FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Hayo maneno uliyoyaandika siyo adhana, hao ni wanadi sala, kitu ambacho hakipo kwenye mafundisho ya Kiislam. Ni utamaduni uliojijenga toka wakati hakuna vipaza sauti na hujitolea mtu kupita nyumba hadi nyumba kuamsha Waislam. Mara nyingi hao hupatikana maeneo yenye Waislam wengi, tena utamaduni huo siku hizi umepotea sana. Nakushauri uhame tu maeneo yenye Waislam wengi au chukulia positive kuwa wanakuamsha uwahi shughuli zako. Wacha uvivu, sala ni bora kwako kuliko usingizi.Maneno hasi ya Azana yananifanya nisilale kila ifikapo alfajiri.
Kwa mbali naskia "Swalah Swalah
Kitanda chako ndio kaburi lako
Usingizi wako ndio kifo chako" na maneno mengine ya kukutoa kitandani.
Oya hz Mambo Kama wangeweza kupigiana simu waambiane muda wa kuswali umefika ingependeza zaidi
Mana tunaosikia hivyo vitisho ni wengi hasa ss tunaolala nusu nusu
Najua Sehem ya wahusika mnasoma na isiishie hapo mkaambiane huko uongozini Mana hw wa mtaani kwang wanajitia viziwi
Adhana ni hii:
Wito wa sala (adhan) hutolewa mara tano kwa siku na muadhin kuwakumbusha Waislam kuja kwenye sala ya faradhi na kuacha mambo ya kidunia nyuma.
Jinsi gani wito wa adhana unafanywa?
Mtu anayefanya adhan anaitwa muadhin, inaitwa kwa Kiarabu.Wakati wa adhan, Waislam wanapaswa kuacha na kuisikiliza. Neno adhan lenyewe linamaanisha "kusikiliza".
Haya ndiyo yanayosemwa katika adhan; Maneno ya kwanza yanasemwa mara nne na mengine mara mbili.
Allahu Akbar - Mungu ni Mkubwa
Ashhadu an la ilaha ila Allah - nashuhudia kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja.
Ashadu anna Muhammadan Rasool Allah - Nashuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu
Hayya 'ala-s-Salah - Hurry to the Prayer (Wake Up for Prayer)
Hayya 'ala-l-Falah - Haraka kwa mafanikio (Rise up for Salvation)
Assalatu khairum-minan-naum - Sala ni bora kuliko usingizi (Sehemu hii inasomwa tu kwa sala za asubuhi.)
Allahu Akbar - Mungu ni Mkubwa
Ilaah illa Allaah hapana mungu ila Mungu Mmoja tu.
Muadhans kawaida huchaguliwa kulingana na tabia nzuri na / au renditions yao ya kusonga ya adhan. Adhans maarufu zinaweza kusikilizwa mtandaoni.