Sihitaji salamu,hizo nimewaachia watu wa pwani Dar na Zanzibar!.
Hivi unadhani ni kwanini suala la Usagaji wa Mahindi kutoka Sumbawanga halipewi kipaumbele kwenye mijadala mingi ukilinganisha na suala la ushoga baina ya Mwajuma na Rebecca?,Je Ushoga wa Mwajuma na Rebbeca ni kitu hatarishi sana katika jamii ya watanzania kuliko Usagaji wa mahindi kutoka Sumbawanga?
Mijadala mingi hapa JF imekuwa ikiongelea na kugusia Ushoga baina ya Mwajuma na Rebbeca lakini sijaona kabisa mijadala kuhusu Usagaji wa nafaka aina ya Mahindi kutoka Sumbawanga,Je ni halali kusagwa kwa mahindi kutoka Sumbawanga katika mashine zetu ila Ushoga baina ya Mwajuma na Rebbeca ni haramu?
Hii imekaaje?
Au ndo yale yale ya Kuingiliwa kinyume na maumbile kwa mtu mume ni haramu ila kuingiliwa kinyume na maumbile mtu muke ni halali?
View attachment 2646971