Vita ya Ukraine - Urusi ina hadhi ya kuziangusha serikali za Ulaya na Marekani

EU inamwona Putin kama adui zaidi kuliko China.
Inajua inahitaji umoja wao ili kubaki kuwa na sauti duniani.
Wanachama wa EU ni waumini wa demokrasia kitu ambacho Putin amekipa kisogo.
Wazungu wanajua athari za utawala wa kiimra kama wa Putin ,,,
hii vita isingetokea kama Urusi wangekuwa waumini wa democracy.
Warusi walio wengi hawapendi vita anayoiendesha Putin kwasasa.

Naweza sema hili ni game ambalo limetokea katika wakati mzuri kwa wamarekani kwani wanae Biden ,,, ni matokeo ya upuuzi wa Trump kukosa jicho la karibu kuichunga Urusi na washirika wake akiwemo China.
 
Leta chanzo wanashambulia ndani ya Russia
 
Hebu tuwekee na CV yako hapa ili tujue tunajadili na mtu wa aina gani!
 
Acha Uwongo,,Chancellor wa Ujerumani alitangaza muda kwamba Hatogombea tena...Russia nu muda tu utasema. USA NA ULAYA Magharibi haijawahi kushindwa,,unajua sababu ni nini?? Vijana kutoka nchi zinazofuata siasa za mkono.wa chuma kama Russia, China,Ulaya mashariki,na hata Uarabuni,,wanapenda mtindo na siasa za Kimagharibi...Putin atatoka kama alivyokwenda Mikhail Gorberchiv...Mtindo na siasa za Kimagharibi zinzavutia Vijana weengi kutoka nchi za Kikomunisti na Ki shoshalist.
 
Biden na Scholz hawatapata awamu zao za 2 kila mmoja. Hilo liko wazi.
Boris anaweza kutokana na asili ya siasa za Uingereza. Zimekaa sana kivyama kama huku Stanza.
 
Wazungu hawampendi mtu. Wale ni monsters wa rasilimali. Pale Ukraine kuna natural gas, kuna coal, kuna chuma, kuna mafuta, wazungu wanataka hizo rasilimali.
Pia ni eneo muhimu kiusalama ili kumthibiti Urusia.
Ingewezekana Ukraine ingefanywa pori tupu lisilokuwa na watu ili kuwa kama DMZ(Dimilitarized zone kati ya Urussi na Marekani akiwa na vibaraka wake wa Ulaya Magharibi.
 
Kaka hii ndio ujue kwamba misaada tunayopewa ndio ndoano ya kuvulia rasilimali zetu. Tusifurahie kupewa misaada na mikopo na wazungu. Mikopo na misaada Yao ni ghali sana. Ogopa sana mtu aliyekupa pesa aliyokopa.
Taratibu watu wataanza kujifunza na kuwa na ufahamu mzuri juu ya haya mambo.

Nchi zetu zinapojiuza kama malaya kwa hawa watu, na kusahau kwamba wajibu ni wetu kujiletea maendeleo, pengine hata hao wanaotuuza nao wataanza kuingiwa na akili kichwani.
 
Ukisikiliza vyombo vya western na wapambe wao humu JF ni kama Russia kapigwa vibaya sana na tayari ameshindwa vita.
 
Hata yule katuni anaetumiwa na mabeberu wa ulaya na America yupo usingizi wa pono mara akizinduka nchi yake yote ilishaliwa himaya ya mrusi🤸
 
Mtanzania akujua tu kusoma, kuandika na kuhesabu, anajiona amekuwa nabii, na mtambuzi wa kila kitu.

Mtu anabwabwaja toka mwanzo mpaka mwisho, bila ya ushahidi wowote!!
 
Tena Russia wamesema wanasubiri kura ya maoni ya lile jimbo la Mashariki (wakikubali kujitenga na Ukraine, watakuwa wamefanikiwa lengo lao, wataacha kupigana), lakini ukweli Urusi mambo yapo shingoni, anatafuta mlango wa kutokea bila aibu.

Ni vigumu sana Russia yenye uchumi dhaifu kiulinganifu, kuwashinda wenzake wengi wenye uchumi mzuri, walioungana.

Ndege za Urusi zilizotunguliwa, zimeonekana kutumia GPS za kawaida za kusafiria kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha kuhudumia ndege zake za kivita. Kwa sasa ndege zake kila zikiruka zinadunguliwa. Wamebakia tu kurusha makombora, lakini siyo kuruka angani kama mwanzo.
 
Wewe hata huna ukijuacho kwenye hili. Huu ni
Huu ni mwendelezo wa vita baridi kati ya Marekani na Soviet. Urusi ni kikwazo kikuu kwa Marekani kufanya inavyotaka kwa mataifa mengine. Urusi ni kikwazo kwa nchi za kibeberu. Kumbuka kuwa Urusi ni chanzo Cha Marekani kushindwa vita zake kama kule Syria, Vietnam, somalia, Afghanistan. Ukomnozi wa Afrika dhidi ya western countries uliitegemea Urusi. Mataifa kama N.Korea, uchina, Venezuela na Iran vinategemea Urusi. Urusi ni mwiba mkali kwa western countries.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…