Marekani na washirika wake ndio wanatumia nchi nyingi kuzinunua na kuwapa wanaopigana dhidi ya Russia
Nakumbuka vita ya Afghan/Russia ya 1979- 1989 America walizitumia nchi kadhaa kununua silaha toka kwa Mrusi halafu zinapita Pakistan mpaka Afghanistan
Mrusi alikuwa akishangaa kila anapouwa Waafghan au kuwashika mateka anawakuta wana AK
Yote hiyo wazungu walikuwa wanaogopa kujulikana wanamsaidia Afghan kwa silaha
Ila sasa unaona dhahir wanampa silaha Ukraine
Mambo yamebadilika sana
Ila vita ya so called dunia vs Iraq walimuonea sana kwani nilikuwepo huko jamaa ni mbwa hao wasiokuwa na chembe ya huruma
Ila nilipoa ile invasion ya Somalia 1993 nilifurahi sana watoto wa baba walichokifanya kwa majeshi yanayojitamba duniani kuwa ni the best
Ila kile walichokipata kiliwapoza wengi
Kwa hiyo Urus inauza silaha Kwa njia HARAMU.
Mana tulitegemea iziuze kwenye majeshi halali na sio Kwa njia HARAMU .
Hata kama Marekani imewapa pesa.
Lazima tujiulize Marekani utoe pesa halafu pesa hizo zikanufsishe viwanda vya Urusi vya silaha na kuongeza pata la Urus.
Ukweli ni kwamba Urusi imewekeza sana kwenye silaha na ndiyo biashara yao kuu Dunia nzima.
Ndio maana Urusi Haina haja na Dunia yenye Demokrasia mana penye Demokrasia ya kweli hakuwezi kuwa na vita Wala uasi.
Mfano Kenya. Leo hii Kenya ingekua Bado inatawaliwa na Ule udikteta wa Moi wa kuwaua watu wote wenye ushawishi wa kisiasa na kusema kila mtu lazima afuate Nyayo ,Kenya ingeingia kwenye civil war na silaha za mitaani zingetoka Urusi. Jeshi la Kenya wanatumia silaha Toka nchi za magharibi.
Kwa Taarifa yako hata silaha za Kongo zinaingizwa kinyemela na zunafadhiliwa na nchi jirani kuingia kama silaha halali kwenye nchi hizo lakini zinanunuliwa na Waasi Kwa manufaa ya nchi jirani na sio Marekani Wala Nini .
Marekani hawezi kutoa pesa za Kununua silaha Toka Urusi wakati uchumi wa Urusi unategemea silaha hizo.
Yaani Marekani atoe pesa wanunue silaha Urusi halafu Marekani huyo huyu atoe pesa nyingi kuisapoti UN kwenda kuwanyanya silaha hao aliowapa silaha kama Sudani na Kongo na Somalia ilivyo Sasa na miaka karibu 20.
Hebu fikiri vikosi vya Tanzania ,Rwanda,Nigeria,Kenya, Ghana nk. vilivyopo Sudani na Kongo wanavyolipwa mabilioni ya Dola Kwa ufadhili wa Marekani ili kuwanyanganya silaha Waasi , na silaha zote ni AK na nyinginezo Toka Urusi halafu hao hao watoe tena Pesa wakanunue silaha Urusi.
Waafrika tunatstizo la kulishwa vitu kichwani badala ya kufikiria wenyewe na kukataa kudanganywa.
Tulitegemea Kongo na Somalia pawe na silaha nyingi za nchi za magharibi ili tuamini kuwa wanatuchonganisha ili watuuzie silaha lakini sio hivyo badala yake silaha ni Toka China na Urusi na wanaofadhili pambano ni nchi jirani.
Nani alimsaidia Kagame kuanzisha vita vya uasi?
Silaha zilipita wapi?
Zilitokea wapi?
Alikua anajificha wapi ?
Je,nani alimsaidia Museveni kufanya uasi?
Nani alimsaidia Kabila?
Lazima tujiulize maswali hayo.
Nchi za magharibi Zina matajiri wengi sana wanaohitaji kuzunguka Duniani na kuwekeza au kutalii na kula Bata. Hawahitaji Dunia yenye vita na machafuko. Ndio maana wanataka Demokrasia ili hata Mwafrika akiwa na uwezo akakae kokote bila kuvunja Sheria.
Mzungu anatamani kuishi popote alimradi pawe na amani na uhuru.
Ndio maana Afrika kusini hutasikia wazungu wakipita mitaani wakipora Mali za watu lakini waafrika wanapora Mali za Waafrika wenzao. Wazungu hawawabagui Wageni lakini waafrika wanawabagua waafrika wenzao. Wanafikiri Afrika kusini ni Mali yao wakati wanashindwa kujiletea maendeleo hata baada ya uhuru. Walipata Uhuru viongozi wao wakawa wanaojimilikisha Mali TU ili nao waishi kama wazungu badala ya kuwainua waafrika kiuchumi ili watoke nje kutafuta fursa wanaodanganyana kuwa wazungu ndio wanawaibia hata pale ambapo makimosa ni yao waafrika hawakubali ili wajirekebishe.
Afrika na Asia Bado wanatumia utawala kama sehemu ya kutajirika Kwa haraka,ndio maana anagombania madaraka na kuuana. Wenzetu wa magharibi walishatoka Huko. Hata china ya Sasa haitaki vita ya kutumia nguvu.
Nchi Moja ya Kiafrika au Kiarabu kama kweli ina watu wanaokubali kutumiwa na nchi za magharibi za wazungu ili kuua waarabu wenzao au waafrika wenzao wenye Lugha Moja na jamii na Mila Moja basi hizo nchi Zina watu wapumbavu na malofa acha wauane waishe mana hawafai kukaa kwenye Dunia hii.
Yani aje Mzungu aniambie nimuue Mwafrika mwenzangu. ? Shenzi kabisa.
Mwafrika anaambiwa na Mwafrika Mwenzake na anaahidiwa madaraka na Mwafrika Mwenzake kumuua Mwenzake.
Tuliona uchaguzi wa 2020 watanzania walikua wanawakata mapanga watanzania wenzao. Walikua wanawakaba na kupora fomu za uchaguzi, walikua wanabadili matokeo na kutumia Polisi na Jeshi lenye askari watanzania dhidi ya Watanzania wenzao Kwa sababu ya ulafi wa madaraka. Sikuona Mzungu akiamuru wakurugenzi wavuruge uchaguzi na Polisi wapige na kujeruhi watu. Sasa ingetokea vita Tungeihusisha Vipi Marekani ?
Huoni kuwa watawala na Waasi wanazirushia mzigo nchi za magharibi ili kuhalalusha uovu wao na kukwepa kutupiwa lawama.?