Vitendo vya Ushoga vinaongezeka kwa kasi sana

Vitendo vya Ushoga vinaongezeka kwa kasi sana

Sheria za nchi yetu zinakataa mapenzi ya Jinsia moja na zinakataza kwa msisitizo mwanaume kuingiliwa kinyume

Kinachotakiwa ni kuhakikisha kila tukio sheria inachukua mkondo wake
 
Mimi sio tambi tambi ila huu uzi utagonga 1K comments within 24hrs
 
Hebu tujadilini mambo ya maana, Yani Rais aache kufanyia Kazi mapendekezo ya CAG atoe matamko kuhusu hizo laana?
Tatizo la watanzania ni malalamiko na kutafuta mtu wa kumtupia lawama always, kila mtu achukue nafasi yake kwenye jamii, hayo matamko tuyatoe kwenye familia zetu....Kwa taarifa yako waendesha hizo kampeni za ushoga hawana shida na nyie mibaba mijitu mizima yenye miaka 36 sijui 43 mliokomaa videvu, target Yao ni hawa watoto wadogo wasiojua Jema na Baya....sasa wewe unataka ukeshe bar, mkeo ashinde group za wasap halafu Rais Samia ndo akulele na kumfunza mwanao, tena Kwa tamko🤣🤣🤣
Hebu kila mmoja atimize wajibu wake, wewe mwenyewe ni Rais hapo ulipo.
 
✳️MAMA SAMIA USIMUNG'UNYE MANENO,IKIWA KUNA USHOGA SEMA KUNA USHOGA‼️TOA MSIMAMO WA SERIKALI YAKO KWA TAIFA ZIMA KUHUSU HILI WIMBI LA USHOGA‼️

Wakati nchi ipo katika hii sintofahamu ya kuzuka kwa wimbi hili la ushoga, nimesikitishwa sana sana na kauli mbalimbali za Rais wa nchi ya Tanzania,Mama Samia katika hotuba zake kadhaa ambazo ndizo alionekana kama analizungumzia hili wimbi linaloendelea,lakini cha kushangaza eti Rais wa nchi anaogopa hata kulitaja Neno ushoga katika hotuba zake hizo alizosikika akiwa anahutubia bali anamung'unya maneno kwa kuupaka rangi ushoga na kuuita Mila na desturi za nje?

Na Nukuu. " Acheni kuiga ya Nje,Ishini kwa maadili yetu!Wewe mtanzania ujulikane wewe ni mtanzania!!tuna mila na desturi zetu za kitanzania.Ya nje yale tunayoletewa hayatupeleki pazuri!! Amesema mlezi kuna wimbi hilo limeingia sasa hivi!Mimi niwaombe sasa sana ndugu zangu,Muwe mabalozi wa wenzenu!! Walindeni wenzenu!! Hii haki inayosemwa kuwa ni haki ya binadamu,Hizi haki zina mipaka yake! Kila pahali kuna mila na desturi zake.Tusilazimishe mambo ambayo sio mila na desturi zetu tukataka kuletewa kama mila na desturi zetu" ...Asema mama Samia

Zaidi sana kuonyesha Rais amelichulia kiwepesi swala hili ameishia kuwaonya tu viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kuwa waache kuiga mila na desturi za nje ,katika hiyo hotuba yake tena baada ya mlezi wa wanafunzi kuligusia swala hilo kwa kunyoosha maneno "Wanafunzi msijihusishe na Masuala ya mapenzi ya Jinsia Moja yaani Ushoga na usagaji ".

Kwanza,Nimeshangaa sana, Rais wa nchi kushindwa kunyoosha maneno kwa kushindwa hata kuutaja ushoga kwa jina eti anauita mila na desturi za nje⁉️.Hili swala ikiwa Rais ametambua limekuwa ni wimbi sio wakati wa kukaa kimya au kumung'unya maneno kama alivyofanya na kulizungumzia kivificho na kwa juu juu tena na kundi la watu wachache


View attachment 2580613


Pili, sisi wananchi tunachotaka, ni Serikali ije na hotuba maalum ya Taifa na itoe msimamo wa serikali hii ya awamu ya sita ya Mama Samia kuhusu hili wanaloliita wimbi la ushoga na usagaji Tanzania kulingana na Ripoti na taarifa zilizotolewa na Dr Mwakyembe hivi karibuni kubaini kuwa yapo mashirika na taasisi nyingi nchini zilizosajiliwa kabisa Tanzania kufanya uhamasishaji wa maswala ya wapenzi wa jinsia moja

Wakati wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Magufuli, Msimamo ulitolewa kuwa Nchi yetu ya Tanzania inaheshimu mikataba yote ya haki za Binadamu wala haipigi vita ya ushoga na usagaji kama ulivyoanzishwa na Paul makonda wakati ule.Je awamu hii ya sita mpo kinyume na msimamo wa serikali ya awamu ya tano kuhusu msimamo ya maswala ya Ushoga na haki za binadamu?

