Hivi ni mimi pekee yangu nimeona na naendelea kuona????
Jana wakati naangalia mpira kupitia dstv channel 223 supersport likawa linakuja tangazo la golf kipindi cha mapumziko, kwenye lile tangazo wanaleta za rainbow, yaani zile alama za upinde zinaonekana japo kwa kificho kificho, na hata tena wakati naangalia marudio ya mpira wa jana Man Utd na Everton nimeliona lile tangazo lao la upinde.
Hata leo kwenye mechi kali ya Liverpool na Arsenal watakua wanaleta hilo tangazo lao,jamani hivi kwa nini hili suala linapigiwa chapuo sana?? Dstv huna napenda kuangalia mpira, kama wanaonyesha hayo mambo yao ya ajabu ajabu nitaacha kabisa kulipia hii huduma yao kusema na ukweli,kijana wangumakawa anasema kuna channel nyingi sana zimefungiwa dstv,maana nilikua sijui kama kuna channel za dstv zimefungiwa!!
Serikali yangu ya Tanzania,taasisi za dini kama Bakwata,Tec,na wengine wenye nguvu,tuungane pamoja kukemea huu ujinga, sisi tuna mila na tamaduni zetu,pia hata maandiko yanasema wazi,familia ni Baba,Mama na watoto, sasa iweje leo hii mwanaume aoe mwanaume mwenzake au mwanamke aoe mwanamke mwenzake?? Kuna familia kweli hapo???