Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Bosi wa Wagner Prigozin sasa ametangaza rasmi kuikalia Bakhmut. Hata mkuu wa NATO naye japo hajasema kwa wazi naye amekubali kazi ya Bakhmut imeisha kwani yeye ametabiri kuanguka kwa Bakhmut baada ya siku tatu.
Sijui kama alichosema raisi Zelensky kama ni kweli dhidi ya uvumi kwamba ana msuguano mkubwa na makamanda wake waliotaka kuuachia mji huo mapema zaidi ili madhara kwa upande wao yasiongezeke.
Pamoja na hayo ni kweli Urusi imepata hasara kubwa na kuonesha ushujaa mkubwa katika vita kinyume na matangazo ya Uiengereza.
Imetajwa kwamba eneo la Vulhedar ilikuwa ni lazima warusi wapite ili kuingiza askari wake wa miguu katikati ya mji. Eneo lote likiwa limetegeshwa mabomu ya kuripua mizinga na huku wanajeshi wa Ukraine wakiwa wamejifcha maeneo ya vilima wakivizia vifaru hivyo kwa msaada wa upelelezi wa droni.
Walichofanya Urusi ni kuvurumisha vifaru vyake usawa huo huo hata kikiripuliwa kingine kinafuata njia hiyo hiyo kama kwamba cha mbele yake ndio kimesafisha njia.
Wanachosema Ukraine jumla ya vifaru 130 vya Urujsi siku hiyo viliripuliwa lakini hatimae vya nyuma vilifika mjini. Angalia vidio hapo chini Hao askari wa miguu nao waliofika huko walijipanga vikosi vidogo 20 ishirini.
Waukraine wanadai wakifika 20 wanawauwa lakini baada dakika 20 wanakuja wengine ishirini mpaka wakajichokea na kumaliza silaha zao. Kwa hakika hii ya Urusi ni dalili ya ushujaa wa hali ya juu katika vita na sidhani kama America ina askari kama hao.
Alichotabiri Zelenksy kuhusu Bakmut na kwamba wanasubiri vifaru vya NATO vifike wiki ijayo itakuwa ni dalili kuvujisha siri za vita na vilivyoipa mbinu Urusi kumalizia kazi yake mjini humo.