1. Nchi gani ya kiarabu imepitisha ushoga?
2. Umeandika nchi za Kiarabu na kwenye mabano umeweka "Islamic"!!! Ujue kutofautisha kati ya nchi za kiisilam na nchi za Kiarabu, kwa sababu si kila nchi ya kiarabu ni ya Kiislam, kama ambavyo si kila muarabu ni Muislam, wengine ni Wakristo.
3. Umeweka kama vile waarabu wote wanatoka nchi moja, hapana, nchi za kiarabu zipo tofauti kama zilivyo nchi za kiafrika, hivyo, huwezi kusema kama kitu kimepitishwa na nchi moja ya kiafrika basi waafrika wote wanahusika.
4. Itapendeza kama ukitoa taarifa usitoe kiujumla, usiseme nchi za kiarabu, ila taja nchi kwa jina lake, kama ambavyo huwezi kutaja nchi za kiafrika kwa ujumla kwa sababu zote zina sera na misimamo tofauti.