system hacker
JF-Expert Member
- Mar 13, 2022
- 426
- 709
Kila mtu ana vitu vyake fulani hivi anavyovijua lakini watu wengi hawavijui.
Inaweza kuonekana kama vidogo lakini ni vikubwa mno kwa tafakuri ya kina. Au pengine watu wanajua lakini hawaipi kipaumbele stahiki. Hebu share nasi kwa kifupi sana!
Naanza mimi:
- Serikali halisi ni familia. Hizi Serikali za kisiasa ni kusanyiko la wapigaji tu. Kama viongozi wangetokana na maadili ya kifamilia kila Taifa lingekuwa bora kupita kawaida.
- Huwa hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya ama bahati nzuri. Kila kitu kimekuwa programmed mapema tu labda na Mungu ama shetani; lakini hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya ama kwa bahati nzuri.
Yaani vile ilivyo Tanzania ama Ulaya ama USA ni programmed years back. There is no way you can make Tanzania kuwa kama Ulaya ama USA kuwa kama Tanzania.
Dunia ina external force ambayo ni kubwa mara milioni kadhaa zaidi ya utashi wa mtu ama watu. Force hii ndio inaweka Dunia kwenye mstari wake. Ndio maana watu huzaliwa bila ridhaa yao hufa pia bila ridhaa yao.
- Sheria zozote ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya wakubwa. Wakubwa mara zote ni wachache ila wana nguvu. Wanyonge ni wengi ila hawana nguvu. Hakuna sheria ya kuwalinda watu wanyonge. Isipokuwa wakubwa wanaweka sheria ili kujilinda na wanyonge. Ndio maana wanaohubiri amani zaidi ni wakubwa sio wanyonge. Wanyonge hawana cha kupoteza, wakubwa wanachakupoteza. Na hii ndio hofu kuu ya wakubwa.
Tuendeleze hapo chini kama unavutiwa na mada kama hii.....