Labda nithibitishe kwanza, mimi napendelea sana maamuzi yanayofuata sheria ambazo zimewekwa - rules based orders.
Nimesikia kuna hawa wanamitindo wamewekwa kizuizini na mahakama kuamuru wakapimwe kama ni mashoga.
Sina ubaya na hilo kwasababu na mimi sisupport vitendo vya ushoga. Ila ambacho ningependa kujua ni kuhusu hayo mamlaka na nguvu ya mahakama kwenye vifungu vya sheria kuamua mtu apimwe kama yeye ni shoga pasipo idhini yake.
Nimeuliza hivo kwasababu, tusipokuwa makini, hii kitu inaweza kutumika kufanya defamation na character assassination.
Imagine leo hii mtu unafanya kazi ya maana na unakutana na watu wengi, unaheshimika na ukoo wako, halafu from no where unasikia kwamba umewekwa lock up kwamba ukapimwe kama wewe ni shoga. Halafu inagundulika kwamba sio kweli. Unadhani utachafuka kiasi gani?
Kuna kitu hakipo sawa kwenye hili. Kwa wanasheria
Pascal Mayalla na wengineo embu tunaomba ufafanuzi kwenye hili.
Mi sio mwanasheria ila, nina guts feeling kwamba kuna kitu cha kisheria hakijakaa sawa hapa.