Labda hujanisoma post zangu za nyuma, Mimi napinga vikali ushoga, lakini IPhone ndio simu Salama duniani kwa Sasa.
Mimi situmii IPhone kwa Sababu ya gharama yake lakini si kwa sababu ya ushoga.
Na ninasisitiza kama uwezo wako ni Infinix tumia hiyo ila usitafute excuse ya kutotumia IPhone eti kwa sababu ni product ya mashoga, huu ni ukosefu wa akili.
Leo mtu anipe offer ya Ki rafiki ya IPhone nitaipokea kwa mikono mwili tena nitaseti kwenye settings mjuwe Dr Matola PhD anapost akitumia IPhone pro max.
Hakuna mtu mwenye akili timamu hapendi vitu vizuri, si kwamba sina pesa ya kujinunulia IPhone latest lakini Nina vipaumbele vyangu, Mimi ni Family Man, familia inahitaji mahitaji kuliko hiyo IPhone.
Mimi wakati wa ujana ndio watu wachache tuliomiliki Blackberry curve and bold mwanzoni, huu siyo wakati wetu ila kwa vijana na wazee wenye pesa ndefu.