Vitabu vya Nyambari Nyangwine ni Janga la Taifa kwa ELimu Yetu

Vitabu vya Nyambari Nyangwine ni Janga la Taifa kwa ELimu Yetu

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
10,827
Reaction score
4,176
Nimesononeshwa sana na matokeo ya mitihani Kidato cha Nne ya Mwaka huu. Ni dhahiri kwamba kila mwaka kunakuwa na wanafunzi wanaofeli, lakini hili la 66% ya watahiniwa kufeli (kupata Division Zero) limeniuma sana.

Kuna sababu nyingi.....

kuanzia migomo ya walimu, watumishi wa umma kutishiwa nyau na serikali dhaifu, kiasi hata wengine kung'olewa meno. siasa kwenye elimu, hasa mijadala ya kishabiki ya wabunge wa ccm wanapokuwa bungeni kwa kuwa na tabia ya kusifia kila kitu kwa kauli za kijuha za 'kiwango cha ufaulu kimeongezeka ...tunaipongeza serikali' mambo yote ya namna hiyo.

lakini baya zaidi ni hili la utitiri wa vitabu vya rejea.

wakati siye tukisoma O'Level kulikuwa na vitabu dizaini moja tu. Vitabu vya Taasisi zetu adhimu...Taasisi ya Elimu Tanzania na Taasisi ya Kukuza Mitaala Tanzania. baada ya utandawazi na ubinafsishaji na nyonyaji na soko huria kumeibuka makanjanja wanaojifanya wanaandika vitabu vya maswali na majibu...moja wapo ni huyu jamaa anajiita Nyambari Nyangwine. Namshukuru Mungu sikuwahi kusoma vitabu vyake na hakika sitakuja kumshauri mtu avinunuwe. Haiwezekani kitabu kikawa na maswali na majibu tu halafu ukategemea kikusaidie kufaulu. hata kama utafaulu utakuwa bogazi tu kwa sababu huna maarifa kichwani.

Kwa kuwa waTZ tupo kama tumerogwa, basi hatuna budi tuchezee madini, tuchezee oembe za ndovu, tuchezee kila kitu, lakini TUSICHEZEE ELIMU.

vitabu vya Nyambari na makanjanja wenzake vipigwe marufuku. Walimu wapewe staha zao. Turudi kwenye mstari. Vinginevyo tunatia aibu, dunia ya leo kuwa kuzalisha wahitimu ambapo idadi ya waliofeli ni kubwa kuliko waliofaulu.
 
wewe una bifu na Nyangine ee! JE! KUNA VITABU MBADALA VYA KUELEWEKA?VITABU VYA TAASISI YA KUKUZA MITAALA NA WAKATI MBATIA ANASEMA HAKUNA MITAALA?
 
Nafikiri mtoa hoja katoa hoja sahihi kabisa. Haiwezekani watu wasome vitabu vya maswali na majibu halafu wategemee kufaulu. Hivyo vitabu vya wachapishaji wasio na ithbati vidhibitiwe. Wakati umefika wa taasisi ya elimu na ukuzaji wa mitaala kufanya kazi yake.
 
wewe una bifu na Nyangine ee! JE! KUNA VITABU MBADALA VYA KUELEWEKA?VITABU VYA TAASISI YA KUKUZA MITAALA NA WAKATI MBATIA ANASEMA HAKUNA MITAALA?

Mtaala upo, na kama haupo wewe usingefaulu. Mtaala upo ila wanauficha. labda tuambiwe sababu za kufichwa kwa Mtaala wa Elimu yetu ni nini?
 
Mtaala upo, na kama haupo wewe usingefaulu. Mtaala upo ila wanauficha. labda tuambiwe sababu za kufichwa kwa Mtaala wa Elimu yetu ni nini?

