Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Habari za Sabato!
Leo nilikuwa napitia hapa kitabu cha Asheri(Jasher). Nikaona kisa cha Waisrael kuwa utumwani kwa zaidi ya miaka 400 huko Misri.
Kisa hicho kwa sehemu kubwa ni simulizi ya kisiasa lakini yenye mchanganyiko na Imani ya Miungu.
Kupitia kisa hicho, moja yamambo niliyoyaona ni kuwa,
Wema na Haki inategemea subira, mikazo, ujasiri na kutokukataa tamaa.
Pili, nimejifunza pia ni muhimu kwa wazazi na jamii kuwarithisha watoto wao maadili, haki na ujasiri ili malengo ya mababu yatimie.
Kisa hiko kinaeleza pia kabla ya Nabii Musa kuzaliwa zilikuwa harakati nyingi za Waisrael kujikomboa kutoka utumwani. Na wengi waliuawa. Ingawaje Biblia ya kawaida haielezi Visa hivyo na harakati hizo.
Biblia ya kawaida inaeleza kuwa Waisrael waliteseka na kumlilia Mungu. Lakini kitabu cha Yasheri kinaelezea kwa undani hawakuishia kulia na kuteseka isipokuwa walimwomba Mungu na harakati zingine ikiwemo Mapigano ya mara Kwa mara yalijitokeza.
Hata hivyo, kisa kinaeleza pia pamoja na harakati zote. Wakati wa Mungu ukifika unakuwa umefika. Na ndipo Musa anazaliwa katika hali ya hatari ya kuuawa.
Wakati Farao akijitahidi kupambana na Watumwa wake, Waisrael. Kumbe anafanya kosa la kimsingi la kumchukua mtoto Musa na kumkuza mwenyewe ndani ya jumba lake.
Kisa kinaonyesha kuwa Mpasuko na ANGUKO LA Farao lilitokea ndani ya jumba lake wala sio nje.
Zile mbinu zote walizozitumia zilitumika hizohizo kumsulubu
Farao aliangamia baada ya Musa na majeshi yake akisaidiwa na Nguvu za Mungu wao(Yahwe)
Kisa hiki na visa vingine kama kisa cha Daudi ambavyo ni visa vya kisiasa.
Karibu vyote vinaonyesha Mpasuko wa dola huanziaga ndani.
Daudi hakutoka tuu from nowhere akachukua Dola ya Mfalme Sauli.
Daudi alikuwa mchungaji wa mbuzi huko porini.
Lakini alikaribishwa kumpigia Mfalme sauli kinubi na kumuimbia. Huko Ikulu aliimba kwa muda kidogo Sauli asijue anayemuimbia ndiye atachukua Dola.
Hizo ndizo siasa zilivyo. Siasa hazihitaji haraka. Siasa muda ukifika umefika.
Ukianza kujiona unastahili kuchukua Dola. Ni wazi hautachukua.
Wanaochukuaga Dola hawajijui ni mpaka dakika za mwisho ndio sauti huwaambia ni wewe.
Nimemalizaĺllĺ