Salaam,
Niende Moja Kwa Moja kwenye hoja yangu, Kwa Imani Mimi ni mkristo napenda kuchimba sana kwenye Biblia maana naamini kabisa ni neno la MUNGU -Zaburi 119:105
Sasa Kuna watu naona wapo mstari wa mbele kupinga ushoga na hata kutaka mashoga wauawe kana kwamba uasherati na uzinzi wao sio tatizo. Watu wanajisifu kulana kimasihara, kula wake za watu kushindana ni nani kalala na idadi kubwa ya wanawake na anaona ni ufahari kabisa ila anapinga ushoga kana kwamba dhambi zake yeye ni halali
Sitetei tabia ya ushoga ila ninachotaka kusema ni kwamba dhambi ni dhambi na usifikiri dhambi yako wewe ni nzuri ila ya mwenzio ndio mbaya.
Kwa wale wenzangu ambao ni wasomaji wa Biblia turejee 1Korintho 6:9,10 dhambi zote hizo ni chukizo Kwa Muumba wetu na kila anayezifanya hataingia kwenye ufalme wa MUNGU
Rejea pia Galatia 5:19-21 kuhusu matendo ya mwili ambayo ni chukizo mbele za MUNGU
Hivyo basi ikiwa tunataka kuwa watu safi mbele za Muumba wetu mtakatifu tuache na pia tukemee dhambi zote hizo bila kubagua vinginevyo ni kwamba anayesema wema ni uovu na anayesema uovu ni wema wote hao ni chukizo mbele za MUNGU.
Amani iwe nanyi, muwe na jioni njema