Vitabu vinavyohamasisha mapenzi ya jinsia moja vyakamatwa Tabora

Vitabu vinavyohamasisha mapenzi ya jinsia moja vyakamatwa Tabora

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Serikali Mkoa wa Tabora imekamata shehena ya vitabu vyenye machapisho ya kufundisha na kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa wanaume na wanawake ambavyo vilikuwa mbioni kuanza kusambazwa katika shule za msingi na sekondari Wilayani Kaliua kupitia Taasisi isiyo ya kiserikali ya Athumani Kapuya.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paulo Chacha akiwa katika Wilaya ya Kaliua amesema vitabu hivyo vimewekwa kizuzini baada ya serikali kupitia watalamu wake kubaini kuwepo kwa uchafu wa maudhui katika vitabu hivyo ambayo vimeingizwa Wilayani humo na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Athumani Kapuya kwa lengo la kuvitoa msaada kwa shule za msingi na sekondari.

Akizungumza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt. Amini Joseph ameongeza kuwa Msaada huo wa vitabu uliingizwa Sanjali na vifaa tiba ikiwemo vilainishi na taulo za kike.

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt. Rashidi Chua chua amesema shehena hiyo imekamatwa ikiwa na vitabu zaidi ya elfu nane ambavyo huenda vingezifikia shule za msingi 139 na za sekondari 32 katika wilaya hiyo.

Kufuatia Sakata hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ameifungia Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali ya Athumani Kapuya kutokuendesha shughuli zake ndani ya Mkoa wa Tabora wakati huo akiagiza kukamatwa kwa waratibu na viongozi wa Taasisi hiyo.

Pia soma:
 
Tatizo vitabu vingi tunatumia kwa uzamini wa Marekani kwa nini tusiletewe na vitabu vya ushoga ndani tusipende dezo bali tuthamili tulivyonavyo kwanza ili kukabiliana na hili janga
 
Kwani inahitaji siku ngapi kumtia mbaroni Athuman Kapuya na wale mapacha wake? Huku kuchukua hatua kwa kujivuta vuta ndiko kunakoyalea huu upuuzi.

Ova
Ushoga kwa Tanzania ni kama ulishahalalishwa kinamna fulani hivi.

Hizo Taasisi zinajulikana na zinasajiriwa........vyombo vipi kila kona.

Kutoka povu kwamba unaweza kupambana nazo ni kujichosha tu.
 
Tatizo vitabu vingi tunatumia kwa uzamini wa marekani kwa nini tusiletewe na vitabu vya ushoga ndani tusipende dezo bali tuthamili tulivyonavyo kwanza ili kukabiliana na hili janga
Ningeshangaa kama ingefika post ya 10 bila Marekani kutajwa! Athuman Kapuya sio mtoto; wala sio maamuma! Ni profesa tena profesa wa elimu; msomi kweli kweli nchi hii. Amewahi kushika vyeo vingi nchi hii tangu uhadhiri, ubunge hadi uwaziri including wa elimu na ulinzi. Kafundisha na kukuza wengi Prof. Kapuya.

Kwa mtu wa kaliba hiyo, kulaumu wengine badala ya kujilaumu kwa ujinga wenu ni kujaribu kutafuta visingizio vya ku-justify ujinga huo. Kwani ni lazima kila mnachopewa na Marekani mpokee?
 
Kapuya kafanyaje tena hapo Kaliua?
 
Kufuatia Sakata hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ameifungia Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali ya Athumani Kapuya kutokuendesha shughuli zake ndani ya Mkoa wa Tabora wakati huo akiagiza kukamatwa kwa waratibu na viongozi wa Taasisi hiyo.
1717472761477.png
 
Back
Top Bottom