Vita ya vifaru kule Vulhedar/Bakhmut ishara ya ushujaa wa Urusi

Vita ya vifaru kule Vulhedar/Bakhmut ishara ya ushujaa wa Urusi

Kwa upande wangu tukiacha ushabiki pembeni, naona kama mwisho wa vita Kati ya Russia na Ukraine inakwenda kuishia pabaya zaidi.
Ukraine bado hajarusha silahaa ndani ya Russia kwasababu bado anajilinda...sababu anajua yeye.

Russia bado anatumia Askari wa kukodi kwa wingi pamoja na wafungwa akijua kuwa vita bado mbichi sana...sijui siku akiwaingiza askari wake kamili.

Nchi zinazomuunga Ukraine bado wanapeleka msaada interns of Money na Silaa siku...je siku wakiamua kuingiza askari wao pamoja na silahaa zao?

Nchi zinazomuunga Russia bado wanatoa msaada wa silahaa...je siku wakiamua kuingiza msaada wa askari na wataalam wao?

Sioni vita hii ikiacha Dunia sehemu salama pa kuishi tena.
Mmoja ataumia sana either Russia au Ukraine ndo vita itaisha, kwasasa Ukraine bado hajaumia sana kwasababu Russia anaumiza miundombinu kama majengo nk.
Russia hajaumia mpaka sasa kwasababu ajaanza kushambuliwa nyumbani kwake na yeye aanze kujilinda.

Tuombe vita iishe ili Dunia iwe sehemu salama pa kuishi.
Nani aliyekuambia Russia anatumia askar wa kukodi tu? Kwa taarifa Yako Kuna makamanda wa juu kabisa wa Urusi tena wengi tu wameshapoteza maisha kwenye hii vita.
 
Sijaelewa mleta mada anasifia Russia Kwa kuwatoa askari wake kafara,,au anasifia jinsi waukraine walivyowatembezea mkong'oto askari wa urusi. ,Aliyeelewa afafanue tafadhari [emoji16]
Iko wazi kabisa kuwa tunasifia ushujaa.Iwapo wameamua kupigana na kushinda ni lazima wapigane.Pale wamekufa na wamepoteza vifaru vyao vya kizamani ambavyo vimekaa miaka mingi kwenye maghala na mwishowe wamepenya mpaka Bakhmut. Utawaita vipi askari kama wale wa Marekani waliokimbizwa mbio kule Kabul na wana ndege za kivita na vifaru na kila kitu.
 
Iko wazi kabisa kuwa tunasifia ushujaa.Iwapo wameamua kupigana na kushinda ni lazima wapigane.Pale wamekufa na wamepoteza vifaru vyao vya kizamani ambavyo vimekaa miaka mingi kwenye maghala na mwishowe wamepenya mpaka Bakhmut. Utawaita vipi askari kama wale wa Marekani waliokimbizwa mbio kule Kabul na wana ndege za kivita na vifaru na kila kitu.
USA ameondoka Afghanistan sio kwasababu ameshindwa bali alishapoteza interest zake Kabul..
Na Kama ulimsikiliza Biden vizuri alishasema majeshi yao kukaa Kabul yanaongeza tu bajeti ya nchi bila manufaa yeyote.
 
Bosi wa Wagner Prigozin sasa ametangaza rasmi kuikalia Bakhmut. Hata mkuu wa NATO naye japo hajasema kwa wazi naye amekubali kazi ya Bakhmut imeisha kwani yeye ametabiri kuanguka kwa Bakhmut baada ya siku tatu.

Sijui kama alichosema raisi Zelensky kama ni kweli dhidi ya uvumi kwamba ana msuguano mkubwa na makamanda wake waliotaka kuuachia mji huo mapema zaidi ili madhara kwa upande wao yasiongezeke.

Pamoja na hayo ni kweli Urusi imepata hasara kubwa na kuonesha ushujaa mkubwa katika vita kinyume na matangazo ya Uiengereza.

Imetajwa kwamba eneo la Vulhedar ilikuwa ni lazima warusi wapite ili kuingiza askari wake wa miguu katikati ya mji. Eneo lote likiwa limetegeshwa mabomu ya kuripua mizinga na huku wanajeshi wa Ukraine wakiwa wamejifcha maeneo ya vilima wakivizia vifaru hivyo kwa msaada wa upelelezi wa droni.

Walichofanya Urusi ni kuvurumisha vifaru vyake usawa huo huo hata kikiripuliwa kingine kinafuata njia hiyo hiyo kama kwamba cha mbele yake ndio kimesafisha njia.

Wanachosema Ukraine jumla ya vifaru 130 vya Urujsi siku hiyo viliripuliwa lakini hatimae vya nyuma vilifika mjini. Angalia vidio hapo chini Hao askari wa miguu nao waliofika huko walijipanga vikosi vidogo 20 ishirini.

Waukraine wanadai wakifika 20 wanawauwa lakini baada dakika 20 wanakuja wengine ishirini mpaka wakajichokea na kumaliza silaha zao. Kwa hakika hii ya Urusi ni dalili ya ushujaa wa hali ya juu katika vita na sidhani kama America ina askari kama hao.