Tunaiomba Serikali yetu ya Tanzania, kupitia kwa Rais wetu samia ,iweze kutuelimisha jamii, ni mikataba gani hiyo ya haki za binadamu mliyosaini kuilinda na kuitetea haki za mashoga ambayo Serikali hiyo hiyo ya awamu ya Tano ilisema inaiheshimu lilipokuja swala la ushoga? Na ikiwa hamjasaini chochote kwanini mnalalamika mnalazimishwa mkubali mila na desturi ambazo sio za kwenu?

Tatu, wananchi tunahitaji hotuba itakayotupa majibu mengi ya maswali yetu! Tunahitaji kujua hizo asasi za kiraia za haki za binadamu na mashirika yote yanayojihusisha na maswala ya wapenzi wa jinsia moja, Ni nani amewasajili hapa Tanzania ?Yameingiaje nchini ?na hatua gani mnazichukua dhidi yao wote wanaojihusisha na maswal haya ya mapenzi ya jinsia moja ambayo yapo kinyume na sheria zetu za Tanzania?

Nne, Ikiwa Rais ameonyesha kujua kuwa lipo wimbi la ushoga na usagaji katika nchi yake,Ni kwanini mpaka sasa Serikali ipo kimya haijatoa msimamo wake kwa ulimwengu kupinga hizo mila na desturi wanazoziita za kigeni ?Je ni hatua gani serikali imefanya ya kupambana na vita hii au ni watu gani wamekamatwa ili kuwajibishwa kutokana na kujihusisha na vitendo hivi vya mapenzi ya jinsia moja?
Msimamo wa Nini wakati sheria tayari zipo kwamba ukijihusisha na ushoga Kuna extreme measures kama kifungo Cha mpaka miaka 30 depending na umri wa uliyemnajisi. Sio tu ushoga hata kumuingilia mkeo kinyume na maumbile nayo ni kifungo kikali.



Sasa mnataka msimamo Gani Tena wakati hayo anayofanya Museveni kwa Sasa tumeshayafanya miaka mingi iliyopita? Ingekua hakuna sheria kuhusu suala Hilo hapo ungekua na hoja. Kazi ni kwa DPP Sasa kuhakikisha anawaburuza mahakamani wenye kesi hizo na hata wwe kama unafahamu Kuna mtu anaingiliwa au anaingiliwa watu kinyume either ME au KE kashtaki maana sheria zipo na atafungwa kuliko kulia Lia mtandaoni wakati tayari maelekezo yapo.
 
Hebu tujadilini mambo ya maana, Yani Rais aache kufanyia Kazi mapendekezo ya CAG atoe matamko kuhusu hizo laana?
Tatizo la watanzania ni malalamiko na kutafuta mtu wa kumtupia lawama always, kila mtu achukue nafasi yake kwenye jamii, hayo matamko tuyatoe kwenye familia zetu....Kwa taarifa yako waendesha hizo kampeni za ushoga hawana shida na nyie mibaba mijitu mizima yenye miaka 36 sijui 43 mliokomaa videvu, target Yao ni hawa watoto wadogo wasiojua Jema na Baya....sasa wewe unataka ukeshe bar, mkeo ashinde group za wasap halafu Rais Samia ndo akulele na kumfunza mwanao, tena Kwa tamko[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hebu kila mmoja atimize wajibu wake, wewe mwenyewe ni Rais hapo ulipo.
Wee nashindwa kukuelewa je una maana MTU mzima ni haki kuwa shoga ila kwa mtoto Ni haramu? Au tuseme mtu mzima mwanaume ni halali kumwingilia mwanamke kinyume cha maumbile na Ni kosa pale inapokuwa Ni mtoto ameingiliwa? Mnajaribu kuhamisha magoli lakini semeni ukweli kuwa kuna mahali tumeshajifunga na mikataba sasa mnakosa pakutokea
 
Wee nashindwa kukuelewa je una maana MTU mzima ni haki kuwa shoga ila kwa mtoto Ni haramu? Au tuseme mtu mzima mwanaume ni halali kumwingilia mwanamke kinyume cha maumbile na Ni kosa pale inapokuwa Ni mtoto ameingiliwa? Mnajaribu kuhamisha magoli lakini semeni ukweli kuwa kuna mahali tumeshajifunga na mikataba sasa mnakosa pakutokea
Nachomaanisha hata Rais akitoa tamko hamna kitachobadilika, mabadiliko yanaanzia na kila mmoja wetu....pia hii kampeni IPO serious, target Yao sio Sisi watu wazima, hivi mbaba Kama wewe utaahidiwa nini Ili uwe papai? Wao wanataka hao watoto Ili waharibu kizazi kijacho, hivyo tulinde vijana wetu, tamko halilei watoto.
Sasa hata Rais akitoa tamko, halafu ndio nini? Sisi wanajamii tuupinge uliwati Kwa nguvu zote.
 
Back
Top Bottom