Dunia kwa sasa iko katikati ya jambo hatari zaidi la kimaadili linalo hatarisha uwepo wa familia na mwendelezo wa vizazi. Vuguvugu la mahusiano yaliyo kinyume na asili (ushoga, ubasha, usagaji) limekuwa likishika kasi duniani huku likisukumwa na upepo wa mataifa ya magharibi chini ya mwamvuli wa haki za binadamu na uhuru wa mtu binafsi katika kujiamulia maisha yake katika kufurahi pasipo kuingiliwa faragha yake. Kwa nguvu, pesa, akili na mbinu mbalimbali wahusika wa vitendo hivyo duniani wanafanya jitihada kubwa kuvieneza huku wakivipandikiza kupitia mitandao, vitabu, majarida, sheria, serikali, dini, shule, vyuo, michezo, burudani, mitindo nk.
Kwa hapa Tanzania hali imeanza kumea kama magugu shambani, na kila mara watu wanaojitokeza hadharani kwa nguvu kulikemea au kulipinga hilo jambo ghafla hapo hapo kuna watu wengine wanaibuka kuwapinga kwa hoja kuwa kulikemea vikali hilo suala ni kulikuza au sio suala muhimu kujadiliwa au hayo ni mambo binafsi ya watu hivyo hayapaswi kupigwa vita!
Napenda kuandika hapa JF, mtu yoyote anayeibuka na hoja ya kusema kuwa tukae kimya kwenye hili suala (kwa hoja ya kuogopa kulikuza au kukwepa kuingilia mambo binafsi ya watu) kuna uwezekano mkubwa sana muhusika akawa ni sehemu ya wanufaika wa mpango wa kueneza ushoga hapa Tanzania kwa kuwa hakuna sayansi inayoeleza namna ukimya utatatua tatizo la kijamii linalosukumwa na kuenezwa kimakusudi na watu wengine tena wenye kutumia akili, pesa na ujanja mwingi.
Tangu lini ukimya dhidi ya uovu unaweza kufifisha huo uovu?
Ni kwa namna gani tukikaa kimya dhidi ya ushoga, ubasha na usagaji basi automatically hivyo vitendo vitatoweka kwenye jamii?
Dawa ya kwanza ya kupambana na ushoga, ubasha na usagaji ni kuukemea hadharani kwa ujasiri wote, kwa nguvu zote tena kila mara.
HAKUNA KUKAA KIMYA.