Ama kampeni ya kupinga wizi na ufisadi na rushwa tukirejea report ya CAG.
Umeona mkuu, hapo tutakuwa tume-hit the spot(tumemkamata mchwawi).
Maana haiwezekani taifa zima makanisani, misikitini, wanasiasa, waandishi wa habari n.k n.k lizunguziwe na kukemewa jambo moja tu kana kwamba ndo kitu kinalimaliza taifa letu, hapana!
Kweli ushoga ni mbaya na wa kupingwa kwa nguvu zote sababu unatuharibia vijana wetu, lakini je? Vipi kuhusu UFISADI, UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA, MATRILLION YANAYORIPOTIWA KUPOTEA baada ya CAG kufanya ukaguzi? Si yanasababisha umasikini!
Vifo mahospitalini kwa kukosa madawa na posho/mishahara na motisha kwa watumishi wa afya!
Barabara mbovu za vumbi za kurekebisha kila mwaka wakati pesa hizo zingetumika kutengeneza lami kila mahali, au ziwape vijana wetu scholarship vyuo vya nje maana hii ya kwetu haina tija mpaka leo barabara, madaraja na reli wanajenga wachina na waturuki maana yake sisi hatuna maarifa ni wajinga!
UJINGA MARADHI NA UMASIKINI! leo tunapiga kelele eti ushoga kweli? Tuko serious?
Hiki ni kituko kilichopangwa na kuratibiwa vyema kabisa! Pongezi kwake director wa muvi hii mpaka sasa Box Office imeshauza $500m