Vitoto vya nyoka nyumbani kwangu

Vitoto vya nyoka nyumbani kwangu

Kwamba mlinzi akasonya huku anawasha kiredio chake na kuondoka[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aise umejua kunichekesha..nimwcheka hadi machozi..how come unaogopa nyoka🥵🙌
How come naogopa nyoka mkuu?
We are talking about nyoka mkuu!NYOKA yule anatembea kwa waves!Mmmhh.

Ameuliwa nikaonyeshwa huyu hapa,nikaona amekufa ndio nikaenda kujisaidia.Na jana ndo nimejua kibofu changu kiko imara🤣
 
How come naogopa nyoka mkuu?
We are talking about nyoka mkuu!NYOKA yule anatembea kwa waves!Mmmhh.

Ameuliwa nikaonyeshwa huyu hapa,nikaona amekufa ndio nikaenda kujisaidia.Na jana ndo nimejua kibofu changu kiko imara🤣
🤣🤣🤣🤣 kweli tumepishana kuogopa vitu .mimi chura, washawasha🙌🙌🥵🥵..nyoka hata awe mkubwa vipi napambana had namuua...wananishangaaga .ila sio chura au washawasha🙌
 
🤣🤣🤣🤣 kweli tumepishana kuogopa vitu .mimi chura, washawasha🙌🙌🥵🥵..nyoka hata awe mkubwa vipi napambana had namuua...wananishangaaga .ila sio chura au washawasha🙌
Hongera sana dear ila usije ukaleta ubabe wako kwa black mambo mkuu.
Huyo lazima akutoe nishai
 
Hhhhhh mkuu Jeep rubicon you made me laugh like a little kid

Sweet innocent you 😂
Hello people.
Naandika hapa nikiwa natetemeka jamani niko ndani ya neti naogopa kushusha miguu chini na nimebanwa na haja lakini naogopa kwenda chooni.😭

Ni hivi,nilikua naenda kuoga bafuni ile kuwasha taa nikaona kitoto cha nyoka cheusi kinatembea kwenye maungio ya tiles.

Nilivyokiona tu kile kinyoka akili ikanambia mama yake hayuko mbali.Nikajikuta natengeneza picha ya mama yake na kwa jinsi ninavyoogopa nyoka nikajikuta napiga yowe moja kali nikageuka fasta kurud chumban na ku dive kitandani na kuchomekea neti.Moyo unadunda nataman kulia na sitapata usingizi leo.

Two weeks ago niliona tena kitoto cha nyoka kama hichi cha leo ila kilikua kimekufa na kwa vile mazingira yalisafishwa na kilikua kimekufa sikujali.

Hichi cha leo kimenitia presha sikuwahi kuwaza nitaona nyoka ndani ya nyumba yangu.Yesu nitetee mimi jamani😭.

Nahisi tu kuna wazazi wao somewhere nyumban kwangu wanazaliana tu jamani😭.Sijui wako mvunguni,sijui wako chini ya bathtub,sijui wako kabatin,sijui wako kwenye moja ya mapoch yangu.

Sitakua tena na amani na hii nyumba,ingekua ugenin kesho ningeaga ila hapa ni kwangu na mbaya nyumba ni kubwa na kila room imejaa vitu.Hata nikitafute mtu anisaidie kuwatafuta awaue ataanzia wapi aishie wapi?

Mlinzi kaja dirishan anauliza madam vp mbona mayowe?Namwambia kuna nyoka bafuni kwangu.Anauliza mkubwa kias gani?Namwambia ni kitoto kama kile tulichoona kimekufa siku ile.Baada ya kumjibu hivyo namsikia anafyonza huko nje then anawasha kiredio chake anaondoka.Namwambia sasa unanisaidiaje?Anasema huyo ni kama mjusi tu we lala then namsikia mwenzie anacheka hlf anamwambia mwambie ni kama mnyoo au hujui kuna siku huyo alishavunja mguu kwa kuogopa mjusi.?

Anyways.Wakuu naomba mnisaidie mawazo ya nini kifanyike kuhakikisha hawa viumbe kama wanaishi humu ndani wanatoka na kufa kabisa.

Hivi hakuna dawa ya ku spray nipulize nyumba nzima kama wapo wafe?

Pia naomba kujuzwa,hivi ukiona vitoto si ni ishara kuwa wazazi wao wapo around eeh?
 
Huyu ndo nyoka alosababisha nisioge jana,nisipate usingizi na nibane haja kwa zaidi ya saa 4.
Najua kuna watakaonicheka ila mi najua mtoto wa nyoka ni nyoka na kuna sehemu nilisoma kuna vitoto vya nyoka vina sumu kali kama za nyoka wakubwa.

Mkuu Carica_papaya minyoo unayoiongelea iko kama.hivi ?
Screenshot_20230415-151701.png
Screenshot_20230415-151701.png
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hao wazazi wake watakuwa hawatumii kondomu....haiwezekani wawe wana zaliana haraka harak hivo...hata matanga ya kitoto cha kwanza hayajaisha
 
Huyu ndo nyoka alosababisha nisioge jana,nisipate usingizi na nibane haja kwa zaidi ya saa 4.
Najua kuna watakaonicheka ila mi najua mtoto wa nyoka ni nyoka na kuna sehemu nilisoma kuna vitoto vya nyoka vina sumu kali kama za nyoka wakubwa.View attachment 2588817View attachment 2588817
Hivi angekuwa Snake Xenzia ungelala kweli ? .
Ngoja nije PM mrembo nikupigie voko.
 
Unaweza Kuwasiliana na Mimi.
Ninapuliza Dawa maalumu ya kuangamiza na Kufukuza wadudu waharibifu Kama Vile
Popo, Mchwa, Mende, Mijusi Panya Na Nyoka. Karibu Sana Bei Nafuu Huduma ya Uhakika
 
Unaweza Kuwasiliana na Mimi.
Ninapuliza Dawa maalumu ya kuangamiza na Kufukuza wadudu waharibifu Kama Vile
Popo, Mchwa, Mende, Mijusi Panya Na Nyoka. Karibu Sana Bei Nafuu Huduma ya Uhakika
Wasipotokea nilioongea nao nitakucheki mkuu
 
Back
Top Bottom