanya, kuripoti na kuchambua taarifa. Wakati mwingine hata makosa yanayofanywa na serikali za mataifa husika utayakuta yakiripotiwa ama kujadiliwa na hizohizo media za ndani...
RT ni tbc ya ulaya
 
Urusi anajua vzr Ukraine kuliko US alivyoijua Iraq ya Sadam. Angesema Putin atumie approach ile dunia nzima ingeandamana kumkamata Putin anyongwe...
hahahaa mama kadungua ndege?
 
Mkuu hii ni jamii forum. Hatufanyi UE hadi tupinde mgongo kuandika kwa madaha ili kukufurahisha proUSA
Kwamba, kuna kipigo cha kikatili, pia kuna kipigo cha upendo! Au sio?!

Mashambulizi ya "kudonoadonoa" ndiyo yakoje hayo? Huo upendo unathibitikaje? Kwa kugawa chakula? Yaani, mtu akikushambulia kwa makusudi, kisha akatoa chakula, ni uthibitisho kuwa anakupenda? How?

Unasema, wakati wa vita ya Iraq, UN ilipuuzwa maana vita haikuwa halali. Sahihi! Wakati wa vita hii ya sasa je? UN ilisapoti?

Vita ya Iraq haukuripotiwa na yeyote zaidi ya Marekani/NATO? Seriously?!

Umemalizia kwa kumsifia Putin, umempongeza n.k. Wakati huohuo unasema kwamba hauna upande katika mgogoro uliopo!

Mimi nimeusoma uzi between the lines bila kubadilisha maneno wala kupunguza ama kuongeza chochote.
 
Hivi ni Kwa nini silaha zote za Wahalifu na magaidi Duniani ni AK 47 ?
Kuna nchi mpaka watoto na Wanawake wamiliki Bunduki aina ya AK 47.
Inaelekea Kuna nchi inaziuza hizo silaha Kwa Wahalifu kama karanga .

Hizi ngozi nyeupe sio rafiki Kwa kiumbe yeyote hata siku Moja mbele ya maslahi yao.

Lakini hata hivyo Marekani ni nchi ya Pili au ya tatu Duniani yenye Waafrika wengi baada ya Nigeria. Kwa hiyo Wamarekani ni ndugu zetu. Tutasimama nao zaidi mana ndugu zetu waafrika wapo wengi kule.
Sio Uarabuni Wala Israel Wala China Wala India Wala Urusi ambapo wanaishi waafrika wanaofikia hata Mili Tano. Ni wabaguzi na hawana habari kabisa kama mtu mweusi naye ni binadamu anayefaa kupata hata ajira kwenye majeshi yao.

Urusi tunaishabikia TU kama simba mana hakuna namna Kwa sababu upende usipende urusi ni baba lao na anagawa mkongoto mpaka Kwa ndugu zake wa Ukrein. Wanauana wenyewe Kwa wenyewe.
Achana nao hawana msaada wowote zaidi ya kutuuzia silaha za kuuana na kukandamizana TU mana anajua waafrika na waarabu ni wapumbavu wanaopenda ngono TU kuliko maisha yao.
Ak 47 ni silaha bora ndio maana kila mtu anataka kuwa nayo
 
Back
Top Bottom