Alichotabiri Zelenksy kuhusu Bakmut na kwamba wanasubiri vifaru vya NATO vifike wiki ijayo itakuwa ni dalili kuvujisha siri za vita na vilivyoipa mbinu Urusi kumalizia kazi yake mjini humo.

Muwe mnakumbuka kutuma na salam za rambirambi
 
Labda inabidi usome tena historia ya Syrian civil war
Ongezea na ya Afghanistan na Iraq

Halafu uje uoneshe u habari nyingine wa USA 🇺🇸 kwenye vita
Hahahahahah USA hata ukigoogle sehemu yoyote wanakwambia tu kuwa hajawahi kushinda vita yeyote zaidi ya kukimbia tu 🤣🤣🤣!

Halafu wamarekani ni wazuri kwenye movie zaidi il kwenye kufa waoga sana. Mwanajeshi akishakuwa muoga kufa anakuwa sawa na 0 tu. Thats very different to Russians. Wao ni aggressive fighters na hawaogopi kifo.
 
Jiongopee, hiki kifurushi cha tanks kitakachokuja awamu hii mtaita maji mma. 🤣🤣🤣!
Uzuri Russia ni kama Magong'ole tu, watapukutishwa mbaki mnazichungulia kwa mbaali nyuzi zenu mlizowaanzishia kuwasifu🤣🤣

Ila ninacho wasifu mashabiki wa Russia ni kama Mashabiki wa Arsenal tu, mna matarajio makubwa sana na hamkati tamaa. Tangu muahidiwa vita kumalizwa ndani ya siku tatu, ikaja Victory day, ikaja winter kote hola, lakini nyie mpo tu kama mzee Wasira🤣🤣🤣.

Sasa hiyo Bakhmut tangu mwezi December wanasema by next week itakua tayari wameshaichukua, leo tayari ni mwezi March😅😅.
Mnazidi kuahidiwa kuwa kuna vifurushi vinakuja
 
Umejaribu kuzingatia vikwazo alivyowekewa Urusi na support anayopata Ukraine kutoka NATO na EU? Je, unajua US walishindwa kumtoa Assadi pale Syria sababu ya support ya Russia? Tuweke ushabiki pembeni twende kwenye reality.
Tatizo kila sehemu ambayo kuna ujinga wa viongozi kikinuka tu USA, hasa kwa madikteta wasio kuwa na dira kama akina Assad, Gaddafi, etc.

Assad wako huyo alishakataliwa na raia wake, kwa kificha aibu akaweka nchi chini ukoloni wa Urusi, so yeye ni order ndio anapokea siku wakoloni wakichoka hana chake

Kwani waliokuwa wakiandamana pale Syria walikuwa ni wamarekani au??? Acha utoto unapojadili masuala mazito haya na wakubwa zako bwashee
 
Tumekusikia msemaji wa Wagner group na Urusi, muhimu unashindwa kuutambua nguvu na ujasiri wa Ukraine hapo tu ndo unapokosea msemaji.

Ukraine ni mbabe wa Russia, enzi za kuogopwa mrusi na majirani zake zimepitwa na wakati, mwaka umekata Putin ameshindwa kutwa Kyiv, alijaribu kupeleka pua yake Kyiv alichokipata hatamani kurudia tena.

Urusi anaendelea kupata hasara kila kukicha, jaribu kuwa mkweli ndg msemaji USA is another level, angekuwa ni USA mda huu tungekuwa tunazungumzia kusafisha safisha tu na kutoa msaada kwa raia wa huko baada ya mkong'oto mkali.

Urusi wamefeli bwashee, tuweke ushabiki maandazi pembeni, eb twende kiuhalisia, sioni kama mrusi atafanikiwa kilichobaki ni kujaribu kufuta aibu tu
Unaumwa, sehemu zote marekani alikokwenda kuvamia peke yake alichezea kichapo na ndio maana huwa haendi peke yake.

Russia ni mbabe sana. Hapo Ukraine Russia anawachapa NATO, umojja wa ulaya na kubwa lao USA
 
Mada ni tofauti sana na maudhui ya Video.

Maudhui yanaonyesha Urusi ilichezea kichapo vibaya sana
Maudhui ni kwamba ujasili na intelligence. Cha kujiuliza, je, walitoboa?

Ulishawahi kutazama movi ingawa na ya zamani inaitwa HARD WAY??

Hapo ilikuwa kwa vyovyote vile wafike ng'ambo na huo ndio ujasiri wa jeshi/askarl
 
Ukiumia unaweza kuendelea na mchezo? au unadhani Japan walipoumia kule Hiroshima aliendelea na mchezo?
Mkuu nimeuliza tu


Uliposema Ukraine 🇺🇦 hajaumia una maanisha nini?

Please nijibu badala ya kuniuliza tena maswali
 
Maudhui ni kwamba ujasili na intelligence. Cha kujiuliza, je, walitoboa?

Ulishawahi kutazama movi ingawa na ya zamani inaitwa HARD WAY??

Hapo ilikuwa kwa vyovyote vile wafike ng'ambo na huo ndio ujasiri wa jeshi/askarl
Afadhali umemfahamisha kama ataelewa.
Katika hali kama ile askari wa kweli lazima afanye kama vile.Ukiwa unajali maisha sehemu kama ile utashindwa vita.
 
Back
Top Bottom