Kweli mkuu, inabidi Nyambari yeye mwenyewe apeleke HOJA BINAFSI kuilazimisha serikali ipige marufuku juu ya madesa yake na makanjanja wengine
 
hahahahahah haya mambo hamkuyaona kabla .its too late to start afreash
 
Mbaya zaidi haya madesa ndio NECTA huyatumia kama marking scheme!
 
actually nina ku award GT's honorable award for the year.

mkuu watu anasema mengi sana lakini wanasahahu kwamba hakuna elimu kama hakuna valid reference. Ukiangalia kwa makini utagunda kwamba Nyambari Nyangwine baadhi ya vitabu vyake vinapotosha sana sana tena vinahadaa kabisa. Upataji wa maarifa ni pamoja na kupata correct and proper knowledge of the subject matter.

sasa most of his books correctness of the subject matter ni ishu kubwa sana sana. angalia vitabu vyake vya litrature na english structure angalia vya biology ni uongo mtakatifu.

kule kwenye maswali na majibu ni uongo mtupu, sintosahau eti swali linasema ""name the vein which transports blood from the liver to the stomach"" jamani jamani kweli hii ni sahihi?? ukienda kwenye majibu unakuta jibu ni hepatic portal vein.

nilichowaambia wanafunzi wangu n kwamba wao wabaki wakariri majibu ya uongo na maarifa potofu huku wakidharau mafunzo ya waalimu wao.
 
Ki ukweli vitabu vya nyambari ni rubbish vina lemaza watoto ila kwa sababu ya ten percent vipo
 
nimesononeshwa sana na matokeo ya mitihani kidato cha nne ya mwaka huu. Ni dhahiri kwamba kila mwaka kunakuwa na wanafunzi wanaofeli, lakini hili la 66% ya watahiniwa kufeli (kupata division zero) limeniuma sana.

Kuna sababu nyingi.....

Kuanzia migomo ya walimu, watumishi wa umma kutishiwa nyau na serikali dhaifu, kiasi hata wengine kung'olewa meno. Siasa kwenye elimu, hasa mijadala ya kishabiki ya wabunge wa ccm wanapokuwa bungeni kwa kuwa na tabia ya kusifia kila kitu kwa kauli za kijuha za 'kiwango cha ufaulu kimeongezeka ...tunaipongeza serikali' mambo yote ya namna hiyo.

Lakini baya zaidi ni hili la utitiri wa vitabu vya rejea.

Wakati siye tukisoma o'level kulikuwa na vitabu dizaini moja tu. Vitabu vya taasisi zetu adhimu...taasisi ya elimu tanzania na taasisi ya kukuza mitaala tanzania. Baada ya utandawazi na ubinafsishaji na nyonyaji na soko huria kumeibuka makanjanja wanaojifanya wanaandika vitabu vya maswali na majibu...moja wapo ni huyu jamaa anajiita nyambari nyangwine. Namshukuru mungu sikuwahi kusoma vitabu vyake na hakika sitakuja kumshauri mtu avinunuwe. Haiwezekani kitabu kikawa na maswali na majibu tu halafu ukategemea kikusaidie kufaulu. Hata kama utafaulu utakuwa bogazi tu kwa sababu huna maarifa kichwani.

Kwa kuwa watz tupo kama tumerogwa, basi hatuna budi tuchezee madini, tuchezee oembe za ndovu, tuchezee kila kitu, lakini tusichezee elimu.

Vitabu vya nyambari na makanjanja wenzake vipigwe marufuku. Walimu wapewe staha zao. Turudi kwenye mstari. Vinginevyo tunatia aibu, dunia ya leo kuwa kuzalisha wahitimu ambapo idadi ya waliofeli ni kubwa kuliko waliofaulu.
umenifurahisha sana kwani mawazo yako yamegongana na yangu kimsingi ni kwamba vitabu vilivyopo mitaani havina quality na ndo vinadidimiza elim tanzania.
 
Mbaya zaidi haya madesa ndio NECTA huyatumia kama marking scheme!

nani kakuambia?? usiseme uongo ambao huna hakika nao. umewah kwenda marking?? je wajua kazi ya kwanza ya panelist ni ipi??

hebu acheni kudharau kazi za wenzenu ama kutufanya mambumbu. ingekuwa ni hivyo usingekuta kuna haja ya kuwa na waalimu darasani.

kama mnadhani fani hii ni ya vishoka kaa na mwanao home mfunze tooooop.
 
Hapa tutapiga kelele weeee lakini hakuna kitu. Cha msingi tuwawajibishe wahusika wakubwa ambao hata MITAALA wameikalia.
 
Kwani vipo katika mitaala kama reference books? Kama havipo kwanini vinatumika?
 
Kingine ni kila shule ina kitabu chake cha kiada,hapo ndipo shughuli inapoanza.
 
Back
Top Bottom