Sawa tunapinga ushoga kwasababu mbalimbali zikiwemo za kidini, madhara ya kiafya na kadhalika.
Lakini nilichogundua mimi ni kwamba kuna ukali sana kwenye upande wa mahusiano kati ya wanaume kwa wanaume lakini upande wa wanawake kwa wanawake kunachukuliwa poa tu. Mnaona sio tatizo zito. Watu wananiambia eti "haina shida" au "sio mbaya kama kwa wanaume".... Nataka niulize; Kivipi yaani?
Sielewi kinachoendelea hapa, Sioni kama kuna sababu yeyote ya kimsingi ya kutetea hawa mnaowaita "wasagaji". Dini nina uhakika hairuhusu, Madhara ya kiafya lazima yawepo kwasababu sii kitu "asili".....
Kwahiyo nakuja kwenu wanajamii, Je kuna mahali hapo ninakosea? Hili swala vipi?
Hii hali hata mimi nimeiona.
Kinachotokea hapo ni kwamba, patriarchy (mfumodume) una tabia ya kutukuza machismo (umwamba).
Katika mfumodume, kuzaliwa mwanamme ni bahati, ni utukufu, ni ukuu.
Kuzaliwa mwanamke ni udhaifu.
Ushawahi kuona picha zimechorwa wakati tinu ya Simba imefungwa na Yanga, Simba kachorwa kama mwanamke kapakatwa na Yanga dume? Maana yake nini? Maana yake kufungwa ni udhaifu, na udhaifu unahusishwa na wanawake, ndiyo maana anayefungwa anakuwa mwanamke kapakatwa na aliyeshinda anakuwa mwanamme.
Mfumodume.
Sasa, katika mfumodume huu, mwanamke kuwa na mpenzi mwanamke si big deal.
Kwa sababu si mwanamke tu, akiwa na mpenzi mwanamke hashuki station yake, yani kwa akili hizo mwanamke ni kiumbe cha chini kabisa, hawezi kushuka chini zaidi kwa kuwa na mpenzi mwanamke, wanasema tu "huyu hajapata mwanamme wa kumshughulikia vizuri. Akipata ataacha". Yani kuna watu wakiona lesbian sehemu wanalaumu wanaume wa hapo, kwamba wameshindwa kazi zao. Hawaoni kwamba mwanamke anaweza kujiamulia mwenyewe kukataa wanaume na kuwa na mpenzi mwanamke.
Ila, mwanamme aliyezaliwa mwanamme, akiamua kuutupilia mbali uanamme wake, akaamua kuwa anakazwa, kwa raha zake nanuhuru wake mwenyewe kwenye mwili wake mwenyewr, hapo mfumodume unapata matatizo sana, kwa sababu mwanamme huyo anaonekana yeye kashinda lottery ya nature ya kuzaliwa mwanamme, halafu kaikataa, kasema yeye anataka kukazwa kama mwanamke.
Pia note kwamba mara nyingi mashoga wanaoshikiwa bango ni bottoms (wanaofirwa), sio mabasha. Yani basha (top)anaonekana kidogo afadhali kwa sababu yeyr bado ana kauanaume fulani kuwafanya wenzake, ingawa naye anaonekana msaliti kwa sababu anawaingikia wanaume wenzake na si wanawake.
Kuna saikolojia kubwa ya dominance, patriarchy na power plays in gender politics, conscious but largely subconsciously.
Kitendo cha kujamiiana na mambo ya gender identity yamekuwa kama vita ya kuwaeeka watu fulani chini, na wengine juu.
Na hawa gays ni kama the most vulnerable and least common denominator hated group in society.
Yani wewe hata kama ni mjinga vipi, masikini vipi, loser vipi, usipokuwa kundi hili la gays, na unatafuta namna ya kujisikia una afadhali katika ujinga wako, umasikini wako, u liser wako, wapige mawe tu hili kundi.
Utapata watu kibao wa kukupa uncritical support na kukufanya ujisikie vizuri.
Na wabongo wanapenda sana habari za kusema mambo kwa mkumbo.
Hapo ndipo unakuta everybody is piling up on the gays, without even understanding the biology, psychology, issues of autonomy and personal freedom, human rights.
Hizo habari za kupunga ushoga kwa dini ni ujinga tu, si kila mtu anaamini dini zenu.
Leo Waislamu wakilazimisha kila mtu asile nguruwe kwa sababu nguruwe ni haramu kwenye dini yao utaona sawa?
Habari za kiafya zipi za kupinga ushoga?
Watu wanaambukizana UKIMWI kila siku kwa heterosexual sex, umepinga watu wasifanye heterosexual sex kwa furaha na faragha zao wakikubaliana?
Wakati huo huo wachimbaji wamekufa mgodini hakuna hata mtu anayeulizia usalama wa Watanzania migodini.
It's a pathetic sense of puritanism and fake modesty.
Wabongo wengi ndiyo wako hivyo.
View attachment 2552454